Rais Magufuli na Goliath wa Tanzania

MAR MATARE

New Member
Oct 2, 2016
4
6
RAIS MAGUFULI NA GOLIATHI WA TANZANIA

Awali ya yote ni vizuri nikatangaza kwamba mimi si mwanachama wa chama chochote na ninayempenda sana Dr. John Magufuli kwa matendo yake na kazi zake toka akiwa Naibu Waziri mpaka alipo sasa.Wapo watu wanaoweza kudai kwamba inawezekana ninajipendekeza kwake. Lakini Januari mwaka 2013, miaka miwili kabla Dr. Magufuli hajawa Rais na wala kufikiriwa kama atakuwa Rais wa nchi yetu, nilitoa hotuba ya saa moja nikielezea nilivyokuwa ninampenda Dr. Magufuli kwa kazi yake nzuri na kwamba ndiye angekuwa Rais na nikaelezea serikali ambayo angeiunda ingekuwaje na ndivyo ilivyokuwa hatua kwa hatua. Hotuba hiyo niliitoa kwenye sherehe ya mahafali ya kidato cha sita 2013 katika shule ya sekondari Beroya iliyoko Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.Shule hiyo inamilikiwa na Sebastian Muungano Waryuba ambaye ameteuliwa kuwa DC wa Tandahimba. Mgeni rasmi siku hiyo alikuwa DC wa Songea wakati huo Joseph Joseph Mkirikiti ambaye ameteuliwa kuwa DC Rwangwa. Hotuba hiyo ilitolewa mbele ya wanafunzi wote wa shule hiyo kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha sita na mbele ya wazazi wao.Ninajua kwamba wapo watu wanaoweza kuthibitisha ukweli huo. Wakati huo mimi nilikuwa mkuu wa shule hiyo. Nikamwomba mkuu huyo mpya awe kama Dr. Magufuli ili kusaidia watanzania. Inawezekana aliniskia maana ameteuliwa na Magufuli! Ukuu wangu ulisitishwa baada ya wiki moja tu! Mwaka huo huo 2013 nikajiunga na Chadema. Siku moja tukiwa watu wanne safarini kutoka Mtwara: Benson Kigaila ambaye alikuwa Mkurugenzi wa mafunzo wa Chadema, Richard Shaba ambaye alikuwa ni mwakilishi wa shirika la Konrad ambalo linaisaidia Chadema kutoka nchini Ujerumani, Philbert Ngatunga ambaye alikuwa Afisa wa Kanda ya kusini na mimi nikiwa mwenyekiti wa Chadema Kanda ya kusini nilitamka wazi wazi kukiwa kwenye gari la Richard Shaba kwamba hapa tulipofikia mtu anayeweza kubadili mwelekeo wa nchi hii ni Dr. Magufuli peke yake. Tulibishana na Benson kwa muda wa nusu saa halafu hakuna aliyeongea na mwingine kutoka Kilwa mpaka Dar es Salaam na ukawa ndio mwisho wangu kuwa Chadema.Kwa bahati nzuri hao wote wako hai wanaweza kuthibitisha. Nimemtumia mheshimiwa Dr. Magufuli CD ya hotuba hiyo kupitia kwa Waziri Mkuu kama sehemu ya mchango wangu wa mawazo katika kuitafutia Tanzania yaliyo mema. Naomba Mheshimiwa Rais aisikilize hatuba yangu hiyo mpaka mwisho atafarijika kuona kuwa kumbe katika safari yake ya uongozi hakuwa peke yake bali kulikuwa na watu waliokuwa nyuma yake na mpaka sasa tunafuatilia kwa karibu utendaji wake

. Je, Dr. Magufuli alitarajiwa kuwa Rais 2015?

Niseme, kwa watanzania walio wengi hawakutarajia Dr. Magufuli kuwa Rais wa Tanzania kwa kipindi hiki pamoja na kwamba alikuwa anang’ara na kumeremeta kati ya viongozi wote wa serikali kwa utendaji wake bora.Kwa nini basi asitarajiwe? Yapo mazingira yaliyokuwa yamemzunguka Magufuli kiasi kwamba kwa hali ya kawaida hakuna ambaye angeamini kwamba katika hali hiyo Magufuli angepenya mpaka aingie mbingu ya Tanzania. Mimi toka mwanzo niliamini kuwa atakuwa Raisi kwa sababu nitakazozionyesha baadaye.

