Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Anna Nkya

Member
Oct 21, 2021
46
150
Rais wa awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amekataa kupokea ekari 50 ambazo Serikali ya Mkoa wa Mbeya imezitoa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu cha Dar es Saalam kampasi ya Mbeya na kutaka wapewe eneo lenye ukubwa wa ekari 500 au 1,000.

Kikwete amesema kama mkoa huo hautawapa eneo wanalolihitaji watahamishia chuo hicho katika mkoa mwingine ambao utakuwa tayari kuwapa ardhi yenye ukubwa wanaouhitaji.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi, Novemba 27,2021 wakati wa mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Afya na Sayansi Shirikishi kampasi ya Mbeya yaliyofanyika jijini hapa.

Kikwete amesema hawawezi kukubali kupokea ekari 50 walizopewa kwakuwa chuo hicho kina hadhi kubwa hivyo wanahitaji ekari 500 hadi 1000 kwa ajili ya kujenga hosteli, makazi ya wahadhiri, wafanyakazi na hospitali.

Kauli hiyo ameitoa baada ya hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Mwanaidi Mtanda kusema kuwa ukosefu wa eneo kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili licha ya kuwasilisha maombi yao kwa Serikali ya mkoa tangu mwaka jana.

"Ingawa simuoni hapa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (Juma Homera) lakini naamini viongozi wa Mkoa watamfikishia ujumbe, tunaomba kiwanja tujenge chuo cha kisasa na hili lipewe kipaumbele" amesema Mwanaidi.

Mara baada ya hotuba hiyo, Kikwete amesema hawawezi kukubali kupokea ekari 50 walizopewa kwakuwa hazikidhi mahitaji yao

"Hii siyo sekondari kupewa ekari 50, tunataka eneo kubwa la ekari 500 hadi 1000 tenga hata kule Forest, mkishindwa tunahamia mkoa mwingine utakaoweza kutoa eneo kubwa, huu ni ujumbe kwa nyie viongozi" amesema Kikwete.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,814
2,000
Muhimu wasilazimishe kutafuta hizo hekari 500 kwa kuwapora wanyonge ardhi yao, wakitaka kuzipata wawe tayari kuwalipa fidia wote watakaoathirika na hili wazo la Kikwete.

Sioni sababu kwanini wasijenge vitu vichache vya msingi kwa eneo lililopo, hizo nyumba za wahadhiri, hosteli, na hospitali vinaweza kuwa sehemu nyingine bora pasiwe mbali sana na chuo, kuliko kulazimisha vyote viwe pamoja kama chuo kimekuwa mbuga ya wanyama.
 

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,189
2,000
Hivi kwa nini wanaendelea kukipanua hiki chuo wakati wameshindwa hata ku manage na kutoa huduma bora kwa wanafunzi walionao. Kwa nini wasianzishe vyuo vipya vinavyojitegemea?

Nasikia ni mwezi sasa toka chuo kimefunguliwa ila mitandao yao ya usajili uko hovyo, wanafunzi wanasoma bila usajili.
 

Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,405
2,000
Muhimu wasilazimishe kutafuta hizo hekari 500 kwa kuwapora wanyonge ardhi yao, wakitaka kuzipata wawe tayari kuwalipa fidia wote watakaoathirika na hili wazo la Kikwete.

Sioni sababu kwanini wasijenge vitu vichache vya msingi kwa eneo lililopo, hizo nyumba za wahadhiri, hosteli, na hospitali vinaweza kuwa sehemu nyingine bora pasiwe mbali sana na chuo, kuliko kulazimisha vyote viwe pamoja kama chuo kimekuwa mbuga ya wanyama.
Sahihi, kama hazipatikani basi ni bora kusurrender kwa majirani zao Rukwa na Iringa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom