Sisi kama Raia wema tuna wajibu wa kukumbushana pale tunapoona Taifa letu pendwa linataka kudidimia kutokana na Uroho wa madaraka wa baadhi ya wagombea ambao tayari wako madarakani.
Rais Magufuli bado ni Amir Jeshi Mkuu mpaka hapo tar 28 siku ya uchaguzi na mpaka kuapishwa kwa Rais mpya tar 30 October au tarehe nyingineyo.
Wakati huo huo Mgombea wa kiti cha urais huko zanzibar kwa tiketi ya CCm Dr Husseni Mwinyi akiwa ni Waziri wa Ulinzi Muungano na akiwa bado ana link na infuluence kubwa ndani ya chombo nyeti cha ulinzi na usalama wa nchi.
Lakini pia Kabla ya kifo chake Hayati Ben Mkapa miezi michache kabala aliandika kitabu kilichosheheni historia yake kiliitwa " My life my Purpose". Kwa maandishi na kauli yake mwenyewe alikiri kusikitishwa na kuumizwa na kitendo kilichotokea huko zanzibar mwaka 2000 wakati wa uchaguzi ambapo watanzania wazanzibar mamia walipoteza maisha na maelfu kuwa wakimbizi wa ndani na nje ya tanzania.
Ingawa alikiri kuwa si yeye aliyetoa amri kwa vikosi vya kijeshi kupiga nakuumiza Raia wake ndani ya kisiwa cha zanzibar lakini alikiri kuwa anawajibika kwa makosa makubwa yaliyofanyika wakati wa utawala wake.
Hivi karibuni wakati kampeni zikiwa zinaendelea na hadi sasa tunashuhudia mambo kama yale aliyojutia hayati Ben kama yanataka kujirudia. Tunaona mamia kwa mamia ya vikosi vya kijeshi ktk viunga mbali mbali ndani ya kisiwa cha zanzibar. Hali hii imeleta hofu kubwa. Watu wanajiuliza je yale ya 2000 yatajirudia tena kama sivyo huu wingi wa majeshi yetu ni kwa sababu gani. Je Rais Magufuli anataka kurudia makosa yale yale ya Ben Mkapa??
Tafadhali sana. Majuto ni mjukuu. Tendeni haki uchguzi huu wananchi wapige kura kwa uhuru na mshindi atangazwe kwa haki.
Una urais wa miaka 10 tu kama utaupata baada ya hapo utaisha atakuja mwingine. Utajuta kupoteza maisha ya watanzania kwa kitu ambacho utakaa nacho kwa miaka mitano tu. Majuto utakaa nayo maisha yako yote ya uhai wako.
Mwinyi na Rais Magufuli jifunzeni kwa Mkapa.