Mwenyekiti wa CCM na Rais John Magufuli amekionya chama chake kisibweteke kwani upinzani wa sasa unatisha kutokana na mikakati yake
Akiwahitubia viongozi wa wilaya na mikoa kote nchini jijini DSM hapo jana Rais amesema wapinzani wa leo wamebadilika na wana mikakati ya hadharani na ya siri katika mapambano ya kutwaa madaraka
Ingawa Rais hakutaja chama chochote kwa jina lakini ni hivi karibuni chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kilifanya mkutano mkuu wake uliovunja rekodi kwa jinsi ulivyopangiliwa vyema na hatimaye ikagundulika kwamba kwa sasa chama hicho kina wanachama wenye kadi milioni 6 na nusu kutokana na operesheni yake ya Chadema ni Msingi iliyofanyika nchini kote kimyakimya kwa miaka miwili.