Wachunguzi wa mambo ya siasa na mwenendo wa siasa katika Afrika walijenga hoja kadhaa ambazo zingemnyima Dr. Magufuli nafasi ya kuwa Rais. Baadhi ya hoja hizo ni kama zifuatazo:-

Kwanza, Magufuli alikuwa mwana-CCM na CCM ilikuwa na wazee wenye chama ambao walidai nchi hii wameitoa mbali na wasingependa kuona nchi hii inaendeshwa wasivyozoea na Magufuli alikuwa amethibitisha kwamba asingefuata mtindo wa uongozi uliozoeleka (mfano: Mzee Kingunge Ngombare Mwiru alidhihirisha hili kwa kujitoa CCM waziwazi).

Pili, Chama cha CCM kilikuwa tayari kimegawanyika katika mitandao mbalimbali na mikubwa ikiwa kati ya Edward Lowasa na Benard Membe ambaye hata Rais wa awamu ya nne aliegemea kwake( Membe). Hivyo walidai kwamba kwa kuwa Dr. Magufuli alikuwa hana mtandao wowote asingeweza kupenya katika vikao vya juu vya CCM.

Tatu, katika mfumo wa ufisadi uliokithiri ndani ya serikali na kwenye chama chake, Dr. Magufuli alionekana peke yake amevaa suti nyeupe wakati wengine wote walionekana wamevaa suti nyeusi ambazo ndani yake mifuko yote ilisheheni kila aina ya ufisadi na rushwa.Hivyo Dr. Magufuli alionekana waziwazi kuwa sio mwenzao au mtoto wa kambo asiyestahili kurithi kiti cha enzi bali mtu wa kutumiwa iliposhindikana kwa wengine kwani Magufuli aliishi kwa imani ya kutoshindwa na kwa nguvu zake.

Nne, Usafi na ubora wa utendaji kazi wa Dr. Magufuli ambao ulimfanya ahifadhiwe ndani ya mioyo ya Watanzania wanyonge na kumwombea dua na sala usiku na mchana kuliwashtua viongozi mbalimbali serikalini na kwenye chama chake kiasi kwamba walianza kujiandaa kukabiliana na umaarufu wake.Mfano wa Waziri Mkuu Pinda wakati akitoa hotuba Chato kuhusu bomoabomoa ya Magufuli ni kitu kinachotokana na hofu hiyo ya utendaji bora wa Magufuli.

Tano, ndani ya CCM na serikalini alionekana kuwa na msimamo mkali na usiobadilika kirahisi, hivyo alionekana kuwa mtu asiyepenyeka kirahisi na mtu asiyestahili kukabidhiwa dola.

Sita, CCM ilikuwa imepoteza kabisa imani kwa watanzania kiasi kwamba watu waliamini hakuna kizuri kinachoweza kuzaliwa na CCM licha ya juhudi kubwa sana iliyofanywa na katibu mkuu Kinana na katibu mwenezi wakati huo Nape kupitia matawi yote ya CCM kufufua chama. Hivyo, bado watu waliamini Magufuli angedhibitiwa na mfumo wa chama na kupoteza malengo yake mazuri.

Saba, wengine walidai kwamba Dr. Magufuli hakuwa ameandaliwa kidiplomasia kwa kushika Wizara ya mambo ya nchi za nje kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake Mkapa, Kikwete na Benard Membe aliyekuwa anaandaliwa.

Nane,kama ingetokea Dr. Magufuli angefanikiwa kuwa Rais,angeyumba mwanzoni kwa sababu mafisadi na wafanya biashara wangeficha fedha nje kwa kuhofia usalama wa fedha zao na kukwepa kodi halali ambayo wangepaswa kulipa.

Tisa, mataifa ya kibepari ambao walizoea kuchuma raslimali za nchi bila kuulizwa wangesita kuwekeza nchini kwa kukumbuka Azimio la Arusha la Nyerere.

Kwa nini niliamini Magufuli angekuwa Rais wa Tanzania 2015?

Mimi sikushawishika na hoja hizo na ndio maana nikatoa hotuba hiyo mwaka 2013 kabla ya uchaguzi ili zipimwe na ndivyo ilivyokuwa. Hoja zangu za kuamini kuwa Dr. Magufuli angekuwa Rais ni kama zifuatazo:-

Kwanza, Kwa wale ambao tumesoma upembuzi yakinifu wa maendeleo ya jamii (Historical and dialectical materialism), tunaamini kwamba katika muhula Fulani wa maisha ya jamii na kwa kutegemea hali halisi (CONCRETE MATERIAL CONDITION), jamii hulazimika kuwa na mfumo Fulani wa maisha ambao huzaa uongozi unaoendana na kipindi hicho ili jamii iweze kuendelea kuwepo kwa sababu uongozi ni zao la jamii na huakisi jamii husika (leadership is the product of the society). Hatua ambayo tulikuwa tumefikia ndani ya mfumo wa ufisadi na rushwa jamii ilisubiri ama kuangamia kwa uasi wa raia (Civil disobedience) au kuzaa aina ya uongozi ambao ungeliponya taifa. Na aina hiyo ya uongozi (kwa Watanzania ambao walikuwa tayari wameshika uongozi serikalini na kwenye chama tawala) ulionekana ndani ya Dr. Magufuli tu na hii nasema bila kujali yeyote atakayesema vinginevyo.Mtu yeyote ana haki ya kupinga lakini kwangu mimi niliyeteseka chini ya mifumo iliyopita ndio wakati wangu kupumzika chini ya rais wangu mzalendo.

Pili, Kwa watanzania wanyonge ambao walikuwa wamepoteza matumaini yao na ambao Frantz Fanon angewaita ‘’Viumbe wa ulimwengu waliolaaniwa’’ (The Wretched of the earth) walikuwa wakiinua sauti zao mbele za Mungu Misikitini, Makanisani, na hata kwa miungu ya babu zao kuliponya taifa hili. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu!

Tatu, nilikuwa nimepata unabii wa Kibiblia (Biblical prophecy) ambao ulinifanya niendelee kushikilia msimamo huo wa Magufuli kuwa Rais wa nchi yetu hata ilipokuwa sababu nilizozitoa zilionekana hazina maana kwa wale waliokuwa wakipotea wakati huo. Mifano ifuatayo itasaidia kuelewa vizuri:

Mfano wa I. Kwa wale wanaosoma Biblia wanaelewa habari za Daudi mfalme wa Israel wakati huo. Mfalme Saul alipomkosea Mungu, Mungu alimtuma Samweli (Nabii wa Mungu) kwenye nyumba ya mtu mmoja aliyeitwa Yese ili ajitwalie mfalme katika wana wa Yese. Yese alikuwa na wana saba halali na Daudi ambaye inasemekana alizaliwa nje ya ndoa na mmoja wa masuria wa Yese. Yese alipitisha wana wake wote saba mbele za Samweli lakini Mungu akawakataa. Na Mungu akamwambia Samweli kwamba yeye hatazami kama wanadamu, kwani wanadamau hutazama sura lakini yeye hutazama moyo. Samweli akauliza: je yupo mwingine aliyebaki?. Yese akasema: Ndio, yupo mdogo wao anachunga kondoo. Samweli akasema: mlete. Alipoletwa Biblia inasema alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri na umbo la kupendeza (Isam 16:12). Huyu Daudi ndiye aliyemuua Goliathi Jemadari wa majeshi ya wafilisti aliyeogopwa na waisraeli na mfalme wao Sauli. Ukisoma zaidi utagundua jinsi Daudi alivyopata vikwazo kutoka kwa ndugu yake Eliabu na mfalme Sauli kumkatisha tamaa ingawa baadaye aliwaletea ushindi na wakamshangilia.Kuna mambo kadhaa ya kufanana hapa kati ya Daudi alivyoingia katika Ufalme na jinsi Dr. Magufuli alivyoupata urais wa Tanzania.

Kwanza, Mungu alikuwa ameukataa ufalme wa Sauli kwa sababu ya uovu wake. Mungu pia alikuwa ameukataa uongozi wa kifisadi Tanzania uliokuwa unanuka mbele yake. Hivyo, alitafuta mfalme mwingine ambaye aliupendeza moyo wake.Dr Magufuli alikuja kama mtoto wa kambo wa CCM.

Pili, Mungu alimtuma Samweli kwa Yese akatafute mfalme miongoni mwa wana wake. Yese aliwasilisha watoto wake aliowapenda na kumwacha Daudi kando mpaka Samweli alipouliza kama kuna mwingine. CCM (Yese) iliwasilisha wana wake mbele za Kikwete na vikao vyake Mungu akawakataa ndipo wazee wa maadili wakasema kuna Dr. Magufuli anahangaika na madaraja huko porini, aitwe!.

Tatu, Daudi alipofikishwa mbele za Samweli alikuwa anapendeza kwa sababu hakuwa na uchafu. Dr. Magufuli alipofikishwa mbele ya Kikwete alionekana ni bidhaa safi ya kuweza kunadiwa sokoni bila mashaka.

Nne, Daudi alipotiwa mafuta, maadui wa kwanza kupambana naye alikuwa ndugu zake. Dr. Magufuli baada ya kutawazwa maadui wa kwanza kupambana nao walikuwa ndugu zake waliokuwa naye serikalini na kwenye CCM ambao wanamwona kama tishio kwao.

Tano, Daudi alikutana na kikwazo cha Sauli kumtaka avae silaha zake za vita.Daudi akataa, akatafuta silaha zake ambazo alizitumia kumuua Goliathi. Dr. Magufuli alipoingia madarakani alishawishiwa kutumia mtindo wa uongozi uliozoeleka wa kulindana, akakataa na kuchagua silaha yake ya kupambana na Goliathi wa Tanzania (Ufisadi) yaani kutumbua majipu.

Sita, Daudi alimpiga Goliathi akaanguka chini, akapanda juu yake na kukata kichwa wakati huo wana wa Israeli walikuwa wanaangalia.Walipomwona amebeba kichwa kwenyebakuli, walianza kushangilia. Dr. Magufuli kadiri anavyopambana na ufisadi bado Watanzania wanaangalia wakisubiri akifanikiwa washangilie. Mimi ninapenda tuungane naye moja kwa moja kumwangamiza Goliathi wa ufisadi na rushwa kila kona.

Saba, pamoja na ukweli kwamba Sauli na majeshi yake walikuwa wameshindwa na Goliathi lakini ndivyo walivyozidi kumchukia Daudi alipoonekana kuwa atakuwa mfalme bora. Lakini, kwa uwezo wa Mungu Daudi alivuka vikwazo mpaka alienda kaburini akiwa mwingi wa siku (mzee). Naye Dr. Magufuli, kadiri anavyozidi kufaulu ndivyo viongozi waliokuwa wameshindwa wanavyozidi kumchukia. Mimi ninaamini Mungu yuko pamoja na Dr.Magufuli atamshindia dhidi ya maadui wake kwa faida ya watanzania wote.

Mfano wa 2.

Daudi alipozeeka alikuwa na watoto ambao kulingana na kanuni za ufalme wa Israeli wangemrithi Daudi. Absalom alikuwa na haki ya kwanza ya urithi lakini kwa sababu ya uchu wa madaraka alijaribu kumpindua Baba yake Daudi, alijitangazia madaraka na wengi wakamfuata lakini Mungu akawakataa.Adonija naye akajaribu kujitangaza mrithi wa Daudi lakini haikuwezekana.Mungu kupitia kwa Daudi akamchagua Sulemani na kumsimika kuwa mfalme wa Israel. Sulemani katika hali ya kawaida asingekuwa mfalme kwa sababu alitokana na Bethsheba mwanamke ambaye Daudi alimuua mmewe Uzia, akamtwaa awe mkewe. Wapo waliojitangazia urithi wa kiti cha urais kwa nguvu wakisaidiwa na nabii nyingi za uongo kutoka kila kona lakini Mungu hakua nao akamchagua Dr. Magufuli ambaye hakufikiriwa kama tulivyoona hapo mwanzo.

Mfano wa 3.

