Rais Magufuli, mambo unayoyafanya yatadumu?

Rais Magufuli, mambo unayoyafanya yatadumu?

Na mimi mfanyakazi wa nchi hii na ambaye sijawahi kushuhudia nyongeza ya mshahara, wala kupandishwa daraja tangu mwaka 2015 ninaweza kweli kumsifia Magufuli! eti ana mazuri aliyonitendea tangu alipochaguliwa kuwa Rais !!

Labda kwa kunisaidia kumaliza deni langu la bodi mapema kuliko ilivyokua enzi za JK kwa kuniongezea asilimia za makato mpaka kufikia 15% kinyume kabisa na mkataba nilio ingia nao hapo awali!

Katika demokrasia, ni wananchi wenye maamuzi ya mtu sahihi wa kuwaongoza. Demokrasia huwapa wananchi nguvu na uwezo wa kupima viongozi na wagombea uongozi kama kweli ni waadilifu (sio wao kujinadi uadilifu) na kisha kuamua kupitia chaguzi makini nani awaongoze; nani apumzishwe.

Ni tawala za kikomunisti/kidikteta ndizo huandaa na kuteua wateule kupokea uongozi kiimla kwa kutumia nguvu za dola. Uadilifu na ufisadi hupimwa katika mizania ya propaganda. Ukweli huwa mhanga wa kwanza katika tawala hizi.
 
Nakuhakikishia kama Magu angeendelea miaka 20 ijayo nchi hii ingegeuka kuwa uwanja wa vita manake kuna kukosekana kwa haki mno kuliko wakati mwingine wowote hilo halina mjadala. Pia jiwe amekuwa akifanya mambo kwa matamshi bila kujenga mifumo itakayodumu. Hivyo akiondoka na yake yataondoka naye hata kama ni mazuri kwani hajui na hafanyi uongozi kwa manufaa ya vizazi vijavyo ila kwa manufaa yake ya sasa ya kisiasa.
 
Mimi sina tatizo hata rais akitokea chama kingine. Ninachomaanisha Rais awapendekeze watu waadilifu kupitia chama chake. Rais Magufuli hana mamlaka yoyote kwenye vyama vya upinzani kwahiyo ni juu ya wapinzani kuchagua watu wanaofaa.
Confused man with confused thinking! Soma hizo za kwako tena kwa makini. Ukishindwa kuelewa namaanisha nini, omba msaada. Kuna shida kubwa!
 
Tz hatuna mfumo endelevu kila ajae huja na yake,ataingia muislamu Kama ilivozoeleka.Waislamu huwa na utu wote tunashiba,usipojenga kipindi Chao utojenga tena, wakristo awatupi makombo chini vyoote uishia mezani kwa wateule.Mapaka,mbwa,nk waliouvunguni chini ya meza wote ni kilio cha njaa, waislamu ukumbuka kutupa makombo chini angalau viumbe vingine navyo vishibe.
 
Katika Inchi zilizoendeea SHERIA na kanuni KUU za mfumo wa uchumi wa Inchi unawekwa kwenye katiba ya Inchi.
Katika utekelezaji wake ni lazima kuwe na mfumo maalumu ambao unawashirikisha wengi ili wasiende kinyume na katiba ya Inchi.
Katika Dunia ya Tatu kila kiongozi mkuu wa Inchi anakuja na mfumo tofauti wa kanuni na SHERIA za uchumi wa Inchi.
Rais aliyeko madarakani anaweza kufanya jambo lolote hata kama linamadhara makubwa kwa Uchumi wa iNCHI na watu wakabaki wanalalamika tu bila kuwa na nguvu ya kumwadhibu au kumwondoa madarakani.
Nchi za dunia ya tatu utumia mifumo ya kikomunisti na kijamaa yaan mtawala kuwa na nguvu kuliko Mungu.
 
Magu anamfumo wa give law and i will give you oders not law and orders na huu mfumo ndio unao kisumbua chama sasa hivi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom