Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Nina uhakika wabunge wa CCM watarudi bungeni, lakini ambao hawatarejea tunashukuru kwa mchango wao

Sisi wana cdm tumemkubali
Watumie wananchi, wasifanye wenyewe. Ndio maana ya uongozi. Mbowe tena usiseme. Ndiye mwoga kuliko wote. Mimi nadhani kuwa Chadema ingeongozwa na Lissu, Heche ama Lema, kungekuwa na mabadiliko ya kweli. Mbowe amekubali kuwa kiongozi wa upinzani bungeni na anaona hiyo inamtosha.
 
Hiyo inaitwa jino kwa meno
Comment safi kabisa. Natamani mgombea urais awe Lissu na muongoza kampeni awe John Heche uwe mwendo wa nyundo tu. CCM Wakipiga nyundo inajibiwa haraka na kwa uhakika na team ya CHADEMA. Hakuna kuremba
 
Retired, don't retire on this! Mungu ana njia nyingi hata hiyo unayosema anaweza akaiamrisha yeye. Kumbuka kilichofanyika Zimbabwe. Smoothly. Au kwenye mkutano wake wa kwanza wa kampeni akakumbana na chango lililomwondoa Herode duniani. Nani alijua kuondoka kwa Nkurunziza kutakuwa kutokukabidhi ikulu kwa rais mteule. Mungu ni hatari. Hawahi wala hachelewi. Aishiye kwa upanga, hufa kwa huo. Every dog has its appointed day. Let's play cool. God is omniscient, omnipresent and omnipotent. Let everybody shout Ameeeen!
Ameeen!!
 
Mimi napendekeza kuwa uchaguzi wa mwaka huu ugeuzwe kuwa fursa ya mapinduzi ndani ya nchi yetu. Wapinzani wa kweli ongozeni umma kwenye mapinduzi. Kwa kauli ya Magufuli ni kuwa watafanya kila litakalowezekana pasiwe na upinzani wa kweli mara baada ya uchaguzi.

Kitendo chochote cha kukosa haki ni lazima kikabiliwe na upinzani imara hata kama hiyo itabidi kufanya vurugu. Itisheni civil disobedience. Zile kauli za woga kwamba 'hatutaki kuingia ikulu kwa damu za watu' ziachwe kabisa, kwani sasa ni dhahiri kuwa haki haiwezi kutolewa bali itadaiwa.

Tujitayarishe kwa mapambano, na kwangu sioni mgombea wa urais anayeweza kuliongoza hili isipokuwa Mh Tundu Lissu. Mbowe ni kiongozi mzuri lakini ni soft sana, na mwoga. Nyalandu ndiyo kabisa hili haliwezi. Tujiandae kwa mapambano, wananchi wataunga mkono wakiona mko makini.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
Kauli ya Magufuli ya leo ni ya kutisha sana na ishara kuwa wapinzani wataondolewa wote bungeni atabaki yesu na wafuasi wake.

Kama wapinzani wanataka kuiondoa ccm madarakani wasisumbuke kuwapigisha kampeni za kupiga kura wananchi badala yake watangaze civil disobedience tu.

Muda wa kuchukua fomu ukifika kuna wengine watatoka nyumba salama ila hawatarejea, Mungu atuepushe na hili.

cc.
Zitto

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Kauli ya Magufuli ya leo ni ya kutisha sana na ishara kuwa wapinzani wataondolewa wote bungeni atabaki yesu na wafuasi wake.

Kama wapinzani wanataka kuiondoa ccm madarakani wasisumbuke kuwapigisha kampeni za kupiga kura wananchi badala yake watangaze civil disobedience tu.

Muda wa kuchukua fomu ukifika kuna wengine watatoka nyumba salama ila hawatarejea, Mungu atuepushe na hili.

cc.
Zitto

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Sio kila siku ni jumapili,wanalijua Hilo washajipanga nalo
 
Wapinzani walikuwa na miaka 5 ya kutafuta katiba mpya yenye kuweka mazingira ya uchaguzi huru na wa haki. Tena hapo mwanzo 2016 walikuwa na Wabunge wengi sana na nguvu ya kutosha.

Lakini walitulia tuli baada ya kuambiwa kuwa hakuna mikutano na maandamano. Kwa sasa it's too little too late. Siyo siri tena - dikteta atawatoa wote Bungeni. Alikwishawatoa kwenye serikali za mitaa tayari.
Wangetakiwa kufanya nini sasa kupata Katiba na Tume Huru ya Uchaguzi?Marufuku ya siasa,mikutano na maandamano iliatolewa mapema sana 2016,na tumeshuhudia wapinzani walivyofanyiwa hata walipokuwa na mikutano yao ya ndani.
Walitwezwa na vyombo vya dola hadharani,2017 pia tulishuhudia maajabu ya awamu ya tano,ndani ya viunga vya Bunge,mchana kweupe watu wasiojulikana walipofanya assassination na bado hakuna aliyetiwa nguvuni,wahusika wanadai wahanga ndiyo mashahidi,lakini Watanzania wapi kimya maana hayupo aliye salama hats sasa.
Tusiwalaumu wapinzani kwa hapa nchi hii ilikofikia,ni suala letu sote.Tuseme inatosha na tufanye maamuzi magumu na kuwakataa wakoloni weusi.Nafasi hiyo tunayo October 2020,tusikubali kuburuzwa.Nchi hii ni yetu sote.
Kipindi cha kwanza cha awamu ya tano kilivyokuwa kigumu,fikiria wanahitaji kurudi uongozini lakini hawatubembelezi ili tuwachague tena,tujiulize itakuwaje kipindi cha pili ambacho hawatakuwa na cha kupoteza?Watatukomesha,tutalimia meno had I tuwe vibogoyo.Ni hatari tupu.
 
Kutegemea external kutahalalisha hoja ya ccm kuwa vyama vya upinzani vinatumika na mabeberu.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app

Kwa hapa tulipofikia hakuna jinsi, isitoshe hoja za ccm sio kipimo cha ukweli ndani ya nchi hii. Wananchi wote wanaojitambua wanajua kinachofanyika. Hizo propaganda za ccm zisikutishe boss. Mbona sisi tunasema wao wanatumia vyombo vya dola, lakini hawaogopi bali wanatumia vyombo vya dola kiwaziwazi?
 
Vyama vya upinzani mmeona hicho kigongo kutoka kwa mshika dola?

Maneno haya aliyoyasema Rais yalipaswa yatolewe kwenye CCM campaign rally na siyo ndani ya chombo huru (at least kikatiba) kama bunge. Ana audacity ya kuonyesha upendeleo wa wazi kwa chama chake mahali ambapo si pake (bungeni) na yeye ni rais anayetakiwa kuwaunganisha watu wote hususani tunapoelekea kwenye uchaguzi.

Tukiingia kwenye uchaguzi bila ya kutengeneza mazingira ya uchaguzi huru na wa haki (hususani bila tume huru), si rahisi kwa wapiga kura wanaotaka upinzani ushike dola kushiriki kwenye uchaguzi ambao rais tayari keshatoa amri kwa vyombo vyenye wajibu wa kusimamia uchaguzi kuwa ni wabunge wa CCM pekee ndiyo watakaorejea bungeni.

Zitto Kabwe, John Mnyika na wengineo - you have the whole monster ahead of you to fry.

hata wa CCM wapo ambao hawatarudi. usimwelewe Rais in negativity tu big
 
Back
Top Bottom