Rais Magufuli yashamshinda?

wMindi,pole sana vitabu vya dini...vinasema hudumia wengine ndio ujifikilie unaongelea maslahi ya waalimu ,madaktari zaidi kumbuka kuwa madaktari ,waalimu ni Rais amejitahidi anaboresha maslahi yao mfano waalimu na madaktari wamepewa kipaumbele kwenye mikopo na stahiki zao za masomo.Jpm amewaundia tume zao za kudumu kushughulikia matatizo yao,mishahara yao ni mizuli vilevile,nyumba na vitu vingine vinakuja taratibu,Mitaala na mazingira wazili anajitahidi sana usiku na mchana...
 
Naomba kifungu kwenye katiba kinacho zuia Mbunge wa Magu kwenda kuhutubia Kyela!Je vyama visivyo na wabunge na madiwani kama cha Mrema ina maana kimekufa?ACT ya Zitto na NCCR ina maana vitafifia?Sababu hawana wabunge zaidi ya Kigoma na Vunjo!CHADEMA haitakiwi kufanya siasa ZNZ Sababu haina diwani wala Mbunge huko

Rais kabla haja implement haya mambo yake ya hovyo hovyo abadili kwanza katiba
 
Jibu swali kwanza ndio uje na ngojera zako hapa,
mlivokaa mkamsema Lowasa ni Fisadi ule ulikuwa ukweli ama uwongo?
unless you are dummy ndio swali hili litakushinda.
 
Nitajie faida tano za kufanya siasa za maandamano kama wewe sio mbunge au muwakilishi wa eneo husika sababu hizo ziwe tofauti kujadili faida za kiuchumi na kijamii@ malafyale
 
Katika utawala wa Rais Magufuli, tutasikia sana prophecies of doom!
 
mlisema Kikwete hatamaliza mda wake wa urais lkn leo ni rais mstaafu tena kastafu kwa Heshima.
hizi kelele zenu tushazizoea. Magufuli anazidi kuchanja mbuga,
Akielekea Serengeti au Mikumi?
 
Jibu swali kwanza ndio uje na ngojera zako hapa,
mlivokaa mkamsema Lowasa ni Fisadi ule ulikuwa ukweli ama uwongo?
unless you are dummy ndio swali hili litakushinda.
Endelea kumtaja kwa sifa na mapambio. Kwani hiyo mahakama yenu bado? Mpelekeni muone mtakavyojiharishia. Huyo boss wako hatii mguu hapo kwa jinsi palivyo juu ya uwezo wake. Jibu unalo sasa kuwa siyo fisadi ni malaika mwelekezaji. Na hashtakiki.
 
We nawe usituchoshe bwana, slaa slaa. Km unahamu naye si umfuate huko canada.
Chama ni taasisi haiwexi kufa kisa mtu au kikundi cha watu wamekimbia kwa maslai yao binafsi
 
Haya maneno mlisha yasema wakati wa jk, jamaa akamaliza muda wake bila tabu. Sasa mnayarudia, tatizo lenu mnafikiri hapa ni south sudan
Usisema bilataabu mkuu, nafikiri tuliyenaye amepatka kwa sababu ya taabu alizozipata jk
 
Endelea kumtaja kwa sifa na mapambio. Kwani hiyo mahakama yenu bado? Mpelekeni muone mtakavyojiharishia. Huyo boss wako hatii mguu hapo kwa jinsi palivyo juu ya uwezo wake. Jibu unalo sasa kuwa siyo fisadi ni malaika mwelekezaji. Na hashtakiki.
kwa hiyo si Fisadi ni Malaika sasa ivi tokea aje Chadema si ndio..?
 

..thanks.

..cdm inahitaji katibu mkuu mwenye ambition na mkakati wa kujenga
chama.

..tulikosea kumwachia Dr.Slaa afanye kila kitu na wengine wakabaki kama cheer leaders tu.

..katibu mkuu aunde TIMU ya kukipeleka chama mbele.

..pia cdm isijielekeze kwenye uraisi peke yake. Tupeleke nguvu kwenye serikali za mitaa na ubunge.
 
nchi Hamna vision, ni one man show
jámaa anapenda sana kusifiwa tu.... wasaidizi wakewamejaa Uwoga kupindukia
sijaribiwi....
 
Nyani Ngabu urais ni taasisi ukimuona rais anatoa maamuzi ujue information zote anazo
Just for clarification
Hivi na swala la sukari alishauriwa sio.. bila kuona implications yake kwa sasa na hapo baadae..
Je maswala mbalimbali anayoongea na kesho yake kutenguliwa kauli nayo tusemeje kuwa hawakujiandaa.. au
Nakwama kuelewa hapa..
 
Hii ni hoja ambayo Watanzania wengi hawaioni.
Na wala hawaoni hatari ya ku entertain mambo kama haya.

1. Hakuna sheria yoyote ya nchi inayozuia mikusanyiko halali ya wananchi
Katiba imeeleza wazi, na kusisitiza hilo katika eneo la siasa sheria za msajili wa vyama vya siasa imeeleza taratibu za mikusanyiko. Sheria ilipitishwa na bunge na kuridhiwa na Rais

2. Hakuna sheria inayozuia kufanya siasa, au inayoelekeza nyakati za kufanya siasa.
Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ipo 24/7 , 365. Hivyo siasa ni tendo endelevu

3. Hakuna sheria inayozungumzia msimu wa siasa.
Hakuna sheria inayompa mamlaka yoyote yule kupanga msimu wa siasa

4. Jukumu la wanasiasa majimbo kama wabunge ni la wananchi.
Kama mbunge hawatekelezi wajibu, wenye jukumu la kumwadhibu kupitia sanduki la kura ni wananchi. Serikali haina nguvu zozote za kisheria za kumbana mbunge

5. Kuzuia au marufuku ya kufanya siasa eneo jingine ni kuua shughuli za siasa.
Ina maana mtu asiye mbunge hawezi kufanya siasa kwasababu hana eneo.

Hilo ni kuua vyama vya siasa, na kwenda kinyume na katiba inayotambua uwepo wake, inayotoa fursa za vyama.

6. Ili kutekeleza agizo la marufuku na kulipa uhalali wa kisheria, Serikali ipeleke mswada bungeni. CCM ni wengi mswada ukipita sote lazima tuuiti.

Bila kuwa na sheria tamko hili halina nguvu za kisheria na kama zipo tuonyeshwe

7. Kuna nafasi, ikiwa mswada utakuwa na uchelewaeshaji au ikiwa marufuku yanaambatana na sababu nyingine kama usalama, watu wafanye kazi n.k , Rais ana nafasi ya kusaini executive order ili tamko lake liwe na nguvu ya kisheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…