Rais Samia amesema tuwe na jamii yenye ujasiri wa kuhoji

Yale ya kupotea kwa kuhoji yamesha dhibitiwa🤔.Ama hivi sasa ni kutojibiwa na kuelekezwa kwa wazee wetu🤔
Serikali ya Rais samia haina mambo wala masuala ya kihuni huni na kishetani.ndio maana unaona watu wapo huru sana kuhoji na kukosoa kwa sababu uhuru upo wa kutosha kabisa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hayo ni maneno ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,simba wa nyika, komandoo wa vita,nyota ya matumaini Mama Samia Suluhu Hasssan katika maazimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Ambapo amesema kuwa tunapaswa kuwa na jamii yenye ujasiri wa kuhoji.

Naungana na kumuunga mkono mh Rais katika hili hasa kwa vijana. Kauli hii ni kama ile ambayo imewahi kutolewa na Hayati Baba wa Taifa ambaye yeye alisema tunapaswa kuwa na vijana jeuri wenye ujasiri wa kuhoji na kuwahoji viongozi wao.

Rais Samia Ndio maana amefanikiwa kuongoza Taifa likiwa limetamalaki kwa amani na utulivu ,kwa kuwa ametoa nafasi ya watu kuhoji masuala mbalimbali yanayoendelea nchini au kufanyika au kufanywa na serikali yake na kuwapatia majibu stahiki.kwa hiyo watu wanakuwa hawana dukuduku wala vinyongo katika mioyo na vifua vyao ,kwa kuwa mambo yanayoleta maswali kwao yanapatiwa majibu kwa wakati sahihi na hivyo kuwafanya watu kuwa na taarifa na uelewa au ufahamu wa kila kitu hapa nchini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Ni mnafiki kiwango cha lami...

Mwambie ivo yaani
 
Ni mnafiki kiwango cha lami...

Mwambie ivo yaani
Uwe na adabu na heshima kwa mh Rais wetu ,ambaye ametoa uhuru wa kutosha kwa watu kuzungumza watakavyo na kukosoa wawezavyo. Msitumie uhuru kwa kushusha heshima ya mtu au kuwadhalilisha wengine
 
Kwenye suala la Bandari mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania na nyota ya matumaini mh mama Samia na Serikali yake walitoa uhuru wa kutosha kwa watu, taasisi,vyama na wadau mbalimbali kutoa maoni yao na mwisho serikali yetu ilifanyia kazi maoni na mawazo yote muhimu na kuja na mkataba bora kabisa kuwahi kushuhudiwa katika Taifa letu.ambao utachochea ufanisi wa bandari yetu hasa katika masuala ya mizigo pale bandarini ,ambapo sasa haitakuwa inakaa sana kama awali ambapo ilikuwa inaongeza gharama kwa wenye mizigo.
-kwa nini wale jamaa walifunguliwa kesi,kusumbuliwa na kulazwa mung'anda kwa siku kadhaa?
-kwa nini mmoja alivuliwa ubalozi?
-hayo maoni yaliyochukuliwa lini?
-mrejesho ulitolewa lini?
-kwa nini leo hii watu wahimizwe maoni?
-what's cooking?
 
Mapishi bila shaka yatakuwa ubwabwa na choda
 
-kwa nini wale jamaa walifunguliwa kesi,kusumbuliwa na kulazwa mung'anda kwa siku kadhaa?
-kwa nini mmoja alivuliwa ubalozi?
-hayo maoni yaliyochukuliwa lini?
-mrejesho ulitolewa lini?
-kwa nini leo hii watu wahimizwe maoni?
-what's cooking?
Walifunguliwa kesi kwa kuwa walikuwa na makosa wanayotakiwa kuyatolea majibu jambo ambalo ni la kawaida kabisa. Pili mtu kuvuliwa ubalozi siyo geni wala siyo la kwanza.maana aliyevuliwa ubalozi hakuwa wa kwanza na hatakuwa wa mwisho.huwezi ukawa unatoa maneno ya kihaini halafu unataka ubaki na hadhi ya ubalozi
 
Wanatakiwa wamuangalie
Wakina steve wanachkua hela kiulaini
Na hakuna kazi yyt wanayofanya
Lucas Ana stahili chochote kitu kwa kweli

Ov
Watakwambia wale wanauzika ni celebrities sasa huyu ndiyo kwanza anasaka mtaji, angehamishia nguvu zake Kwa kugonga inbox zao uenda ipo siku wangempumzisha Kwa kacheo fulani . Afikiliwe kijana hata kama mmemjua kupitia JF.
 
Rais ni mnafik kiwango cha SGR
Ulihoji nini ukaminywa?

IMG-20231209-WA0028.jpg
 
Walifunguliwa kesi kwa kuwa walikuwa na makosa wanayotakiwa kuyatolea majibu jambo ambalo ni la kawaida kabisa. Pili mtu kuvuliwa ubalozi siyo geni wala siyo la kwanza.maana aliyevuliwa ubalozi hakuwa wa kwanza na hatakuwa wa mwisho.huwezi ukawa unatoa maneno ya kihaini halafu unataka ubaki na hadhi ya ubalozi
Nani alishawahi kuvuliwa ubalozi?
NB:Umejichagulia maswali ya kujibu.Hayo mengine unayaacha hovyo.Yang'atwe na mbu?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hayo ni maneno ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,simba wa nyika, komandoo wa vita,nyota ya matumaini Mama Samia Suluhu Hasssan katika maazimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Ambapo amesema kuwa tunapaswa kuwa na jamii yenye ujasiri wa kuhoji.

Naungana na kumuunga mkono mh Rais katika hili hasa kwa vijana. Kauli hii ni kama ile ambayo imewahi kutolewa na Hayati Baba wa Taifa ambaye yeye alisema tunapaswa kuwa na vijana jeuri wenye ujasiri wa kuhoji na kuwahoji viongozi wao.

Rais Samia Ndio maana amefanikiwa kuongoza Taifa likiwa limetamalaki kwa amani na utulivu ,kwa kuwa ametoa nafasi ya watu kuhoji masuala mbalimbali yanayoendelea nchini au kufanyika au kufanywa na serikali yake na kuwapatia majibu stahiki.kwa hiyo watu wanakuwa hawana dukuduku wala vinyongo katika mioyo na vifua vyao ,kwa kuwa mambo yanayoleta maswali kwao yanapatiwa majibu kwa wakati sahihi na hivyo kuwafanya watu kuwa na taarifa na uelewa au ufahamu wa kila kitu hapa nchini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Vipi kuhusu hayo maneno yake!! Safari hii hayajakata kiu ya Watanzania na kuifariji mioyo yao?
 
Back
Top Bottom