Rais Magufuli: Watendaji wangu wananichelewesha. Naomba chama changu CCM kinisaidie kuwasukuma, tumechelewa!

Kutafuta visingizio kila kukicha! Kwanza alidai wapinzani wanamchelewesha sasa kahamisha goli! Kaniki ndiyo rangi yake usimlaumu dobi bure kubali tu that you have no ability to lead this country to the promise land.
 
Wengi ni wapinga maendeleo. Wanaharibu kwa jina la kutimiza uliyowatuma. Inasikitisha sana
 
Kama nchi haikuendelea wakati kipo chama kimoja(one nation one political party) anadhani kuirudisha kulekule ndio kuleta maendeleo eeh?..

Kimsingi hakustahili kuwa rais, urais ni zaidi ya kujenga reli. Ni sawa umchukue mtu kisa ni mshambuliaji mzuri, udhani siku akiwa kocha atakuwa kocha mzuri.
 
Anacheleweshwa na nani wakati anajifanya yeye ndo anajua kila kitu?

Mwenyekiti wa Mtaa yeye
Tarishi yeye
Polisi yeye
Hakimu yeye
Jaji yeye
Spika wa Bunge yeye

Anacheleweshwa na nani? Si akiri tu maarifa zero!
 
Mzee ulituambia kuwa mbowe na genge lake (wapinzani) ndio walikuwa wanakuchelewesha kutuletea maendeleo, ukatuambia tusikuchanganyie magunzi kwenye kurunzi. Sasa mbona tena tumeweka betri tupu lakini malalamiko yanaendelea?
Watawakumbuka wapinzani na baadaye wataomba poo.Sasa hivi bado kitambo kidogo tu wataanza kuraruana wao kwa wao.Tatizo ni mifumo yetu,mkiambiwa tubadili Katiba turekebishe mfumo wa utawala unaolimbikiza vitu vyote kwa Rais.

Vinginevyo Mzee avumilie maana kayataka mwenyewe.Alikuwa na nafasi October 2020 kujipumzisha kwa heshima aliposhindwa,kwa nini akatenda dhambi?
 
Pale ambapo upinzani utakapozimwa na kubaki chama kimoja basi hapo ndipo upinzani wa kweli utaibuka kutoka katika chama hiko hiko kimoja....
Haaaa!!! Mweeee!!!

Chirani vipi tena ... Mura!!! Mbona umebadiri channeri gafra!!! sio tena wapinzani wanaocherewesha maendereo ... Aaaaa Mura!!! Sasa mbona kama unatuchezeya akiri



Soon mtaanza kupotezana na kutekana haina muda mrefu wallah mwaka huu hauishi mtaanza kujiteka na kupotezana wenyewe kwa wenyewe

Alifkiri Urais ni kama kula chips kuku
 
Mzee ulituambia kuwa mbowe na genge lake (wapinzani) ndio walikuwa wanakuchelewesha kutuletea maendeleo, ukatuambia tusikuchanganyie magunzi kwenye kurunzi. Sasa mbona tena tumeweka betri tupu lakini malalamiko yanaendelea?
.... na mara nyingi kwenye hafla za kuwaapisha anawasifia wateule wake kuwa si vilaza wala wazembe. Leo analalamika kwamba wanamchelewesha.....!!
 
Makatibu wa CCM wilaya na mikoa ndio waliopewa magari ya kufuatilia utendaji wa serikali. Magari hayo ukiyatafuta kila siku,iwe mchana au usiku utakuta limepakiwa either hotelini au bar. Sasa ninajiuliza ofisi za chama zinakuaga karibu na maeneo hayo au maeneo hayo ndiko ziliko ofisi za chama.
Hahahaha ni sheeeeda
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom