Uchaguzi 2020 Rais Magufuli, Waziri Mwinyi na Vyombo vya usalama vimejipangaje kuepuka Majuto kama Yale ya Mkapa kwenye Confession yake "My life my Purpose"?

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
15,886
2,000
Sisi kama Raia wema tuna wajibu wa kukumbushana pale tunapoona Taifa letu pendwa linataka kudidimia kutokana na Uroho wa madaraka wa baadhi ya wagombea ambao tayari wako madarakani.

Rais Magufuli bado ni Amir Jeshi Mkuu mpaka hapo tar 28 siku ya uchaguzi na mpaka kuapishwa kwa Rais mpya tar 30 October au tarehe nyingineyo.

Wakati huo huo Mgombea wa kiti cha urais huko zanzibar kwa tiketi ya CCm Dr Husseni Mwinyi akiwa ni Waziri wa Ulinzi Muungano na akiwa bado ana link na infuluence kubwa ndani ya chombo nyeti cha ulinzi na usalama wa nchi.

Lakini pia Kabla ya kifo chake Hayati Ben Mkapa miezi michache kabala aliandika kitabu kilichosheheni historia yake kiliitwa " My life my Purpose". Kwa maandishi na kauli yake mwenyewe alikiri kusikitishwa na kuumizwa na kitendo kilichotokea huko zanzibar mwaka 2000 wakati wa uchaguzi ambapo watanzania wazanzibar mamia walipoteza maisha na maelfu kuwa wakimbizi wa ndani na nje ya tanzania.

Ingawa alikiri kuwa si yeye aliyetoa amri kwa vikosi vya kijeshi kupiga nakuumiza Raia wake ndani ya kisiwa cha zanzibar lakini alikiri kuwa anawajibika kwa makosa makubwa yaliyofanyika wakati wa utawala wake.

Hivi karibuni wakati kampeni zikiwa zinaendelea na hadi sasa tunashuhudia mambo kama yale aliyojutia hayati Ben kama yanataka kujirudia. Tunaona mamia kwa mamia ya vikosi vya kijeshi ktk viunga mbali mbali ndani ya kisiwa cha zanzibar. Hali hii imeleta hofu kubwa. Watu wanajiuliza je yale ya 2000 yatajirudia tena kama sivyo huu wingi wa majeshi yetu ni kwa sababu gani. Je Rais Magufuli anataka kurudia makosa yale yale ya Ben Mkapa??

Tafadhali sana. Majuto ni mjukuu. Tendeni haki uchguzi huu wananchi wapige kura kwa uhuru na mshindi atangazwe kwa haki.

Una urais wa miaka 10 tu kama utaupata baada ya hapo utaisha atakuja mwingine. Utajuta kupoteza maisha ya watanzania kwa kitu ambacho utakaa nacho kwa miaka mitano tu. Majuto utakaa nayo maisha yako yote ya uhai wako.

Mwinyi na Rais Magufuli jifunzeni kwa Mkapa.
 
Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
618
1,000
Solution ya mwaka 2010 kuacha Mpemba aiongoze Zanzibar ilikuwa akili kubwa sana imetumika kwa CCM, bahati mbaya haiwezi kudumu miaka yote. Kuna haja ya kutafuta suluhisho kuepusha shari za kila chaguzi Zanzibar.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
51,839
2,000
Solution ya mwaka 2010 kuacha Mpemba aiongeze ilikuwa akili kubwa sana imetumika kwa CCM, bahati mbaya haiwezi kudumu miaka yote. Kuna haja ya kutafuta suluhisho kuepusha shari za kila chaguzi Zanzibar.
Viongozi wote wa CCM walikua na unafiki uliotupoza kidogo lakini Magufuli hakuweza hata unafiki ametupa mateso mwanzo mwisho.

CCM kuondoka ni katika uchaguzi huu, wamekataa kuondoka kwa kheri wataondoka kwa shari.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
15,886
2,000
Solution ya mwaka 2010 kuacha Mpemba aiongoze ilikuwa akili kubwa sana imetumika kwa CCM, bahati mbaya haiwezi kudumu miaka yote. Kuna haja ya kutafuta suluhisho kuepusha shari za kila chaguzi Zanzibar.
Solution ni Tume huru Ya ZEC ili kuepushe malalamiko ya pande zote mbili.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
15,886
2,000
Viongozi wote wa CCM walikua na unafiki uliotupoza kidogo lakini Magufuli hakuweza hata unafiki ametupa mateso mwanzo mwisho.

