Kwanini Rais Samia katumia strategies hizi? Kuna Nini kimejificha?

econonist

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,804
21,777
Tunapoelekea kwenye uchaguzi wa 2024 na 2025, inaonekana Kuna mbinu ambazo Samia amezitumia ili kushinda huo uchaguzi.

1. Strategy ya kisheria, Muswada wa Tume Huru ya Uchaguzi feki:

Ili kupata uhalali wa upinzani kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa wa 2024 na uchaguzi mkuu wa 2025, Samia aliamua kupitia serikali yake, kupeleka miswada ya uchaguzi, ikiwemo ya kuanzisha Tume Huru ya Uchaguzi.

Tume Huru ya uchaguzi inayotaka kuanzisha ni feki maana bado inasimamiwa na Rais na hata upatikanaji wa wajumbe umeegemea upande wa Rais.

Hivyo Samia Katumia hii strategy Kama chambo, ili kuvigawa vyama vya upinzani vitakavyoshiriki uchaguzi wa 2024 na 2025. Hata Kama CHADEMA haitashiriki, vyama vingine vya upinzani vikishiriki vinampa uhalali Samia kushinda uchaguzi mkuu.

Pia, Ili hii strategy ya uongo ipate nafasi, wakafanya maiigizo ya kupokea maoni ya makundi mbali mbali, ili kesho apate uhalali wa kusema tuliunda Tume Huru ya Uchaguzi kwa kupokea maoni ya watu wote. So hata uchaguzi Mkuu uende vibaya hakuna wa kulalamika maana kila mmoja alitoa maoni na yakawekwa kwenye miswada.

Swali la kujiuliza kwanini Samia Katumia njia ndefu hivi ingali lengo lake ni kuwa na Tume Huru Feki? Anaogopa Nini?

2. Strategy ya kijeshi. Kuliingiza jeshi la JWTZ kwenye siasa za uchaguzi mkuu wa 2025.

Kwenye mkutano wa CDF, Samia alidai Kuna vyama vya upinzani vinalenga kuleta vita au fujo baada ya uchaguzi mkuu wa 2025. Kwa hivyo, akaliamuru jeshi la JWTZ liwe tayari kwa lolote. Hii kauli ya Samia inalenga kuwaogofya wapinzani kwenye harakati za uchaguzi mkuu wa 2025 kwa kuogopa kufuatiliwa na wapelelezi wa JWTZ.

Kauli ya Samia, pia inalenga kuwafunga break wapinzani. Kuna kauli wapinzani wakiongea jeshi litaingilia kati na kuwatishia. Hivyo wapinzani wataanza kuwa answerable kwa Jeshi na kuacha kufanya siasa na kuwapa uwanja CCM wafanye siasa kwa uhuru.

Kwa mfano upinzani wakidai hawatakubali matokeo ya uchaguzi au wakidai hawatashiriki uchaguzi mkuu wa 2025, je JWTZ kwa Amri waliyopewa na Samia hawatachukua Kama kiashiria Cha fujo?.

Na je Samia akiiba uchaguzi mkuu wa 2025 Kama ilivyokuwa 2020, upinzani watalalamikia wapi?. Maana JWTZ itatumika Kama Kinga ya kuwashughulikia walalamikaji. Hivyo hata Samia akiiba kura, JWTZ wataingilia kati na kuwatishia walalamikaji kuwa wanahatarisha amani.

Swali la kujiuliza kwanini Samia kawatumia JWTZ Kama Kinga ya kuiba uchaguzi mkuu wa 2025? Anaogopa Nini?

3. Strategy ya Kisiasa. Kuanza kampeni mapema.

Samiah kaanza kampeni mapema Sana. Mtu anaweza kudhania tupo kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa 2025. Wabunge wakiwa bungeni wanampigia kampeni, mawaziri kwenye ziara zao wanampigia kampeni, wakuu wa mikoa wanampigia kampeni, wakuu wa wilaya wanampigia kampeni, wasanii wanampigia kampeni , machawa wanampigia kampeni na Makonda kwenye ziara zake anampigia kampeni. Ni kwanini ameanza kampeni mapema, kila kitu kipo kwenye viganja vyake. Kwanini uharaka huo?.

Lazima tujue kwamba Samia ana Bunge, ana Halmashauri na manispaa zote, ana wenyeviti wa Vijiji na Mitaa. Anaogopa Nini mpaka aanze kampeni mapema?. Kuna nguvu gani imejificha hatuioni yeye anaiona?. Yani unamiliki serikali yote na chama tawala ila bado unahangaika kupiga kampeni kabla ya muda wa uchaguzi mkuu, Tena mwaka mmoja na miezi kadhaa?

Swali la kujiuliza, Kwanini Samia aanze kampeni mapema wakati muda bado wa uchaguzi mkuu? Anaogopa Nini?
 
Pia, Ili hii strategy ya uongo ipate nafasi, wakafanya maiigizo ya kupokea maoni ya makundi mbali mbali, ili kesho apate uhalali wa kusema tuliunda Tume Huru ya Uchaguzi kwa kupokea maoni ya watu wote. So hata uchaguzi Mkuu uende vibaya hakuna wa kulalamika maana kila mmoja alitoa maoni na yakawekwa kwenye miswada.
Maoni yamekuwa incorporated in the sheria? NO, A BIG NO! kwa hiyo hana excuse yoyote ni ushenzi tu. Mbadala ni W A tu!
 
Samia ni Mwamba sana wa Siasa, baada ya JKs anafuata Samia katika ma Rais wote waliowahi kutawala nchini.

anajua sana Siasa za kulainisha udongo kwa kuumwagia maji badala ya kuupiga nyundo

Watu walipiga sana kelele za ruhusa ya mikutano ya hadhara wamepewa na sasa hawafanyi Mikutano

wamepewa Ruhusa ya maandamano na sasa yamedorora

kuna wahuni wamejaribu kum frustrate ili asaini mikataba mipya ya kuzalisha Umeme kabla ya kuzinduliwa kwa Mradi wa Stiglers gauge wamechemka na sasa mradi unazinduliwa awamu ya kwanza hivi karibuni

kama kuna kitu kikubwa sana ambacho Samia anacho kwny utawala wake ni kutokukurupuka kwmy Maamuzi
 
Kwani kutaka kutawala au kutaka uongozi ni Nia ovu? Mbona kila mtu anataka uongozi au ni Nia ovu pia
.
JamiiForums-565905357.jpg
 
uhakika wa kutoboa hana kwa haki ama isiyo haki, wananchi wengi huku chani hawamuelewi kabisa, hata huko juu natumaini haeleweki , anaeleweka kwa wachache sana wasio na uwezo wowote haswa wanaoitwa chawa.
 
Napenda kukupinga. Sis tuliandamana majuz juz je haikua kampen? Kutwa MMm mitandaon anapiga kampeni za chama chetu , nadhan tujikite kueneze falsafa zetu hawa jamaa wa ccm wana mbinu kali na wana umoja ambao sisi bawaacha hatuna
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwani kutaka kutawala au kutaka uongozi ni Nia ovu? Mbona kila mtu anataka uongozi au ni Nia ovu pia
Hapana,tunataka Mtu yeyote anaetaka kutuongoza afanye hivyo kwa RIDHAA zetu 👈sio kwa HILA na WIZI na KUTANGAZWA na WAKURUGENZI wa HALMASHAURI ambao wenyewe ni MAKADA wa CCM.

Anaetaka kutuongoza awe CCM au CHADEMA apate kwanza RIDHAA ZETU WANANCHI.
 
Tunapoelekea kwenye uchaguzi wa 2024 na 2025, inaonekana Kuna mbinu ambazo Samiah amezitumia ili kushinda huo uchaguzi.

1. Strategy ya kisheria, Muswada wa Tume Huru ya Uchaguzi feki:

Ili kupata uhalali wa upinzani kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa wa 2024 na uchaguzi mkuu wa 2025, Samiah aliamua kupitia serikali yake, kupeleka miswada ya uchaguzi, ikiwemo ya kuanzisha Tume Huru ya Uchaguzi.

Tume Huru ya uchaguzi inayotaka kuanzisha ni feki maana bado inasimamiwa na Rais na hata upatikanaji wa wajumbe umeegemea upande wa Rais.

