Rais Ruto atangaza kuanzia Januari 2024 matibabu Kenya ni bure.

Usahihi ni kwamba Kiwango cha bima kimepunguzwa kutoka Ksh. 500 hadi 300. Ila kwa wale wasio na uwezo kabisa ndio watapata tiba bure. Kwa hiyo sio kweli kwamba wananchi wote watatibiwa bure.
Hi ndiyo report sahihi. Ni nchi chache sana duniani ambapo halipi ibima ya afya hata senti moja.

Muhimu viwango viwe rafiki, wasio na kazi, uwezo watibiwe bure kama Kenya.

Pesa tupunguze kununua V8, misafara, semina, kongamano tuwekeze kwenye afya.
 
Hizo ni blah blah tu za wanasiasa wa kiafrika.
Kama wakenya hata milo mitatu kuipata ni shida sembuse huduma za afya bure kwa wote.

Hata hapa Tanzania kwa miongo kadhaa tumekuwa tukiambiwa mtoto (chini ya miaka 5), mjamzito na mzee matibabu ni bure, sasa njoo kwenye uhalisia ndio utashangaa.
 
Hiyo ndio Leadership sio ulaghai laghai huu wa hapa Nyumba ya Chawa.
 
Na Tanzania ije hii, swala la Afya ya mtu ni muhimu zaidi
Tanzania bado wanakukuruka na bima ya afya kwa wote.Ishu ya matibabu ni ya msing sana.Ila naona serikali nyingi za nchi za africa zimeanza kufanya biashara kwenye matibabu.Na wanafanya mazaha mwingi sana linapokuja suala la huduma za afya
 
Pesa wanazotafuna machawa wa mama tu zingetosha kugharimia afya kwa watu wengi mno,ila basi tu,sijaona chama kinachochukia wananchi wake kama hiki
 
Back
Top Bottom