CCM kuondoka ni katika uchaguzi huu, wamekataa kuondoka kwa kheri wataondoka kwa shari.
Kwa kweli kama wanajianda kufanya yale ya mwaka 2000 basi wajiandae kwa majuto maisha yao yote.
 
Mnyapesimeka

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
7,871
2,000
Viongozi wote wa CCM walikua na unafiki uliotupoza kidogo lakini Magufuli hakuweza hata unafiki ametupa mateso mwanzo mwisho.

CCM kuondoka ni katika uchaguzi huu, wamekataa kuondoka kwa kheri wataondoka kwa shari.
Kweli kabisa kimsingi CCM hapana ikataliwe nchi nzima.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
51,839
2,000
1603752180136.png
 
USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,458
2,000
Atakaye leta upuuzi atadhibitiwa tu
Sisi kama Raia wema tuna wajibu wa kukumbushana pale tunapoona Taifa letu pendwa linataka kudidimia kutokana na Uroho wa madaraka wa baadhi ya wagombea ambao tayari wako madarakani.

Rais Magufuli bado ni Amir Jeshi Mkuu mpaka hapo tar 28 siku ya uchaguzi na mpaka kuapishwa kwa Rais mpya tar 30 October au tarehe nyingineyo.

Wakati huo huo Mgombea wa kiti cha urais huko zanzibar kwa tiketi ya CCm Dr Husseni Mwinyi akiwa ni Waziri wa Ulinzi Muungano na akiwa bado ana link na infuluence kubwa ndani ya chombo nyeti cha ulinzi na usalama wa nchi.

Lakini pia Kabla ya kifo chake Hayati Ben Mkapa miezi michache kabala aliandika kitabu kilichosheheni historia yake kiliitwa " My life my Purpose". Kwa maandishi na kauli yake mwenyewe alikiri kusikitishwa na kuumizwa na kitendo kilichotokea huko zanzibar mwaka 2000 wakati wa uchaguzi ambapo watanzania wazanzibar mamia walipoteza maisha na maelfu kuwa wakimbizi wa ndani na nje ya tanzania.

Ingawa alikiri kuwa si yeye aliyetoa amri kwa vikosi vya kijeshi kupiga nakuumiza Raia wake ndani ya kisiwa cha zanzibar lakini alikiri kuwa anawajibika kwa makosa makubwa yaliyofanyika wakati wa utawala wake.

Hivi karibuni wakati kampeni zikiwa zinaendelea na hadi sasa tunashuhudia mambo kama yale aliyojutia hayati Ben kama yanataka kujirudia. Tunaona mamia kwa mamia ya vikosi vya kijeshi ktk viunga mbali mbali ndani ya kisiwa cha zanzibar. Hali hii imeleta hofu kubwa. Watu wanajiuliza je yale ya 2000 yatajirudia tena kama sivyo huu wingi wa majeshi yetu ni kwa sababu gani. Je Rais Magufuli anataka kurudia makosa yale yale ya Ben Mkapa??

Tafadhali sana. Majuto ni mjukuu. Tendeni haki uchguzi huu wananchi wapige kura kwa uhuru na mshindi atangazwe kwa haki.

Una urais wa miaka 10 tu kama utaupata baada ya hapo utaisha atakuja mwingine. Utajuta kupoteza maisha ya watanzania kwa kitu ambacho utakaa nacho kwa miaka mitano tu. Majuto utakaa nayo maisha yako yote ya uhai wako.

Mwinyi na Rais Magufuli jifunzeni kwa Mkapa.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
15,886
2,000
Atakaye leta upuuzi atadhibitiwa tu
Ben sasa hivi analiwa na Mende na Minyoo ya ardhini. Amevuna nini? Utawala miaka mitano sinuliisha?? Urais kaenda nao kuzimu?? Sasa hivi anawaka kama kuni kwenye tanuru. Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu kweli kweli.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom