Siku ya sheria imekaribia na Rais Magufuli atahutubia na jaji Mkuu atahutubia.
Hatujui Rais atasema nini lakini ni wazi hotuba ya Jaji Mkuu itasheheni historia ya Mahakama Kuu (High Court) kwa miaka hii 100. Hongera sana Mahakama Kuu.
Hakuna majaji watenda haki kama Mahakama ya Rufani. Ukiwa na kesi yako Mahakama ya Rufani pale tarajia kupata haki yako kiusahihi. Hongera sana majaji wa Mahakama ya Rufani, wanaitwa Justice of Appeal.
Lakini pamoja na mafanikio hayo lipo tatizo sugu katika Mahakama ya Rufani yaani Court of Appeal.
Shida kubwa pale Mahakama ya Rufani ni msongamano (backlog) wa kesi zilizojazana pale. Kama kesi ilichukua miaka minne huku mahakama za chini, ukiongeza na miaka itayosubiri pale Mahakama ya Rufani basi tarajia hata miaka minane kupata haki yako.
Mawakili wajanja wanajua uchelewaji huu. Wanajua ukiwashida kesi wanaenda Mahakama ya Rufani. Wanajua pale hawashindi kesi lakini watakuwa wamefaulu kukuchelewesha kwa miaka mitatu kesi itakapokaa pale.
Watu wakisikia kesi inaenda Court of Appeal wanakata tamaa. Si kwamba watashindwa kesi pale bali wameshajua itachelewa kwa miaka miwili au mitatu. Leo hii kuna kesi za mwaka 2013 eti ndiyo zinasikilizwa mwaka huu!
Hivyo hili ni tatizo la kila mmoja. Mahamakani ni kama hospitalini ambako unaweza kujikuta unafikishwa bila kutarajia.
Hivyo kila mtanzania ni mkatarufani mtarajiwa (appellant) au mkatiwarufani mtarajiwa (respondent). Wapo wanaokufa kwa pressure kwa sababu kesi zao zimerundikana mahakamani.
Kesi kurundikana pale kuna maana nyingi lakini maana kuu ni kushindwa kwa mfumo wa mahakama.
Maana mojawapo ni kwamba mahakama za chini kama Mahakama Kuu (High Court) zimejaa uonevu ndiyo sababu sasa watu wanakimbilia Court of Appeal.
Hakimu au Jaji wa Mahakama Kuu (High Court) anaweza kupindisha haki makusudi akijua hata ukienda Mahakama ya Rufani utasota mitatu hadi kubadili maamuzi yake.
Mahakama hii ina majaji (Justice of Appeal) zaidi ya 20. Kwa idadi hii Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa Mahakama ya Rufani kuwa na majaji wengi.
Tulitarajia kwa wingi huu tuongoze kwa kutokuwepo msongamano wa kesi pale Court of Appeal. Kinyume chake pale ndipo panapoongoza kwa msongamano utadhani kesi huwa zinaanzia pale.
Namalizia. majaji wa Mahakama ya Rufani ni wasafi kimaadili na watenda haki. Lakini hili la ucheleweshaji kesi linaharibu sifa nzuri ya Mahakama ya Rufani.
Tunaomba Jaji Mkuu alizingatie hili. Atakapohutubia keshokutwa walau aseme wamejipangaje kuondoa kabisa msongamano uliopo ili Court of Appeal pasiwe tena chombo cha kuchelewesha kesi.