Fatma Karume akwama Mahakama ya Rufani kesi ya kupinga kuvuliwa uwakili

lord atkin

Senior Member
Sep 30, 2018
197
683
Hatimaye Mahakama ya Rufani, (Highest Court of the Land), almaarufu "an Appex Court" imetupilia mbali maombi ya wakili machachari Fatma Karume kupinga uamuzi wa Jaji kiongozi kumsimamisha uwakili.

Katika kesi hiyo Fatma Karume alikuwa akiwakilishwa na mawakili wasomi Peter Kibatala na Rugemeleza Nshala, huku Jaji kiongozi na AG wakiwakilishwa na Deborah Mcharo, learned State Attorney.

Mahakama ya Rufani imekubaliana na pingamizi la nne lililoibuliwa na Wakili wa serikali kwamba kesi hiyo imekuwa misconceived kwa Mwombaji kupinga kwa njia marejeo uamuzi wa Jaji kiongozi kwa njia ya maombi ya marejeo badala ya kupinga uamuzi huo wa kusimamishwa uwakili Mahakama kuu kama kifungu cha 22 cha Sheria ya mawakili kinavyotaka.

HISTORIA YA HILI SAKATA

1. Jaji Kiongozi Feleshi (as he then was) alimsimamisha Fatma Karume kupractice uwakili na kumripoti kwenye kamati ya nidhamu ya Mawakili .

2. Kamati ya nidhamu ya mawakili yenyewe ilienda mbali zaidi kwa kumfutia kabisa uwakili Fatma Karume. Uamuzi huu ulitolewa bila Fatma Karume kupewa nafasi ya kujitetea katika kamati.

3. Fatma Karume alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa kamati ya nidhamu ya mawakili kwa Mahakama kuu jopo la majaji watatu. Mahakama kuu, Jopo la majaji watatu lilitengua maamuzi ya kamati ya mawakili na kuamuru kamati isikilize upya ili Fatma Karume apate haki ya kujitetea.

4. Mahakama ya Rufani
Katika hali isiyo ya kawaida wakati kamati ikiamriwa isikilize upya shauri la Fatma Karume, yeye na mawakili wake walikimbilia Mahakama ya Rufani wakiomba marejeo siyo ya maamuzi ya Mahakama kuu, Jopo la majaji watatu tena lahasha, waliomba marejeo ya uamuzi wa awali kabisa wa Jaji Kiongozi.

5. Maamuzi ya Mahakama ya Rufani

Kwa maamuzi haya sasa ni wazi kwamba hata Jaji Kiongozi Feleshi alikosea kumripoti Fatma Karume kwenye Kamati ya Mawakili na kila kitu kilichoendelea katika kamati ya mawakili mpaka Mahakama kuu Jopo la Majaji watatu ni ubatili. Mahakama ya Rufani ina maoni kwamba Fatma Karume alipaswa kuomba Mahakama kuu itengue suspension ya Jaji kiongozi kama kifungu cha 22 (2) (b) cha Sheria ya Mawakili kinavyotaka na si kuomba Marejeo Mahakama ya Rufani moja kwa moja na wala haikupaswa kwenda kamati ya mawakili.

View attachment 2670926
Screenshot_20230627-221228.jpg
View attachment 2670927
 
Hatimaye Mahakama ya Rufani, (Highest Court of the Land), almaarufu "an Appex Court" imetupilia mbali maombi ya wakili machachari Fatma Karume kupinga uamuzi wa Jaji kiongozi kumsimamisha uwakili.

Katika kesi hiyo Fatma Karume alikuwa akiwakilishwa na mawakili wasomi Peter Kibatala na Rugemeleza Nshala, huku Jaji kiongozi na AG wakiwakilishwa na Deborah Mcharo, learned State Attorney.

Mahakama ya Rufani imekubaliana na pingamizi la nne lililoibuliwa na Wakili wa serikali kwamba kesi hiyo imekuwa misconceived kwa Mwombaji kupinga kwa njia uamuzi wa Jaji kiongozi kwa njia ya maombi ya marejeo badala ya kupinga uamuzi huo wa kusimamishwa uwakili Mahakama kuu kama kifungu cha 22 cha Sheria ya mawakili kinavyotaka. View attachment 2670926View attachment 2670928View attachment 2670927
Huyu aendelee kubwabwaja Twitter tuu
 
Inawezekanaje mawakili wasomi hivi wanashindwa kung'amua technicalities kama hizi?!
 
Dada Fatuma yupo vizuri sana katika sheria.

Ila ulimi wake una ukaraha kama vile babu zake hawajamwaga damu za watu na sijawahi msikia akilisemea hilo.

Wakina FERESHIccm mpeni leseni yake dada yetu mpendwa.
 
Hatimaye Mahakama ya Rufani, (Highest Court of the Land), almaarufu "an Appex Court" imetupilia mbali maombi ya wakili machachari Fatma Karume kupinga uamuzi wa Jaji kiongozi kumsimamisha uwakili.

Katika kesi hiyo Fatma Karume alikuwa akiwakilishwa na mawakili wasomi Peter Kibatala na Rugemeleza Nshala, huku Jaji kiongozi na AG wakiwakilishwa na Deborah Mcharo, learned State Attorney.

Mahakama ya Rufani imekubaliana na pingamizi la nne lililoibuliwa na Wakili wa serikali kwamba kesi hiyo imekuwa misconceived kwa Mwombaji kupinga kwa njia marejeo uamuzi wa Jaji kiongozi kwa njia ya maombi ya marejeo badala ya kupinga uamuzi huo wa kusimamishwa uwakili Mahakama kuu kama kifungu cha 22 cha Sheria ya mawakili kinavyotaka.

HISTORIA YA HILI SAKATA

1. Jaji Kiongozi Feleshi (as he then was) alimsimamisha Fatma Karume kupractice uwakili na kumripoti kwenye kamati ya nidhamu ya Mawakili .

2. Kamati ya nidhamu ya mawakili yenyewe ilienda mbali zaidi kwa kumfutia kabisa uwakili Fatma Karume. Uamuzi huu ulitolewa bila Fatma Karume kupewa nafasi ya kujitetea katika kamati.

3. Fatma Karume alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa kamati ya nidhamu ya mawakili kwa Mahakama kuu jopo la majaji watatu. Mahakama kuu, Jopo la majaji watatu lilitengua maamuzi ya kamati ya mawakili na kuamuru kamati isikilize upya ili Fatma Karume apate haki ya kujitetea.

4. Mahakama ya Rufani
Katika hali isiyo ya kawaida wakati kamati ikiamriwa isikilize upya shauri la Fatma Karume, yeye na mawakili wake walikimbilia Mahakama ya Rufani wakiomba marejeo siyo ya maamuzi ya Mahakama kuu, Jopo la majaji watatu tena lahasha, waliomba marejeo ya uamuzi wa awali kabisa wa Jaji Kiongozi.

5. Maamuzi ya Mahakama ya Rufani

Kwa maamuzi haya sasa ni wazi kwamba hata Jaji Kiongozi Feleshi alikosea kumripoti Fatma Karume kwenye Kamati ya Mawakili na kila kitu kilichoendelea katika kamati ya mawakili mpaka Mahakama kuu Jopo la Majaji watatu ni ubatili. Mahakama ya Rufani ina maoni kwamba Fatma Karume alipaswa kuomba Mahakama kuu itengue suspension ya Jaji kiongozi kama kifungu cha 22 (2) (b) cha Sheria ya Mawakili kinavyotaka na si kuomba Marejeo Mahakama ya Rufani moja kwa moja na wala haikupaswa kwenda kamati ya mawakili.

View attachment 2670926View attachment 2670928View attachment 2670927
Tatizo la huyu dada ni kidomodomo chake.
Haijulikani kama ni wakili, mtetezi wa Zenj, mwanasiasa au mwanaharakati.
Maneno too much!
Hana mume?
 
Back
Top Bottom