Rais Magufuli: Watanzania mniombee ili nimalize vizuri kipindi changu cha uongozi kama ilivyo kwenye katiba baada ya hapo niwaachie wengine

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,875
Hizi ni kama salamu kwa Ndugai na wale wengine wenye nia ya kubadilisha Katiba ili kuongeza muda wa Rais kukaa madarakani.

Leo jijini Dodoma katika sherehe za uzinduzi wa wa barabara katika mji wa kiserikali yenye urefu wa kilomita 51.2, pamoja na uzinduzi wa Jengo la ofisi za TARURA mji wa Mtumba, Rais Magufuli amesema kuwa muda ukifika ataachia madaraka kama ambavyo Katiba inaelekeza.



Nami kama kiongozi muniombee, nisiwe na kiburi, nisiwe na jeuri. Nikawe mtumishi wa kweli kwa Watanzania wote bila kuwabagua kwa rangi zao, kwa dini zao, kwa makabila yao. Nikatimize wajibu wangu katika kipindi ambacho kimepangwa kwenye Katiba, ili kusudi baada ya hapo tuwaachie wengine watakaokuja watimize wajibu wao.

Nataka kuwahakikishia Watanzania ninawapenda lakini pia nataka niwahakikishie kazi hii ni ngumu sana. Ina mateso sana. Inahitaji sala, Inahitaji dua, Inahitaji nguvu za Mwenyezi Mungu. Kwenye hilo ndugu zangu, naomba muendelee kuniombea na mimi naendelea kuwaombea.


Pia soma > Ally Kessy: Katiba sio msahafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Maendeleo hayana vyama!
 
Hata kama yeye anataka. Mambo ya urais wa Tanzania yameshapangwa tangu ENZI za nyerere. Huo mpangilio hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote yule. Usidhani CCM wote wanataka magufuli aongeze MUDA WAKE. Wapo wengi wanaoutaka urais hapo. Hawawezi kumuachia.

HIZI KELELE ZISIKUPE TABU.
Geresha tu hiyo ili baadae ije kuonekana amelazimishwa na wananchi
 
Back
Top Bottom