Rais Magufuli: Watendaji wangu wananichelewesha. Naomba chama changu CCM kinisaidie kuwasukuma, tumechelewa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,854
141,792
Rais Magufuli amesema kuwa Rais ni kazi ngumu sana kwa sababu wewe unaweza kupanga mipango hii kumbe wenzako nao wana mipango mingine.

Rais Magufuli amewataka viongozi wa CCM wamsaidie kufuatilia utendaji wa watendaji wake kwani wengine wanachelewesha maendeleo.
Rais Magufuli amesema yeye haogopi anaweza kufukuza kuanzia mkuu wa mkoa hadi mtendaji wa kijiji ikibainika watu hao ni wazembe na anateua wengine fasta.

Rais Magufuli ametoa onyo kwa watendaji wote wanaomchelewesha kwamba wasije kumlaumu atakapochukua hatua stahiki dhidi yao.

Rais Magufuli leo amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Morogoro.

Source ITV

Maendeleo hayana vyama!
 
Pale ambapo Upinzani utakapozimwa na kubaki chama kimoja basi hapo ndipo upinzani wa kweli utaibuka kutoka katika chama hiko hiko kimoja.

Pale ambapo kitabaki chama kimoja katika serikali basi ndipo raisi ataanza kuwagundua na kuwatenga wavivu halisi na watendaji wa hovyo hovyo katika uongozi wake.

Kipimo cha mtendaji bora sasa hivi sio kuwaponda tena na kuwajibu wapinzani laa bali kipimo halisi cha sasa ni utendaji bora,wapinzani wa kuwajibu tena hawapo kabisa.

Pigeni kazi huko.
 
Rais katoa mwelekeo wake kwa kipindi hiki cha miaka mitano ni jukumu la watendaji kufuata maelekezo.

Tanzania ya viwanda inawezekana,

Maendeleo hayana vyama.
 
Back
Top Bottom