Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,059
Tanzania haiendelei na haiwezi kuendelea kwa sababu waovu waliostahili adhabu, ndiyo viongozi wa kuwasimamia watu wema na kuwaonesha njia kuhusiana na maisha yao ya kila siki. Ukimpa nafasi mtu mwovu akuongoze, unatarajia atakuongoza kupeleka wapi?
Hivi karibuni, viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali wamekuwa wakikiri kuwa wao na wabunge ni zao la uovu.
Ni watu ambao hawakuchaguliwa na umma kwa sababu uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 haukuwa uchaguzi huru wala wa haki. Lakini pia mahakama kuu ilitoa hukumu inayosema kuwa wabunge wote waliotangazwa kuwa walipita bila kupingwa, akiwemo na Waziri Mkuu Majaliwa, ni wabunge batili. Cha ajabu, bila aibu watu hawa bado wameng'ang'ania madaraka.
Ukweli ni kwamba, kila mmoja anajua kuwa uchaguzi wa 2020 ulizidi katika kiwango cha uovu. Lakini tunajua kuwa hata kabla ya 2020, Tanzania haijawahi kuwa na uchaguzi huru na wa haki chini ya CCM.
Wote waliopo bungeni kuanzia PM, mawaziri mpaka wabunge ni mazao ya uovu. Rais yupo kwenye nafasi hiyo siyo kwa kuchaguliwa bali kwa mujibu wa katiba iliyokanyagwa kwa kiwango cha ajabu mwaka 2020.
Tena kwa kauli yake mpaka alifikia kutoa kauli ya kuwabeza wapiga kura pale aliposema kuwa hata kama wananchi wakiwapigia kura vyama vingine, zitahesabika kwa CCM.
Kwa kuwa wote, wakiwemo viongozi wa CCM, Serikali, vyama vya upinzani na wananchi mmoja mmoja, tunakiri kuwa Waziri Mkuu, mawaziri, wabunge na madiwani, ni mazao na ni washirika wa uovu, kwa nini tusingekubaliana kuwa kwa sababu watu hawa ni zao la uovu na ni washiriki wa uovu, basi nao wanastahili kuadhibiwa, ili kujenga mfumo wa kuwawajibisha watu wanaodharau na kupora mamlaka ya umma katika kuwachagua watu wanaotaka wawaongoze.
PENDEKEZO:
Waziri Mkuu, Mawaziri, Wabunge, Madiwani, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na vijiji aa sasa, kwa kushiriki uovu na kuwa zao la uovu mwaka 2020, wasiruhusiwe kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya miaka 10 kuanzia 2025.