James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,205
- 1,509
Sina uhakika kama hiki ninachokiandika kitamfikia rais lakini angalau Watanzania watajua kinachoweza kutokea huko mbeleni.
Binafsi naona Rais Magufuli anapambana na UZEMBE NA RUSHWA kuliko marais wote waliopata kuiongoza Tanzania. Sikubaliani naye kwa kila kitu lakini kwa hili namsifia.
Kitu kinachonipa shida ni baada ya Rais Magufuli kumaliza muda wake. Je, Rais atakayemfuatia atafuata nyayo zake? Hili swali linanipa wasiwasi. Hivi rais Magufuli utajisikiaje kama rais atakayefuata atayafutilia mbali yale mazuri uliyoyaanza? Kazi yote uliyoifanya itakuwa ni sifuri. Ni sawa na kupiga hatua mbili mbele halafu hatua tatu nyuma.
Kutatua jambo hili yafaa kuwe na succession plan. Inabidi waanze kuandaliwa watu waadilifu kuanzia sasa ili nchi isije kuangukia kwenye wrong hands.
Mungu ibariki Tanzania.