Kwanza kabisa nilishangaa sana namna baadhi ya Vyombo vya Habari vilivyoliwasilisha suala la noti mpya. Kwa namna Mh. Rais alivyozungumza kuhusu suala hili, sikutaraji kabisa Vyombo vya Habari hivyo kuupa Umma tafsiri isiyo ya kweli katika suala hili la noti mpya: Mhe. Rais alizungumza mambo ya msingi sana ili kuamsha hali ya uzalendo kwa walengwa aliokuwa akiwahutubia siku ile, lakini nashangaa sana kuona baadhi ya Vyombo vya Habari havitaki kuyamulika mambo hayo ya msingi ila vimejikita kueneza tafsiri isiyo ya kweli katika kile alichokizungumza Mhe. Rais kuhusu noti mpya. Baadhi yetu tunashangaa sana. Nina hakika kama hotuba ile ya Mhe. Rais itarushwa yote, basi watu wataujua ukweli ambao Mhe. Rais aliutoa siku ile.