Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,808
- 11,973
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewateua Majaji wa Mahakama ya Rufaa wafuatao: -
- Amemteua Jaji Zainab Goronya Muruke kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Muruke alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi cha Mashauri ya Ndoa, Talaka na Mirathi - Temeke, Dares Salaam;
- Amemteua Jaji Dkt. Benhaji Shaaban Masoud kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Masoud alikuwa Mkuu wa Shule ya Sheria Tanzania;
- Amemteua laji Amour Said Khamis kuwa Jaii wa Mahakama va Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Khamis alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora;
- Amemteua Jaji Leila Edith Mgonya kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mgonya alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Masijala Kuu Dar es Salaam;
- Amemteua Jaji Gerson John Mdemu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mdemu alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma; na
- Amemteua Jaji Agnes Zephania Mgeyekwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mgeyekwa alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi.