Rais Magufuli yashamshinda?

Rais Magufuli yashamshinda?

mlisema Kikwete hatamaliza mda wake wa urais lkn leo ni rais mstaafu tena kastafu kwa Heshima.
hizi kelele zenu tushazizoea. Magufuli anazidi kuchanja mbuga,

hahahaha! eti kwa heshima! wakat huyu aliyechukua kijiti analilia kaachiwa nchi imeoza! kuozesha nchi ndo heshima?!
 
Mimi kila siku naomba asifike kituo cha mabasi cha Ubongo saa kumi na mbili asubuhi. Maana akiona mabasi yanavyokwenda mikoani na idadi kubwa ya wasafiri, anaweza kusema " Marufuku mabasi kuondoka Dar, watu wote hawa wakiondoka nani atafanya kazi?"
 
Mimi kila siku naomba asifike kituo cha mabasi cha Ubongo saa kumi na mbili asubuhi. Maana akiona mabasi yanavyokwenda mikoani na idadi kubwa ya wasafiri, anaweza kusema " Marufuku mabasi kuondoka Dar, watu wote hawa wakiondoka nani atafanya kazi?"

Hahaaaaa jamaa ana mambo mengi sana kwa kweli.
 
tena atashinda kwa kura nyingi mnoo. hawa wapinzani hawana ajenda pumzi imekata mapema sana. wamebaki kufanya siasa za kinafiki mitandaoni
Kwani Cuba wana vyama vingapi na wana maisha gani? Hata Tanzania tutarudi kwenye chama kimoja na tutakuwa na maisha mazuri sana kama Cuba hakuna shaka. Demokrasia haiji kwa kulazimisha inabidi watu wawe tayari ama sivyo ufalme uendelee. Usiwe na shaka.
 
Yapo baadhi ambayo ni mazuri ambapo mtu unaona kabisa hapa nia ni nzuri lakini mengine yana ukakasi kidogo.


Sasa mbona unauliza na kujijibu mwenyewe? Kwani ulitegemea yawe mazuri kwa 100% ? Hata yeye Raisi Magufuli si ni binadamu tu kama wengine ambaye pia hufanya mazuri na pengine hukosea pia kama mimi na wewe tulivyo?
 
Ukipita mitaani watu washachoka na story zake...
biashara haziendi.....mood iliyopo ni kusubiri labda mambo yatanyooka soon...
sasa sijui yasiponyooka itakuaje....

Mitaa ipi hiyo unayoiongelea?
 
Hivi ni mimi tu au na wengine mpo mnaoona kama vile mambo yashamshinda huyu Magufuli?

Kuna hali fulani hivi naiona ambapo jamaa ni kama anaamka tu kila asubuhi na kutoa maamuzi ya kukurupuka kurupuka.

Yaani yeye ni amri tu....fanya hivi....fukuza huyu....twende kule...nk.

Yapo baadhi ambayo ni mazuri ambapo mtu unaona kabisa hapa nia ni nzuri lakini mengine yana ukakasi kidogo.

Tatizo kubwa sana ninaloliona ni kwamba Rais wetu hana mpangilio katika kufanya kazi zake. kwa mfano, aliamua kushughulikia tatizo la vitanda katika Hospitali. Ni kweli vitanda ni tatizo kubwa na linahitaji ufumbuzi. lakini je, katika muktadha wa afya na matibabu, ukosefu wa vitanda ndio tatizo namba moja? uwepo wa vitanda utapunguza vifo katika hospitali zetu kwa kiwango kikubwa? maana kuna matatizo ya vifaa tiba, kuna matatizo ya madaktari na wauguzi, na juu ya yote kuna matatizo ya mfumo. mfano kama hospitali za chini zinaimarishwa, maana yake mrundikano utapungua Muhimbili.

Katika Elimu, pamoja na matatizo lukuki yaliyopo katika sekta hii: ubovu wa mitaala, matatizo ya walimu, nyumba za walimu, madarasa, maabara, madawati, na mengine mengi, yeye akakomaa na madawati. ni kweli ni moja ya matatizo, lakini je, linaweza kuleta mabadiliko makubwa, impact kubwa katika elimu kama likitatuliwa kwanza hilo?

Kukosa mpangilio kunakuja pia katika maamuzi. ana utaratibu wa kutoa maamuzi ya ghafla. bila mpango, bila bajeti. mfano mzuri ni hii amri ya Serikali kuhamia Dodoma. haijulikani kama kuna tathmini imefanyika kuona impact ya kuhamia ghafla namna hii.

Mwendo wa namna hii matokeo huwa baadaye ni kujikuta umesababisha matatizo mengi kuliko unavyoweza kuyakabili. JK alikuwa na kawaida ya kupaa kwenda majuu mambo yanapomzidia. Magu yeye atakuwa na kautaratibu gani ili angalau apumue? kutumbua majipu zaidi?
 
Back
Top Bottom