Mkuu toa basi na suluhisho la kutibu ugonjwa.
Mimi naamini tulipokuwa tumefikia inabidi tuvurugane kwanza kisha mambo yakae vizuri. Sijaona Serena ikifungwa, sinaona Hyatt Regency ikifungwa. Zinazofungwa ni zile za deal, zile zilizokuwa zinategemea deal toka serikalini. Zile zilizokuwa zinategemea mikutano ya serikali kwa gharama kubwa ambazo zilihusisha cha juu!! Unakuta Ofisi nzima anahamia hotelini ili kufanyia kazi huko kwa wiki nne; wanalala, wanakunywa na kucheza muziki bili ikija ni mamilioni na waliohusika kuandaa wanachekelea njia nzima kwenda kujinyakulia cha juu.