Hivyo Samia Katumia hii strategy Kama chambo, ili kuvigawa vyama vya upinzani vitakavyoshiriki uchaguzi wa 2024 na 2025. Hata Kama CHADEMA haitashiriki, vyama vingine vya upinzani vikishiriki vinampa uhalali Samiah kushinda uchaguzi mkuu.

Pia, Ili hii strategy ya uongo ipate nafasi, wakafanya maiigizo ya kupokea maoni ya makundi mbali mbali, ili kesho apate uhalali wa kusema tuliunda Tume Huru ya Uchaguzi kwa kupokea maoni ya watu wote. So hata uchaguzi Mkuu uende vibaya hakuna wa kulalamika maana kila mmoja alitoa maoni na yakawekwa kwenye miswada.

Swali la kujiuliza kwanini Samiah Katumia njia ndefu hivi ingali lengo lake ni kuwa na Tume Huru Feki? Anaogopa Nini?

2. Strategy ya kijeshi. Kuliingiza jeshi la JWTZ kwenye siasa za uchaguzi mkuu wa 2025.

Kwenye mkutano wa CDF , Samiah alidai Kuna vyama vya upinzani vinalenga kuleta vita au fujo baada ya uchaguzi mkuu wa 2025. Kwa hivyo, akaliamuru jeshi la JWTZ liwe tayari kwa lolote. Hii kauli ya Samiah inalenga kuwaogofya wapinzani kwenye harakati za uchaguzi mkuu wa 2025 kwa kuogopa kufuatiliwa na wapelelezi wa JWTZ.

Kauli ya Samiah, pia inalenga kuwafunga break wapinzani. Kuna kauli wapinzani wakiongea jeshi litaingilia kati na kuwatishia. Hivyo wapinzani wataanza kuwa answerable kwa Jeshi na kuacha kufanya siasa na kuwapa uwanja CCM wafanye siasa kwa uhuru.

Kwa mfano upinzani wakidai hawatakubali matokeo ya uchaguzi au wakidai hawatashiriki uchaguzi mkuu wa 2025, je JWTZ kwa Amri waliyopewa na Samiah hawatachukua Kama kiashiria Cha fujo?.

Na je Samiah akiiba uchaguzi mkuu wa 2025 Kama ilivyokuwa 2020, upinzani watalalamikia wapi?. Maana JWTZ itatumika Kama Kinga ya kuwashughulikia walalamikaji. Hivyo hata Samiah akiiba kura, JWTZ wataingilia kati na kuwatishia walalamikaji kuwa wanahatarisha amani.

Swali la kujiuliza kwanini Samia kawatumia JWTZ Kama Kinga ya kuiba uchaguzi mkuu wa 2025? Anaogopa Nini?

3. Strategy ya Kisiasa. Kuanza kampeni mapema.

Samiah kaanza kampeni mapema Sana. Mtu anaweza kudhania tupo kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa 2025. Wabunge wakiwa bungeni wanampigia kampeni, mawaziri kwenye ziara zao wanampigia kampeni, wakuu wa mikoa wanampigia kampeni, wakuu wa wilaya wanampigia kampeni, wasanii wanampigia kampeni , machawa wanampigia kampeni na makonda kwenye ziara zake anampigia kampeni. Ni kwanini ameanza kampeni mapema, kila kitu kipo kwenye viganja vyake. Kwanini uharaka huo?.

Lazima tujue kwamba Samiah ana Bunge, ana Halmashauri na manispaa zote, ana wenyeviti wa Vijiji na Mitaa. Anaogopa Nini mpaka aanze kampeni mapema?. Kuna nguvu gani imejificha hatuioni yeye anaiona?. Yani unamiliki serikali yote na chama tawala ila bado unahangaika kupiga kampeni kabla ya muda wa uchaguzi mkuu, Tena mwaka mmoja na miezi kadhaa?

Swali la kujiuliza, Kwanini Samiah aanze kampeni mapema wakati muda bado wa uchaguzi mkuu? Anaogopa Nini?
Anajua hawezi kupata ushindi ukifanyika uchaguzi huru na wa haki,banajijua kubwa amepwaya sana kwenye urais, hivyo ameamua kutumia kadi za wananchi kujipigia debe. Tangu aingie madarakani alianza kampeni mara moja kwa kutumia chawa wake waliosambaza picha na matangazo yake nchi nzima
 
Back
Top Bottom