Rais Magufuli na Jaji Mkuu Siku ya Sheria: Msongamano wa kesi Mahakama ya Rufani kikwazo cha kupata haki

Kisanduku

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
284
482
Siku ya sheria imekaribia na Rais Magufuli atahutubia na jaji Mkuu atahutubia.

Hatujui Rais atasema nini lakini ni wazi hotuba ya Jaji Mkuu itasheheni historia ya Mahakama Kuu (High Court) kwa miaka hii 100. Hongera sana Mahakama Kuu.

Hakuna majaji watenda haki kama Mahakama ya Rufani. Ukiwa na kesi yako Mahakama ya Rufani pale tarajia kupata haki yako kiusahihi. Hongera sana majaji wa Mahakama ya Rufani, wanaitwa Justice of Appeal.

Lakini pamoja na mafanikio hayo lipo tatizo sugu katika Mahakama ya Rufani yaani Court of Appeal.

Shida kubwa pale Mahakama ya Rufani ni msongamano (backlog) wa kesi zilizojazana pale. Kama kesi ilichukua miaka minne huku mahakama za chini, ukiongeza na miaka itayosubiri pale Mahakama ya Rufani basi tarajia hata miaka minane kupata haki yako.

Mawakili wajanja wanajua uchelewaji huu. Wanajua ukiwashida kesi wanaenda Mahakama ya Rufani. Wanajua pale hawashindi kesi lakini watakuwa wamefaulu kukuchelewesha kwa miaka mitatu kesi itakapokaa pale.

Watu wakisikia kesi inaenda Court of Appeal wanakata tamaa. Si kwamba watashindwa kesi pale bali wameshajua itachelewa kwa miaka miwili au mitatu. Leo hii kuna kesi za mwaka 2013 eti ndiyo zinasikilizwa mwaka huu!

Hivyo hili ni tatizo la kila mmoja. Mahamakani ni kama hospitalini ambako unaweza kujikuta unafikishwa bila kutarajia.

Hivyo kila mtanzania ni mkatarufani mtarajiwa (appellant) au mkatiwarufani mtarajiwa (respondent). Wapo wanaokufa kwa pressure kwa sababu kesi zao zimerundikana mahakamani.

Kesi kurundikana pale kuna maana nyingi lakini maana kuu ni kushindwa kwa mfumo wa mahakama.

Maana mojawapo ni kwamba mahakama za chini kama Mahakama Kuu (High Court) zimejaa uonevu ndiyo sababu sasa watu wanakimbilia Court of Appeal.

Hakimu au Jaji wa Mahakama Kuu (High Court) anaweza kupindisha haki makusudi akijua hata ukienda Mahakama ya Rufani utasota mitatu hadi kubadili maamuzi yake.

Mahakama hii ina majaji (Justice of Appeal) zaidi ya 20. Kwa idadi hii Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa Mahakama ya Rufani kuwa na majaji wengi.

Tulitarajia kwa wingi huu tuongoze kwa kutokuwepo msongamano wa kesi pale Court of Appeal. Kinyume chake pale ndipo panapoongoza kwa msongamano utadhani kesi huwa zinaanzia pale.

Namalizia. majaji wa Mahakama ya Rufani ni wasafi kimaadili na watenda haki. Lakini hili la ucheleweshaji kesi linaharibu sifa nzuri ya Mahakama ya Rufani.

Tunaomba Jaji Mkuu alizingatie hili. Atakapohutubia keshokutwa walau aseme wamejipangaje kuondoa kabisa msongamano uliopo ili Court of Appeal pasiwe tena chombo cha kuchelewesha kesi.
 
Kweli kabisa asee kesi Zinakaa sana pale kupitia rufani utasota hadi ukate tamaa...tunataka kusikia mkakati wao JR wameonfezwa Sana lkn kesi hazipungui
 
Hakuna cha manpower ndogo. Nimesema kwamba Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa Supreme Court kuwa na majaji wengi.
Unajua idadi ya kesi za court of appeal mpaka sasa!!??
unajua idadi ya majaji wa court of appeal...!!!?
hujui.....
 
Ripoti ya mwaka jana inaonyesha kesi zaidi ya 1000 pale Mahakama ya Rufani.

Majaji pale hawapumziki huenda ndiyo sababu wengine wanapatwa kisukari au ugonjwa wa moyo.

Unajua idadi ya kesi za court of appeal mpaka sasa!!??
unajua idadi ya majaji wa court of appeal...!!!?
hujui.....
 
Ripoti ya mwaka jana inaonyesha kesi zaidi ya 1000 pale Mahakama ya Rufani.

