Rais Magufuli: Watendaji wangu wananichelewesha. Naomba chama changu CCM kinisaidie kuwasukuma, tumechelewa!

Rais ndiye anayewateua kwa utashi wake, sasa wakimchelewesha wananchi wa kawaida tunahusikaje? Pili kuamini kuwa chama kitasaidia, akumbuke wakati chama kilikuwa na makatibu wake kwenye mashirika ya umma nini kilitokea.
 
Na bado, tulianza kukanyaga Sheria za nchi kwamba zinatuchelewesha, tukaja wapinzani, Sasa tupo na wale tuliowateua wenyewe,mpaka tuje tujue tatizo ni Nani tutakuwa tumeharibu nchi yetu sana
 
Mzee ulituambia kuwa mbowe na genge lake (wapinzani) ndio walikuwa wanakuchelewesha kutuletea maendeleo, ukatuambia tusikuchanganyie magunzi kwenye kurunzi. Sasa mbona tena tumeweka betri tupu lakini malalamiko yanaendelea?
Hapo chacha😆😆
 
Rais Magufuli amesema kuwa Rais ni kazi ngumu sana kwa sababu wewe unaweza kupanga mipango hii kumbe wenzako nao wana mipango mingine...
He! C tuliambiwa wapinzani ndio wanachelewesha maendeleo? Imekuwaje tena watendaji wake mwenye uwezo wa kuwawajibisha muda wowote ule?

Mtatafutana nasa wenyewe kwa wenyewe!!
 
Kumbe sio wapinzani wanaochelewesha maendeleo!
Hii nchi ni ya ajabu sawa kuwahi kutokea dunia!!leo yamekuwa hayo tena?toka ameingia madarakani ameshafukuza wangapi?mbona mambo bado ni yale yale tu?

Watendaji wameacha kufuata taaluma zao zinawaongoza kufanya nini, bali mwanasiasa anataka kifanyike nini!!mfano juzi nimemuona mwenyekiti wa ccm, wa wilaya anamshinikiza injinia kuwa baada ya siku tatu nataka hili daraja magari yaaanze kupita, ole wako nirudi siku hiyo nikute bado, polisi mnasikia aje akamatwe, kazi hiyo anayozungumizia , zisukwe nondo, imwage zege , si chini ya wiki nne!!
 
Ulisema upinzani unakuchelewesha, ukaamuru Nec wakuletee wabunge wa ccm majimbo yote , umeona umeshindwa umeanza kusingizia wateule wako.

Ukutegemea usimamizi wa chama chako kwa wateule wako hilo litakuwa anguko lako. Yaani mwenyekiti wa chama wa mkoa akague miradi ya serikali!

Hilo lilimshida Nyerere,wewe unataka kulirudia tena. Imarisha taasisi za serikali, Kama mahakama, Takukuru, Polis na Tiss zipe nguvu ya kisheria kuweza kuchunguza na kushitaki, siyo kusubiri waambiwe chunguzeni pale au mradi mradi fulani.

Taasisi ziwe huru zisiwe chini ya CCM. Taasisi hizi zifuatilie miradi yote na matumizi ya pesa pale wanapogundua ufujaji wachukue hatu za kisheria.

Huo diyo ushauri wangu kwako.
 
Ni mtumishi gani hajafuata maelekezo yake ??

Hakuna mtumishi wa umma anaeweza kukataa maelekezo yake akabaki.

Yeye mwenyewe ndio tatizo kubwa yaani ni zigo haswa.

Ameshaona hana jipya, anatafuta mtu wa kumwangushia jumba bovu Kwasababu anajua hawawezi kumjibu kwasasa.
Hapo unamuonea bure mzee wa watu.

Haiwezekani akawa anatoa maelekezo kwa watendaji wake on a daily basis.

Mambo mengine watendaji wanapaswa kutumia tu utashi wao kuyafanyia maamuzi, wala haihitaji maelekezo kila mara.

Sasa hao wanaokaa tu kusubiri kuambiwa cha kufanya ndio wanaozungumziwa hapa, wajiongeze.
 
Hiyo katiba na sheria tulimpa za nini? Mbona watendaji wanapopoleka hela kitovuni halalamiki?
 
Hapo unamuonea bure mzee wa watu...
Ni kwamba Magufuli anaweza akatoa maelekezo ukayafuata, akiona yameleta kelele nyingi na yeye anatafuta sifa Anakufukuza.

Kwani yule mama wa kikokotoo alifukuzwa kazi Kwasababu gani ??

Pili, unaweza ukasema ujiongeze mwenyewe, utakachofanya akachukia pia Akakufukuza na mipasho juu.

Ndio maana watendaji wake kila mtu anasubiria maagizo.
 
Ni kwamba Magufuli anaweza akatoa maelekezo ukayafuata, akiona yameleta kelele nyingi na yeye anatafuta sifa Anakufukuza...
Hizo ni mbinu tu za kujustify uzembe na kushindwa kutimiza wajibu kwa watendaji.

Swala hapa ni kuwa ukipewa kazi fanya yakihitajika maelezo toa, hizi kazi hakuna mtu kazaliwa nazo mkuu, wala si za milele kwamba ukiwa na nafasi flani basi ndio mpaka kiama, watu wafahamu kuwa wamebeba dhamana za kuwatumikia watanzania, ukifutwa kwa kufanya maamuzi ni bora zaidi kuliko kufutwa Bila ya kufanya maamuzi yeyote.
 
Back
Top Bottom