Rais Samia aiingiza Tanzania kwenye orodha ya nchi 10 tajiri Afrika 2021

Unamawazo mazuri Ila basics za uchumi hazitambui unachosema hapo, Ndio maana kipimo cha Utajiri ni GDP na sio GNP
Hazitambui kwa kuwa kuna nia ovu ya kupotosha.Niseme hivii, kipimo kizuri cha uchumi wa nchi kukua ni GNP,kutumia GDP kupima uchumi wa nchi kukua is "Rogue Economics." Kama wewe ni Economist wake up and see things in the right perspective,usikubali kudanganya.
 
Unabishana na Tarakimu?
Sibishani na tarakimu za GNP,zinaweza kuwa sawa.Ninachosema ni kwamba sio njia sahihi ya kupima ukuaji wa uchumi,naomba unielewe.
Kipimo kizuri cha uchumi kukua ni GNP mkuu sio GDP! Sisi tunataka Gross National Product ikue(GNP) na sio GDP(Gross Domestic Product), msidanganye watu.Kukua kwa GNP kuna maana kwamba wazawa ndio wanaotawala uchumi wa nchi.Kwa upande mwingine GDP kukua kuna maana moja tu,nayo ni kwamba tumeruhusu watu wa nje watawale uchumi wetu au tumeshaiuza nchi.This is bad news for our country.Sasa mali ya mtu amekuja kuiwekeza Tanzania,hii haisaidii sana mzawa.Tunataka mzawa akue, ndiye awe muwekezaji nchini mwake.Vikodi kodi hivyo na ajira si chochote,mzawa anabaki kuwa mtumwa tu.Nadhani wewe unatumiwa na maadui zetu kuwapa Watanzania a fake sense of security,kumbe wanakaangwa.
 
Kama Tanzania iko kwenye kumi bora kiuchumi na ndio tuko hivi! Basi umaskini wa Afrika ni balaa.
 
Back
Top Bottom