Kwani mbeya hawana chuo kikuu?
..kuna chuo kikuu tayari.
..lakini watakuwa mabwege wakiichezea fursa hii iliyowaangukia.
..kuna mikoa na maeneo mengi hapa Tz yanamezea mate fursa ambayo Mbeya wameipata.
Kwani mbeya hawana chuo kikuu?
Harvard University ina eneo kubwa sana ambalo ni mji wao kabisa, lakini wenzetu hawana haja ya kuanzisha Constituent Universities kwasababu nchi ina uwezo wa kuanzisha vyuo vikuu vingine vikubwa. Sisi Tanzania hatuwezi tu kuanzisha vyo vikuu kama uyoga, hatuna rasilimali hizo. Ndiyo maana utakuta tuna wahadhiri wanafundisha vyuo zaidi ya viwili,....
Mtu hawezi kuwa bwege kiasi hicho, utakuwa ni uhujumu wa makusudi...kuna chuo kikuu tayari.
..lakini watakuwa mabwege wakiichezea fursa hii iliyowaangukia.
..kuna mikoa na maeneo mengi hapa Tz yanamezea mate fursa ambayo Mbeya wameipata.
What's your point anyway?Unaujua Jitegemee Sec,Makongo Sec ni ekari ngapi?
Mzumbe na MUST wanatoa kozi ambazo UDSM wanazitoa, mfano udaktari ???Mbeya tayari kuna vyuo vya serikali vya MUST na Mzumbe kwa nini visipanuliwe hivyo na viwe vikubwa kama UDSM badala ya kuendelea kuhamishia matawi ya vyuo vingine huko?
Jakaya ni mkuu wa UDSM anasemea chuo anachokiongoza.Msingependa kuwa na Kagera University?
Mtu hawezi kuwa bwege kiasi hicho, utakuwa ni uhujumu wa makusudi.
Inawezeka.Apo ata viwanja vya mpira ni ngumu kupata
Kwani mbeya hawana chuo kikuu?
sasa kuna nini kagera mzee, nipo hapa kagera hivi ninavyoandika niambie kuna nini nitoke nje niangalie. kitu gani wahaya mtasimama mbele za watu kuiambia dunia kuwa kagera ni bora kuliko maeneo mangine ya Tanzania? hata kumega wilaya zenu watengeneza chato ingefaa tu.Kagera siyo sitimbi, nchi inayopakana na nchi tatu utasemaje ni sitimbi?
Mzumbe na MUST wanatoa udaktari ???
Ulikuwa hufahamu ???UDSM inatoa udaktari?
Jakaya ni mkuu wa UDSM anasemea chuo anachokiongoza.
Ulikuwa hufahamu ???
Siku hizi ana sautiRais wa awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amekataa kupokea ekari 50 ambazo Serikali ya Mkoa wa Mbeya imezitoa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu cha Dar es Saalam kampasi ya Mbeya na kutaka wapewe eneo lenye ukubwa wa ekari 500 au 1,000.
Kikwete amesema kama mkoa huo hautawapa eneo wanalolihitaji watahamishia chuo hicho katika mkoa mwingine ambao utakuwa tayari kuwapa ardhi yenye ukubwa wanaouhitaji.
Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi, Novemba 27,2021 wakati wa mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Afya na Sayansi Shirikishi kampasi ya Mbeya yaliyofanyika jijini hapa.
Kikwete amesema hawawezi kukubali kupokea ekari 50 walizopewa kwakuwa chuo hicho kina hadhi kubwa hivyo wanahitaji ekari 500 hadi 1000 kwa ajili ya kujenga hosteli, makazi ya wahadhiri, wafanyakazi na hospitali.
Kauli hiyo ameitoa baada ya hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Mwanaidi Mtanda kusema kuwa ukosefu wa eneo kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili licha ya kuwasilisha maombi yao kwa Serikali ya mkoa tangu mwaka jana.
"Ingawa simuoni hapa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (Juma Homera) lakini naamini viongozi wa Mkoa watamfikishia ujumbe, tunaomba kiwanja tujenge chuo cha kisasa na hili lipewe kipaumbele" amesema Mwanaidi.
Mara baada ya hotuba hiyo, Kikwete amesema hawawezi kukubali kupokea ekari 50 walizopewa kwakuwa hazikidhi mahitaji yao
"Hii siyo sekondari kupewa ekari 50, tunataka eneo kubwa la ekari 500 hadi 1000 tenga hata kule Forest, mkishindwa tunahamia mkoa mwingine utakaoweza kutoa eneo kubwa, huu ni ujumbe kwa nyie viongozi" amesema Kikwete.
Kwahiyo hizi lawama unazielekeza kwa Serikali au JK?Chuo anachokiongoza kinaendeshwa pesa za serikali zinazotoka kwa raia wote wa nchi hii.
Hostel zikiwa nje ya chuo hiongeza costs za kuishi kwa wanafunzi,Muhimu wasilazimishe kutafuta hizo hekari 500 kwa kuwapora wanyonge ardhi yao, wakitaka kuzipata wawe tayari kuwalipa fidia wote watakaoathirika na hili wazo la Kikwete.
Sioni sababu kwanini wasijenge vitu vichache vya msingi kwa eneo lililopo, hizo nyumba za wahadhiri, hosteli, na hospitali vinaweza kuwa sehemu nyingine bora pasiwe mbali sana na chuo, kuliko kulazimisha vyote viwe pamoja kama chuo kimekuwa mbuga ya wanyama.
JK hajaanza leo kuongelea hili suala.Siku hizi ana sauti
Hoja yako ingekuwa na mantiki sana kama UDSM-Mbeya kingekuwa hakiwezi kujiendesha vizuri kama MUHAS. Lakini kinafanya vizuri na kimejaa wataalamu wabobezi kwenye udaktari. Hapa shida yako ni ipi haswa ???Kwa nini Muhimbili ambao wamebobea kwenye udaktari wasiende kufungua tawi huko huko badala UDSM?