Rais Magufuli na 'mgonjwa aliyerogwa'

Rais Magufuli na 'mgonjwa aliyerogwa'

Wahenga walinena ya kwamba "Mficha maradhi mauti humuumbua"
 
Sasa si 'mgonjwa atakufa'?
Mgonjwa hatokufa atazimia tu na akipata fahamu tena ataisoma namba tu.

Unajua MKULU wetu anajaribu Model mpya ambayo ameibuni mwenyewe kule maabara alipokuwa anachanganya yale makemikali ya maganda ya korosho. Model yake ya kuufanya uchumi wa Tanzania kuwa uchumi wa kati.

Model yake inataka kwanza ni lazima uchumi uote kutu, hatua ya kwanza (kusanya fedha zote kutoka kwa wafanyabiashara na walalahoi, hapa unawalamba kodi za kukaza mkanda).
Hatua ya pili weka bei elekezi ambazo zitaongeza bei za bidhaa zilipangiwa bei elekezi.

Hatua ya tatu, kopa fedha nyingi kutoka nje ili kujenga reli na kuanzisha michakato ya kujenga viwanda.
Hatua ya nne, kutoa marufuku kwa wanaopendekeza mawazo mbadala ili mawazo yako yawe ndio pekee na yazoeleke. Hatua ya nne inaendana pia na kutishia kutoa noti mpya. Hatua ya tano ni kuwafurahisha watani kwa kuwaambia wafyatue watoto ili awasomeshee bure lakini hatatoa chakula cha msaada watakapopatwa na njaa au uhaba wa chakula.

Hatua itakayofuata ndio itaingiza uchumi katika uchumi wa kati. Hatua hii bado ni siri aliyoikumbatia Mkulu ataandika kwenye kimemo tena kwa mkono ili kudhibiti usiri wake na ataitangaza hatua hii siku uchumi utakapofikia hatua kuwa umeota kutu kweli, kweli kabisa. Hapo tena atamwagia ile coating ya kuyeyusha kutu, coating ya mafuta ya maganda ya korosho na uchumi utaanza mchakato wa kuingia uchumi wa kati. Magu hafanyi vitu kwa kubahatisha, anafanya mambo ya kimaabara.

Alishawaambia atawatumbua kama mliodhani anawatania, yametimia sasa.

Mpeni muda mganga amshughulikie mgonjwa wake, kwa ramli, kwa kikombe cha babu au kwa madawa kemikali. Mkimpigia kelele sana mganga anaweza kumu-overdose mgonjwa. Semeni polepole na kwa sauti laini, sauti kama mrenda(bamia).

Link Hivi ni kweli TRA wanakusanya zaidi ya trilion 1 kwa mwezi? nina wasiwasi
 
Kama ni kuambiwa anaambiwa sana tuu! ,tatizo ni kuamini analoambiwa! .

Ukishajenga pre conceived negativity kuwa watu ni wezi!, then hata ukiambiwa hakuna any economical activities za kusisimua uchumi, utaamini watu wanaiba hizo activities!.

Pasco
Hivi mnatakaje kwani?
Pasco waambie watu wafanye kazi waache kulalama
Halafu maisha sio lazima uajiriwe serikalini,mbona wewe uliacha kazi na upo juu tu kuliko uliwaacha huko
Fanyeni kazi kwa bidii
 
Humu kuna dalili za UCHOCHEZI, nasubiri TAMKO
 
Kuna vitu ukiviamini kwa asilimia 100 basi ni ngumu sana mtu mwingine kuja kukuambia vinginevyo.Ni sawa na mtu ambae anaumwa halafu anaamini 'kalogwa'

Mtu huyu hata umpeleke hospitali atakua tu bado anaamini 'kuna mkono wa mtu.

Ikitokea hospitali wamesema 'hana malaria' ndo kabisaa atazidi kuamini ni 'mkono wa mtu'.

Hadi itokee mtu mwingine ambae anaweza kumsikiliza ashauri 'hebu pima na typhoid' au 'pima UTI..' na akutwe na magonjwa apewe dawa apone ndo unaweza kidoogo kumfanya akusikilize vinginevyo watu dizaini hii wanaweza kufa au kusababisha kifo cha mtoto au ndugu anaeumwa.

Sasa hoteli zinafungwa na zingine zinauzwa, biashara zinakufa kwa wingi
pesa imepotea lakini Rais anaamini kuna 'hujuma' na dawa ni kuanza msako wa 'walioficha hela majumbani' au kuchapisha noti au kubadili noti.

Cha ajabu 'madaktari ' wetu nao wa kumwambia 'ukweli' kuhusu 'ugonjwa'
wako kiimya kabisa tunapiga ramli wakati magonjwa haya yana vipimo vyake
na dawa zake zinajulikana.

Hadi 'mgonjwa' afe ndo waje kusema ilikuwa 'typhoid'?
Watasema alikuwa na 'typoid' kwa kuwa wataona aibu kutamka hadharani kwamba alirogwa...
 
Kama ni kuambiwa anaambiwa sana tuu! ,tatizo ni kuamini analoambiwa! .

Ukishajenga pre conceived negativity kuwa watu ni wezi!, then hata ukiambiwa hakuna any economical activities za kusisimua uchumi, utaamini watu wanaiba hizo activities!.

Pasco
1. Mnakumbuka alikuwa waziri wa uchkuzi, alipokuwa anaongelea yale magari yaliyokuwa yanasafirisha mizigo zaidi alisema anatamani watozwe faini hadi wafilisike;

2. Alipoambiwa, huko sinza mahoteli yameenza kugeuzwa hosteli alisema acha wazigeuze maana zilikuwa zinatumiwa na wafanyakazi wa serikali sasa hawawezi kwa maana amewazuia;

3. Alipoambiwa badalini mizigo haipo ya kutosha alisema , mbona mapato yameongezeka, na kama hawalipi ushuru afadhali wasije

4. Alisema athakikisha waliokuwa wanaishi kama malaika wanaishi kama masheteni

5. Alisema vile vile acha watalii wasije kwa kuwa hawataki kulipa VAT

6. Ameshangaa Dr. kusaini malipo ya kumtibia Seif Sharifu Hamadi kwa kuwa alikataa kusalimiana naye

Inaonyesha hayo ndiyo maisha aliyoyazoea. Tuna bahati mbaya kama taifa, ila ni kweli yeye ni bora kulipko Lowasa kwa baadhi ya mambo.
 
Kuna vitu ukiviamini kwa asilimia 100 basi ni ngumu sana mtu mwingine kuja kukuambia vinginevyo.Ni sawa na mtu ambae anaumwa halafu anaamini 'kalogwa'

Mtu huyu hata umpeleke hospitali atakua tu bado anaamini 'kuna mkono wa mtu.

Ikitokea hospitali wamesema 'hana malaria' ndo kabisaa atazidi kuamini ni 'mkono wa mtu'.

Hadi itokee mtu mwingine ambae anaweza kumsikiliza ashauri 'hebu pima na typhoid' au 'pima UTI..' na akutwe na magonjwa apewe dawa apone ndo unaweza kidoogo kumfanya akusikilize vinginevyo watu dizaini hii wanaweza kufa au kusababisha kifo cha mtoto au ndugu anaeumwa.

Sasa hoteli zinafungwa na zingine zinauzwa, biashara zinakufa kwa wingi
pesa imepotea lakini Rais anaamini kuna 'hujuma' na dawa ni kuanza msako wa 'walioficha hela majumbani' au kuchapisha noti au kubadili noti.

Cha ajabu 'madaktari ' wetu nao wa kumwambia 'ukweli' kuhusu 'ugonjwa'
wako kiimya kabisa tunapiga ramli wakati magonjwa haya yana vipimo vyake
na dawa zake zinajulikana.

Hadi 'mgonjwa' afe ndo waje kusema ilikuwa 'typhoid'?
Duuuuh
 
Kwa hiyo suala ni kupandishwa kwa kodi? Mimi nimesema kuwa kulikuwa na masuala ya deal kati ya wenye hotel na wenye maamuzi serikalini. Hakika nakuambia hata kama kodi ingepanda kiasi gani lakini serikali ikaendelea na mtindo wake ambapo Ofisi zilikuwa zinahamia mahotelini, hizo hotel wala zisingetikisika hata chembe.
Hilo ni moja ya matatizo. Wewe unafikiri kuna tatizo moja?
Kupandishwa kodi ni tatizo ndio.

Nchi za wanaopenda mambo ya uchumi,sio mambo kuombewa kwa Mungu. Walipoingia katika hali ngumu ya uchumi walipunguza interest rate, benki kuu za zili-slash interest rate kwenda near kamanda 0. mabenki mengine ya nchi,mabenki ya biashara, (mabenki ya wakulima, ushirika na ushirikina) nayo yalipunguza riba za mikopo kwa wateja. Hatua hii ililenga kuwahamasisha watumiaji,walaji na wajasirimali kuufanya mzunguko wa fedha uendelee. Je Serikali ya Magu wanafanya nini?
Huoni lipo tatizo,matatizo hapo?

Wanaibuka wanasema, wafanyabiasha wameficha sukari, wafanyabiasha wamehodhi fedha.
Matatizo ni mengi.

Mkulu aitishe au aunde jopo la washauri wa uchumi, awaeleze nini anakusudia kufanya kwa uchumi na apate mawazo kutoka kwa wataalamu hao, wataalamu hao wawe wa nyanja tofauti za uchumi, tena asichague wale tu watakaoimba zidumu fikra za mwenyekiti. Agonganishe mawazo yao. Vyenginevyo atatupeleka kuzimu au atatupa matumaini hewa kama kile kikombe cha babu.

Kuongoza nchi sio kupiga push up kweye jukwaa la kuombea "kula".

Tuendelee kumwombea Mkulu ili anapoutumbua uchumi autumbue in slow motion.
 
Mkuu toa basi na suluhisho la kutibu ugonjwa.

Mimi naamini tulipokuwa tumefikia inabidi tuvurugane kwanza kisha mambo yakae vizuri. Sijaona Serena ikifungwa, sinaona Hyatt Regency ikifungwa. Zinazofungwa ni zile za deal, zile zilizokuwa zinategemea deal toka serikalini. Zile zilizokuwa zinategemea mikutano ya serikali kwa gharama kubwa ambazo zilihusisha cha juu!! Unakuta Ofisi nzima anahamia hotelini ili kufanyia kazi huko kwa wiki nne; wanalala, wanakunywa na kucheza muziki bili ikija ni mamilioni na waliohusika kuandaa wanachekelea njia nzima kwenda kujinyakulia cha juu.
Umenena mkuu ila sasa serikalini wamegeukia fedha za miradi kutoka kwa wafadhili wa nje kufanya hotelini mikutano na warsha.
 
Acheni mawazo yakijinga....!!
Kaka kuna watu wana mawazo mpaka unawaonea huruma. Maana unajiuliza kwa mawazo hayo kweli wataweza kuipeleka nchi katika huo uchumi wa kati? Hizi akili nyingi za watanzania zinatosha kuifanya nchi iwe na uchumi wa mwisho.
 
Kuna vitu ukiviamini kwa asilimia 100 basi ni ngumu sana mtu mwingine kuja kukuambia vinginevyo.Ni sawa na mtu ambae anaumwa halafu anaamini 'kalogwa'

Mtu huyu hata umpeleke hospitali atakua tu bado anaamini 'kuna mkono wa mtu.

Ikitokea hospitali wamesema 'hana malaria' ndo kabisaa atazidi kuamini ni 'mkono wa mtu'.

Hadi itokee mtu mwingine ambae anaweza kumsikiliza ashauri 'hebu pima na typhoid' au 'pima UTI..' na akutwe na magonjwa apewe dawa apone ndo unaweza kidoogo kumfanya akusikilize vinginevyo watu dizaini hii wanaweza kufa au kusababisha kifo cha mtoto au ndugu anaeumwa.

Sasa hoteli zinafungwa na zingine zinauzwa, biashara zinakufa kwa wingi
pesa imepotea lakini Rais anaamini kuna 'hujuma' na dawa ni kuanza msako wa 'walioficha hela majumbani' au kuchapisha noti au kubadili noti.

Cha ajabu 'madaktari ' wetu nao wa kumwambia 'ukweli' kuhusu 'ugonjwa'
wako kiimya kabisa tunapiga ramli wakati magonjwa haya yana vipimo vyake
na dawa zake zinajulikana.

Hadi 'mgonjwa' afe ndo waje kusema ilikuwa 'typhoid'?

Hao wanaouza na au kufunga hizo hotels "kwa wingi" wamekwambia sababu za kufanya hivyo? Na pili je unajua kuna biashara ngapi zinafunguliwa kila siku?
 
Kufungwa kwa hotel ni mojawapo tu matokeo ya biashara kupotea jumla na mara nyingi huwa ni hatua ya mwisho. Serena na Kilimanjaro Hotel hazijafungwa ndiyo lakini sijui kama unafahamu bei za baadhi ya huduma kubwa pale zilivyolazimika kushushwa kutokana na kukosekana kwa uteja.
Kukodi hema kubwa (marquee) ilikuwa mpaka $3,000 lakini sasa hivi hata kwa $1,000 unaweza kukodi. Kutumia bustani ya Serena kwa ajili ya cocktail ilikuwa around $1,000 lakini sasa hivi ni dollar mia kadhaa.
Hoteli hizi kubwa hazijafungwa sababu wateja wake kwa asilimia kubwa wanatoka nje ya nchi ambako hakuna Magufuli na siasa zake za kubadili hela.
Zinazotegemea wateja wa humu humu ndiyo zinalazimika kufungwa kutokana aina ya uteja wake.

Mkuu toa basi na suluhisho la kutibu ugonjwa.

Mimi naamini tulipokuwa tumefikia inabidi tuvurugane kwanza kisha mambo yakae vizuri. Sijaona Serena ikifungwa, sinaona Hyatt Regency ikifungwa. Zinazofungwa ni zile za deal, zile zilizokuwa zinategemea deal toka serikalini. Zile zilizokuwa zinategemea mikutano ya serikali kwa gharama kubwa ambazo zilihusisha cha juu!! Unakuta Ofisi nzima anahamia hotelini ili kufanyia kazi huko kwa wiki nne; wanalala, wanakunywa na kucheza muziki bili ikija ni mamilioni na waliohusika kuandaa wanachekelea njia nzima kwenda kujinyakulia cha juu.
 
Kwa hiyo suala ni kupandishwa kwa kodi? Mimi nimesema kuwa kulikuwa na masuala ya deal kati ya wenye hotel na wenye maamuzi serikalini. Hakika nakuambia hata kama kodi ingepanda kiasi gani lakini serikali ikaendelea na mtindo wake ambapo Ofisi zilikuwa zinahamia mahotelini, hizo hotel wala zisingetikisika hata chembe.

Pia waulize kwamba kuna sababu zozote za hao wanaofunga au kuuza hizo hotels wametaja? Na je wanaweza kutuambia nia biashara ngapi zinafunguliwa kila siku?

Maana naona kuna watu wanaandika tu hisia zao bila kuwa na takwimu mradi tu wafurahishe hisia zao.
 
Kama ni kuambiwa anaambiwa sana tuu! ,tatizo ni kuamini analoambiwa! .

Ukishajenga pre conceived negativity kuwa watu ni wezi!, then hata ukiambiwa hakuna any economical activities za kusisimua uchumi, utaamini watu wanaiba hizo activities!.

Pasco
Pasco nakuapia hakuna mwenye ubavu wa kumwambia, wanaogopa watatumbuliwa. You keep silent as long as you are getting your bread!
 
mkuu
Mkuu toa basi na suluhisho la kutibu ugonjwa.

Mimi naamini tulipokuwa tumefikia inabidi tuvurugane kwanza kisha mambo yakae vizuri. Sijaona Serena ikifungwa, sinaona Hyatt Regency ikifungwa. Zinazofungwa ni zile za deal, zile zilizokuwa zinategemea deal toka serikalini. Zile zilizokuwa zinategemea mikutano ya serikali kwa gharama kubwa ambazo zilihusisha cha juu!! Unakuta Ofisi nzima anahamia hotelini ili kufanyia kazi huko kwa wiki nne; wanalala, wanakunywa na kucheza muziki bili ikija ni mamilioni na waliohusika kuandaa wanachekelea njia nzima kwenda kujinyakulia cha juu.
mkuu sometime acha ushabiki wa kijinga hizo hotel unazosema hujasikia hazijafungwa ni watanzania wangapi kwa siku wanazitumia kama si wageni asilimia 99 kutoka nje tena ya nchi
pili uchumi maana ya consumption unaanza na serikali ili watu wapate heka ni lazima serikali i spend
tatu hamna serikali yyte duniani unaweza juzuia mambo ya dili kama ambavyo watu hawawezi kuwa sawa duniani kinachofanyika ni kupinguza kiwango cha hayo madili na ndio maana unakuta takwimu za mambo mbalimbali kama rushwa,hali za usalama wa nchi,vipato vya watu takwimu hotolewa kwa viwango.
hivi kama magufuli anafanya vizuri ni kwa nini kila mwenye uwezo n ava uelewa wa mambo wakusema ana nini!! mbona kuna watu kama akina sokoine na nyerere mbona hata kama si mwanachama wa ccm tunawasifia.na jua tunamsema magufuli kwa sababu kauli na matendo yake yanatuletea madhara mpaka kwenye maisha ya mtu moja moja.tafadhali isiwe mfano wa watu ambae bibilia ok nasema una macho lakini huoni ina masikio lakini husikii.hata kama upendi upinzani haikufanyi kukubali kila kitu hata kama ni cha hovyo ila kwa sababu ya mapenzi na ccm
 
Kuna vitu ukiviamini kwa asilimia 100 basi ni ngumu sana mtu mwingine kuja kukuambia vinginevyo.Ni sawa na mtu ambae anaumwa halafu anaamini 'kalogwa'

Mtu huyu hata umpeleke hospitali atakua tu bado anaamini 'kuna mkono wa mtu.

Ikitokea hospitali wamesema 'hana malaria' ndo kabisaa atazidi kuamini ni 'mkono wa mtu'.

Hadi itokee mtu mwingine ambae anaweza kumsikiliza ashauri 'hebu pima na typhoid' au 'pima UTI..' na akutwe na magonjwa apewe dawa apone ndo unaweza kidoogo kumfanya akusikilize vinginevyo watu dizaini hii wanaweza kufa au kusababisha kifo cha mtoto au ndugu anaeumwa.

Sasa hoteli zinafungwa na zingine zinauzwa, biashara zinakufa kwa wingi
pesa imepotea lakini Rais anaamini kuna 'hujuma' na dawa ni kuanza msako wa 'walioficha hela majumbani' au kuchapisha noti au kubadili noti.

Cha ajabu 'madaktari ' wetu nao wa kumwambia 'ukweli' kuhusu 'ugonjwa'
wako kiimya kabisa tunapiga ramli wakati magonjwa haya yana vipimo vyake
na dawa zake zinajulikana.

Hadi 'mgonjwa' afe ndo waje kusema ilikuwa 'typhoid'?
Kama hayo mahotel na hizo biashara zilikuwa zinafanya kazi kiuhalali pasingekuwa na hotel kufungwa wala biashara kufa.sijasikia kiongozi yeyote aliyetamka ya kuwa wateja wanaoingia ktk mahotel wazuiwe wala wafanya biashara wazuiwe kufanya biashara. Je uliwahi jiuliza kwa nini? Sasa kati ya yeye na wewe nani kalogwa na hajui kama anaumwa.
 
Back
Top Bottom