IJue U.T.I ,chanzo, dalili, madhara na tiba

IJue U.T.I ,chanzo, dalili, madhara na tiba

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,812
Reaction score
2,737
WhatsApp Image 2026-07-25 at 11.48.02.jpeg


U.T.I NI NINI

U.T.I. (yaani Urinary Tract Infection kwa kirefu) ni ugonjwa unaotokana na maambukizi (infection) katika mfumo wa mkojo (urinary tract). Maambukizi haya yanasababishwa na bakteria tunamuita E.coli

ZIPI DALILI KUJUA UNA U.T.I
1. Kukojoa mara kwa mara na maumivu ukikojoa. Wengi wanajisikia hivyo lakini wanapotezea tu.
2. Kuhisi kuunguzwa na mkojo kwenye kibofu au mrija wa mkojo. Wengi Hapa ndo hujiuliza kuna nini.
3. Maumivu ya misuli na tumbo. Wengi hapa ndo wanakodi bajaji kwenda hospitali.
4. Mkojo kuwa na harufu mbaya na pia kubadilika rangi kuwa njano nyeusi . Wengi hii hawajali. Ndo maana vyoo vya umma vina harufu mbaya mbaya.
5. Kwa mtu aliyeathiriwa figo anaweza kuwa na maumivu mgongoni au kwenye mbavu (hasa upande mmoja) pia kichefuchefu na kutapika. Wengi hapa wanajua malaria, au typhoid, nk.
6. Kushikwa na hamu ya kukojoa ila mkojo unatoka kidogo. Wengi hii pia huwapa hofu kidogo.
(Ukiona dalili hizo wahi hospitali kwanza au kituo cha afya ukapime. Ukichelewa inaweza kuwa too late)


NINI MADHARA YA KUCHELEWA KUTIBU U.T.I
1.U.T.I. hizi zinaathiri hadi mfumo wa uzazi na hapo wanandoa hupaswa kupata tiba kwa pamoja.
2.U.T.I huleta maumivu ya mgongo na mbavu hivyo unashindwa kufanya kazi, na kurudi nyuma kimaendeleo
3.U.T.I Ikifika hatua ya juu inaathiri kibofu,figo na inaua


KWA VIPI U.T.I INAKUWA SUGU (INAJIRUDIA RUDIA)
Bakteria hawa waitwao E.coli wana uwezo mkubwa mno wa kujishika kwenye
njia ya mkojo hasa kinga za mwili zinaposhuka. Hivyo dawa nyingi unazotumia, zinasafisha njia na kuua bakteria kidogo na kuacha wengine wakizaliana na kurudia tena kukuambukiza.

MIMEA TIBA
Mchanganyiok wa ,imea ya bottle brush na bidens pilosa (mashona nguo) imeonesha mafanikio makubwa kumaliza maambukizi ya bakteria hawa wanaosababisha UTI kuwa sugu.

bidens pilosa.jpeg
bottlebrush_image.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom