Rais Magufuli yashamshinda?

Rais Magufuli yashamshinda?

Siyo kweli, Ccm hawapo tayari kuachia madaraka hata Wapinzani wakishinda, hilo lipo wazi, wakiachia watakula wapi ilhali madaraka ndiyo shamba lao miaka yote.
Upinzani madhubuti unahitajika regardless kama CCM wataachia madaraka au la
Kwa sasa upinzani Bara hamna!ZNZ ndiyo kuna upinzani sana
 
Kabla Magufuli hajawa Rais nilikuwa na mashaka mashaka huenda zile speed zake za kukamata samaki za wachina zikakwamishwa ndani ya CCM atakapo pata Urais. Kwa mtazamo wangu Rais Magufuli anafanya kazi zake vizuri na kwa uhakika kabisa. Mambo mengine hayahitaji kupanga. Kipindi cha Kikwete tulikuwa tuli ongea sana kwamba hapati muda wa kupita kwa wananchi na kuona hali halisi ya maisha. Leo hii Magufuli anafanya hayo. Na akipita akikuta/ akipata taarifa kwamba kuna mambo hayaedi vizuri yeye kama Rais anayo mamlaka ya kufanya mabadiliko mara moja. Leo hii tumeona Bodi ya Pamba itahamishwa kutokana na ziara zake za karibuni, Kesho tutasikia kingine kwa manufaa ya Taifa na wananchi. Tufike mahala tumshukuru mungu kwa kumpa ujasiri Mh. Rais. Tuwekeni siasa pembeni, tu focus tunataka maisha ya namna gani na tuangalie ni nini rais anafanya na ni nani angekuwa na uthubutu kama wake. Leo hii mama yangu mzazi aliyekuwa anasumbuliwa kwa hati ya kiwanja chake kule kijijini kwa zaidi ya miaka 4 hati ile kaipata mwezi wa sita mwaka huu. Mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na sisi wengine tuonyeshe uzalendo kwa nchi yetu. Mwenye kupinga au kudharau kazi na maamuzi ya Rais kwa sasa huyo atakuwa si mwenzetu. Unapo jenga nyumba mpya ili kuhamia humo kuna mambo mengi kabisa ambayo kwa njia moja au nyingine yatakuwa ya shida shida na maudhi ambayo utapitia kabla ya wewe kuishi kwa amani na kuenjoy maisha ndani ya nyumba hiyo. Mwanzo ni mgumu. Nchi hii ilikuwa imeoza. Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki RAIS na wananchi wake wenye kuamini mabadiliko.
 
Habari wadau,

Ingawa ana muda mfupi madarakani lakini nimejaribu kumfuatilia Magufuli na kugundua kuwa itamchukua muda mrefu sana kutulia na kuanza mission za maendeleo ya nchi yetu.

Magufuli ni mtu mwenye kujiamini, lakini hadi sasa haamini kuwa yeye kachaguliwa kuwa RAIS wa nchi hii. Badala ya kukaa na kuwa makini na majukumu yake, bado anatumia muda kujionesha na kutangaza kuwa yeye ni Rais, wakati tayari ana wadhifa huo.

Zipo kauli kadhaa ambazo hazihitajiki kuzitamka, mfano;

1.Mimi ndio Rais nikihamia Dodoma watanifuata wote vinginevyo hawapati mishahara au waache kazi (Utadhani kuna aliembishia)
2. Siamini kama leo wewe Kikwete ungeniomba pesa za ukarabati wa chuo maana wewe ulikuwa Rais
3. Nikihamia Dodoma nyumba zote za serikali zilizoko Dar es salaam nitaziuza ( Utadhani za familia yake)
4. Mimi ndio mkuu wa Sumatra nchi nzima

Ukitizama kauli hizo chache utagundua kuwa bado Magufuli hajatulia, badala yake anatumia muda mwingi kuonesha Power yake, au kutaka sifa

Jambo lingine; Magufuli anaangaika na "audience", kwamba watu wanasemaje?, au nini kinawafurahia kusikia?, ndio maana mahamuzi mengi anafanya kwa pupa hili ashangiliwe na wananchi.

Mimi naamini kama hasipoacha tabia za kuonesha kuwa yeye ndie mwenye "POWER" na sifa ambazo hazina msingi atajikuta miaka 2 au 3 imepita na hakuna alilofanya. Matokeo yake itakuwa kama wakati ule ambapo wana wa Izrael walitamani kurudi Misri, kwamba bora kule tulikuwa watumwa lakini tulikuwa tunakula na kunywa. Yaani wananchi wataona bora turudi enzi za Kikwete.
 
Ukiwa na mtazamo kama huu ni dhahiri unahitaji miaka kama sitini zaidi kufikia ilipo Uganda au miaka 70 kufikia ilipo Kenya na karne kama saba kufikia ilipo Singapore.
Hivi ni kweli kwamba 'DJ' ndiye alikuwa mwenyekiti au mjumbe wa baraza la mawaziri lililopitisha uamuzi wa kujenga nyumba za mawaziri Mikocheni pamoja na headquarters za mawizara yote!?
Je, ni 'dj' aliyesimamia ununuzi wa uniforms hewa na kulipa billion 60, wizi wa makontena na flow meter bandarini!?
Na ni 'dj' aliyeahidi 'kuwalinda' ...(wino wa kuandika umeniishia)
Unadhani wakioshapewa buku 7 zao wanawaza yote hayo basi? Wao ni kutetea na kumeza kila kinachotamkwa na serikali bila kufanya analysis
 
Hivi ni mimi tu au na wengine mpo mnaoona kama vile mambo yashamshinda huyu Magufuli?

Kuna hali fulani hivi naiona ambapo jamaa ni kama anaamka tu kila asubuhi na kutoa maamuzi ya kukurupuka kurupuka.
Yaani yeye ni amri tu....fanya hivi....fukuza huyu....twende kule...nk.

Yapo baadhi ambayo ni mazuri ambapo mtu unaona kabisa hapa nia ni nzuri lakini kuna mengine yenye ukakasi sana hadi kunifanya nianze kuhoji hekima na busara za huyo bwana!
ktk maisha kuna uzuri na ubaya ila kazidi kidogo
 
Rais ni Magufuli na ataendelea kuwa magufuli. huko anakopita ni shangwe na vigelegele. wananchi wanatamani aseme neno roho zao zifrahi. huku mko busy kutunga ngonjera na hadithi zisizo na vichwa wala miguu......
Hujui ulisemalo
 
Kitu kibaya kabisa ni kuendelea kutazama tu bila kujishughulisha.Hii ndiyo furusa ya kushamiri kwa kutekeleza yale yote uliyokuwa unataka kufanya kipindi cha nyuma kwa ajili ya maendeleo yako, familia yako na Taifa kwa ujumla . Ni kwa awamu hii kama unajambo jema kwa taifa linaloweza kuibua furusa za wananchi kujijengea uwezo wa kujitegemea unaweza kusikilizwa kwa urahisi.
Badala ya kuendelea kunakili tu maelekezo ya rais anayoyatoa, sasa tuyafanyie kazi kwa nia ile ile ya kuhakikisha Tanzania inakuwa ya viwanda na inayojitegemea kiuchumi na kijamii.
 
Kauli zake hizi Dr Rais Magufuli tumuiteje?
Usiogope wewe
Beleshi iitwe Beleshi wala sio Kijiko kikubwa
"Mikutano ya kisiasa hadi 2020"
Lkn yy anafanya mikutano
DIKTETA UCHWARA huyu
Malafyale ,wewe hujui hata unachokisema waliofanya mkutano Tunduma jana mbona hawajazuiliwa,Tatizo unaongea bila kujitathimini,Rais ni mbunge wa Tanzania nzima,na kila mbunge anatakiwa kuhudumia watu wake..wewe Malafyale huwezi kutoka eneo lako la mbeya kufanya mikutano mwanza,utakuwa huwatendei watu wako haki.Kaa kituo chako cha kazi Fanya kazi na wananchi waliokuchagua,Tatizo la wabunge walikuwa wamebweteka hawaendi majimboni mwao kazi kula mishahara bila jasho ikikaribia uchaguzi hao...kama mvua,hataree...
 
Kitu kibaya kabisa ni kuendelea kutazama tu bila kujishughulisha.Hii ndiyo furusa ya kushamiri kwa kutekeleza yale yote uliyokuwa unataka kufanya kipindi cha nyuma kwa ajili ya maendeleo yako, familia yako na Taifa kwa ujumla . Ni kwa awamu hii kama unajambo jema kwa taifa linaloweza kuibua furusa za wananchi kujijengea uwezo wa kujitegemea unaweza kusikilizwa kwa urahisi.
Badala ya kuendelea kunakili tu maelekezo ya rais anayoyatoa, sasa tuyafanyie kazi kwa nia ile ile ya kuhakikisha Tanzania inakuwa ya viwanda na inayojitegemea kiuchumi na kijamii.
Umenena kweli ndugu,tuige.mifano ya wachina,wahindi na wazungu wao huwa wanafanya kazi kwa bidii.mtu anaetaka maendeleo hafikilii hata siku kuangalia mbowe na wenzake wataongea nini.Nimempongeza mbunge mwakanjoka jinsi alivyofanya jana wananchi wanaondoa nyumba zao kupisha barabara kwa hiayari hiyo ndio kazi anatakiwa kusimama mbunge.Uchumi haujengwi kwa majungu ...ukiwa unaipiga CCM majungu wao wanazidi kusonga mbele.
 
Hivi unaujua ukweli wewe ? mlivokaa mkamsema Lowasa ni Fisadi ule ulikuwa ukweli ama uwongo?
Nanyi juzi kwenye mkutano wenu wa kupeana kiti mlimwitaje? Malaika! Mlimtaja mara nyingi na mtaendelea kumtaja mara nyingi kuliko mnavyolitaja jina la Mungu wenu. Wakurupukaji wakubwa ninyi msiokuwa na ubunifu zaidi ya kuvisubiri vichwa vibuni ili ninyi vilasa mliopindukia m-cut na kupaste. Akili ya kasuku nyie.
 
CHADEMA ingekuwa imara kama zamani huyu easily angeondoka 2020
Lkn kwa upinzani huu wa hovyo hovyo wa kutowasikiliza wanachama na kujiona viongozi kama Mungu watu
Wapinzani wanawatumia wanachama wao kwenye maadamano tu
Kwenye teuzi wanapuuzi kauli za wanachama wa kawaida
Wao na CCM hamna tofauti
Magufuli atashinda 2020 hata kukiwa na TUME HURU
Mark my words
Mkuu nani aliyekupuuza?
 
Back
Top Bottom