Majaji pale hawapumziki huenda ndiyo sababu wengine wanapatwa kisukari au ugonjwa wa moyo.
Hakuna kitu hapo. Tuambie zilifikaje 1000? Ni wastani wa kesi ngapi zinakatwa Mahakama ya Rufani kwa mwezi? Huko kuna presentation kama Mahakama Kuu? Nambie ile kesi ya kupinga wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi ilipataje kusikilizwa rufani yake wakati leo zinasikilizwa za 2013?
Kisanduku hiyo Mahakama ilikuwa zamani. Haipo tena. Kuna mmoja tu anatawala vyombo vyote vya dola. Hakuna Mahakama wala Bunge. Mhimili uliojichimbia zaidi kazini!
 
Presentation pale haipo ila pana Written Submission ambayo unnandika kabla ya siku ya kusikilizwa. Tena siku hizi kama unajiamini ukishaandika unaweza usiende kusikilizwa.

Wanasoma tu Written Submission wanatoa Judegment.

Hivyo kushughulikia kesi yako ni siku moja tu tena haizidi hata saa moja kesi imeisha.

Tabu ni kuipata hiyo siku ya kusikilizwa.

Kuhusu wastani wa kesi kusikilizwa wastani unakaribia kesi 100 kwa mwezi.

Hili Jaji Mkuu huwa halisemi sijui kwa nini.

Hakuna kitu hapo. Tuambie zilifikaje 1000? Ni wastani wa kesi ngapi zinakatwa Mahakama ya Rufani kwa mwezi? Huko kuna presentation kama Mahakama Kuu? Nambie ile kesi ya kupinga wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi ilipataje kusikilizwa rufani yake wakati leo zinasikilizwa za 2013?
Kisanduku hiyo Mahakama ilikuwa zamani. Haipo tena. Kuna mmoja tu anatawala vyombo vyote vya dola. Hakuna Mahakama wala Bunge. Mhimili uliojichimbia zaidi kazini!
 
Asante kwa kuliona hili kuwa kuchelewa kutolewa kwa maamuzi Mahakamani au kucheleweshwa kwa haki kuamuliwa ni sawasawa na kukatiliwa au kunyimwa haki.

Ili limekuwa ni tatizo kubwa sana kwenye legal system kwenye nchi ya Tanzania ambapo jambo likipelekwa kwenye vyombo vya kutolea maamuzi kisheria maamuzi yanachelewa mpaka kupelekea wahusika kukataa tamaa na wengine kupelekea kupata stress na pengine mpaka kifo.

Hili jambo la ucheleweshaji wa maamuzi halipo mahakamani tu, pia hili jambo limetokea sana kwenye maeneo mengine ya kutafuta haki kama vile TUME YA UTUMISHI WA UMMA. Kama kungekuwa na uwezekano wa kuifanyia mabadiliko hii TUME basi Mh. Rais anaombwa aliangalie kwa macho mawili; hii TUME iko slow sana kwenye kutoa maamuzi, hii TUME mara nyingi inakuwa bias bila ku-base kwenye hoja ambayo mtumishi amepeleka na kuamua kuwa corrupted na waajiri, eti kuna baadhi ya wajumbe wa TUME kwa maana ya Commissioners wanakuwa corrupted na wanarubuniwa na waajiri ili kuwakandamiza waajiriwa juu ya masuala yao yanayopelekwa TUME YA UTUMISHI WA UMMA kwa maana ya rufaa.
 
Safari ijayo nitauleta uzi hapa kwa great thinkers utakaohusu utendaji wa TUME YA UTUMISHI WA UMMA tu ili great thinkers walichambue hili jambo kwa makini ili kama hii TUME inafanya kazi ipasavyo ya kutenda haki na hatimae kumsaidia Mh. Rais au laa!! na nini kinatakiwa kifanyike.
 
Sawa. Lakini nilivyomwelewa mleta mada kasema kuhusu Court of Appeal huku kesho ikiwa siku ya kuanza mwaka mpya wa Mahakama.

Safari ijayo nitauleta uzi hapa kwa great thinkers utakaohusu utendaji wa TUME YA UTUMISHI WA UMMA tu ili great thinkers walichambue hili jambo kwa makini ili kama hii TUME inafanya kazi ipasavyo ya kutenda haki na hatimae kumsaidia Mh. Rais au laa!! na nini kinatakiwa kifanyike.
 
Law day imepita na mmesikia kila kitu. Sasa mmeelewa nilimaanisha nini
 
Back
Top Bottom