Rais Magufuli: Watendaji wangu wananichelewesha. Naomba chama changu CCM kinisaidie kuwasukuma, tumechelewa!

Kama nchi haikuendelea wakati kipo chama kimoja(one nation one political party) anadhani kuirudisha kulekule ndio kuleta maendeleo eeh?

Nyerere hakuwa mjinga kuachia madaraka, Nyerere hakuwa mpumbavu kufosi kuanzishwa mfumo wa vyama vingi(mind you majority waliukaa mfumo wa vyama vingi).

Sasa mzee baba washauri wake wamkalishe chini kisha wampige pindi la tulipotoka mpaka tulipo ndipo atajua namna ya kuhandle haya mambo.
 
Kama nchi haikuendelea wakati kipo chama kimoja(one nation one political party) anadhani kuirudisha kulekule ndio kuleta maendeleo eeh?

Nyerere hakuwa mjinga kuachia madaraka, pia Nyerere hakuwa mpumbavu kufosi kuanzishwa mfumo wa vyama vingi(mind you majority waliukaa mfumo wa vyama vingi lakini mzee akafosi sababu alishaona mbali).

Sasa mzee baba washauri wake wamkalishe chini kisha wampige pindi la tulipotoka mpaka tulipo ndipo atajua namna ya kuhandle haya mambo.
 
Mwenyekiti wa CCM wilaya ni F4 level, atamfukuza kazi mkurugenzi wa manispaa au Halmashauri? Tatizo lililipo CCM ni kile kipengele cha kuweza kusoma na kuandika unakula kiongozi, Kipengele hiki kitamtesa sana Rais.
 
Si mlisema wapinzani wamewachelewesha sana?? Nn kimez...
Makatibu wa CCM wilaya na mikoa ndio waliopewa magari ya kufuatilia utendaji wa serikali. Magari hayo ukiyatafuta kila siku,iwe mchana au usiku utakuta limepakiwa either hotelini au bar. Sasa ninajiuliza ofisi za chama zinakuaga karibu na maeneo hayo au maeneo hayo ndiko ziliko ofisi za chama.
 
Mwenyekiti wa CCM wilaya ni F4 level, atamfukuza kazi mkurugenzi wa manispaa au Halmashauri? Tatizo lililipo CCM ni kile kipengele cha kuweza kusoma na kuandika unakula kiongozi, Kipengele hiki kitamtesa sana Rais.
Hawa wenyeviti wa ccm wanaotembelea vieitee, unaijua vieite wewe??
 
Rais asipowatumbua viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na mikoa, hatakaa afanikiwe. Viongozi wa serikali wanachokifanya ni kula kwa Karibu na viongozi wa CCM ,ili wapate abc za ndani za chama maisha yaende na aweze kukwepa kutumbuliwa.
Hawa wenyeviti wa ccm wanaotembelea vieitee, unaijua vieite wewe
 
I would appreciate kama ataanza kujifukuza yeye mwenyewe kwanza.
Anapotaka kuteuwa watendakazi si huwa anafanya vetting?
Ukifanya makosa kwenye kuteuwa usitegemee output yeyote yenye tija.
 
Walifanya vizuri kutumia polisi na mjinga Mahera, kupora kura zote za wapinzani. Sasa wanahangaika wa kumsingizia hawampati. Inawalazimu kuanza kusingiziana wenyewe kwa wenyewe.

Unaweza kumsingizia paka kila uchafu uliopo ndani ya nyumba yako. Ukimwua ndiyo utajua ni namna gani alikuwa anazuia uharibifu wa panya.

Rais Magufuli atastaafu bila kuwa na amani wala furaha moyoni mwake maana 70% ya mambo aliyoyanzisha hayatakuwa yamekamilika. Mbaya zaidi atauacha uchumi ukiwa umeparalyse completely. Waliokuwa wakimsifu, taratibu wataanza kujitenga naye.

Asilimia kubwa ya wateule wa Magufuli ni watu wenye upeo mdogo, wanachojua ni kila siku kumsifia Magufuli badala ya kuwa na mipango madhubuti ya kubadilidha maisha watu. Wenye akili wanachojua ni kutimiza wajibu, siyo kushinda unamsifia Rais.

Kwa vile Rais anapenda sana kusifiwa, basi lazima anabakia na hao wenye akili ndogo na wanafiki.
 
Rais katoa mwelekeo wake kwa kipindi hiki cha miaka mitano ni jukumu la watendaji kufuata maelekezo.

Tanzania ya viwanda inawezekana,

Maendeleo hayana vyama.
Ni mtumishi gani hajafuata maelekezo yake ??

Hakuna mtumishi wa umma anaeweza kukataa maelekezo yake akabaki.

Yeye mwenyewe ndio tatizo kubwa yaani ni zigo haswa.

Ameshaona hana jipya, anatafuta mtu wa kumwangushia jumba bovu Kwasababu anajua hawawezi kumjibu kwasasa.
 
Rais asipowatumbua viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na mikoa, hatakaa afanikiwe. Viongozi wa serikali wanachokifanya ni kula kwa Karibu na viongozi wa CCM ,ili wapate abc za ndani za chama maisha yaende na aweze kukwepa kutumbuliwa.
Sidhani kama kuna haja ya kuhangaika na hao watu wao, cha msingi ni kukitenganisha chama na serikali full stop.

Mifumo ya serikali ikiachwa huru inaweza kujicheck yenyewe kwa namna ilivyoundwa sio hii 'one man show', eti hadi choo cha soko kinasubiri rais aje ndio kero itatuliwe, huyu rais ana uwezo wa kufika maeneo mangapi kwa mwaka?

Huku tunapoelekea ndio watakuwa na massive failure, kama hadi ajira wanatoa kwa kuangalia kadi za chama.
 
Nchi hii ina watu 50+m kama mtu ana speed ya kobe weka pembeni weka mwingine
 
Back
Top Bottom