Wayahudi waliokuwa utumwani walipokaribia kuuwawa, Mungu alimwinua Esta akaingia Ikulu kinyume na taratibu na kupitia kwa Esta wayahudi wakaokolewa. Hili linaweza kuwa jibu kwa wale waliodai kuwa taratibu za vikao ndani ya chama cha CCM hazikufuatwa kama mzee Kingunge Ngombare Mwiru alivyodai kuhusu Magufuli. Mungu hana njia moja ya kumwinua mtu. Biblia inasema Mungu humwinua mtu kutoka mavumbini na kumketisha pamoja na wafalme. Matendo ya Magufuli yalikuwa yametangulia mbinguni na Mungu akayapeleka Ikulu na Magufuli akapelekwa hazina yake ilipokuwa

Mfano wa 4

Waisraeli walipokuwa wameteseka sana Misri na kilio chao kikamfikia Mungu alimwita Musa kutoka machungani ambaye alikuwa nje ya Misri lakini mwebrania mwenzao akaenda kuwakomboa wana wa Israel. Musa alionekana ndiye Mungu alimwandaa kwa kazi hiyo.Kadhalika Mungu aliposikia kilio cha watanzania wengi alimwinua Dr. Magufuli aliyekuwa nje ya mfumo wa ufisadi aje awakomboe watanzania. Wapo watu waliomnung’unikia Musa jangwani wakikumbuka matango na makaburi ya Misri wakaangamia na ndivyo watanzania wengine wanavyomnung’unkia Dr.Magufuli wakikumbuka mfumo uliooza na kunuka.

Mfano wa 5.

Yesu alipokuja kama Masihi, wana wa Israel hawakumtarajia aje vile walivyofikiri. Walitegemea angekuja kwa utukufu na utawala wa kutisha awakomboe waisraeli kwenye utawala wa warumi wakati huo. Lakini wakakuta Yesu anakuja kuwaosha wanafunzi wake miguu, anakula na wenye dhambi na kutangaza kuwa hakuja kwa wenye afya bali wasiokuwa na afya. Maana wenye afya hawahitaji tabibu ndivyo Watanzania walivyotegemea kuona Magufuli akiingia kama waliotangulia wanakuja kugundua kwamba amekuja kwa wenye shida na sio wenye neema. Tungeweza kutangaza sasa Watanzania wote bebeni mizigo yenu mliolemewa nenda kwa Magufuli mpate pumziko. Tushirikiane kufunua uovu huu na kila mtu atimize wajibu wake.Wanaohoji namna Magufuli alivyoingia madarakani, mifano hiyo ya Kimungu inaonesha kwamba Mungu akimtaka mtu hawezi kuchaguliwa njia ya kumwita.

Sababu ya nne, kwa nini niliamini Dr. Magufuli angekuwa Rais ni kwamba nilimpima katika kanuni za sayansi za Isaac Newton.Katika safari nyingine, naomba tusafiri na mheshimiwa Magufuli tukimtazama kwa jicho la Isaac Newton na kanuni zake za mwendo na mjongeo (laws of motion). Newton katika kuchunguza kanuni za mwendo na mjongeo wa vitu aliandika kanuni tatu zinazotawala mwendo na mwenendo wa vitu. Naomba wasomaji wangu waniruhusu tumtembeze Dr. Magufuli katika kanuni hizi ili tumpime kama mambo anayofanya au vikwazo anavyokutana navyo vinathibitishwa na kanuni hizi.

Je Dr. Magufuli anapimika katika kanuni za mwendo na mjongeo za Isaac Newton?

1. Kanuni ya kwanza ya Newton, inasema kwamba kitu chochote hubaki katika hali ya utulivu (at rest) au huendelea katika mstari uliyonyooka bila kikomo mpaka nguvu (force) Fulani kutoka nje itumike kubadili hali ambayo kitu hicho kinayo. (Every body remains in its state of rest or uniform motion in a straingt line, unless an external force is applied to make it act otherwise). Kulingana na kanuni hii ufisadi katika Tanzania ungeendelea kujikita katika mawazo na vitendo vya watu au mafisadi wangeendelea na vitendo vya ufisadi na kukaa kimya juu ya matatizo ya watanzania bila kikomo mpaka nguvu kutoka nje itumike kubadili mwenendo na mwelekeo wa ufisadi huo. Hiyo nguvu kutoka nje ilikuwa awe Magufuli ambaye hakuwa ndani ya mfumo wa ufisadi. Kwa maelezo zaidi nitoe mfano wa gari. Watu wanapokuwa wanasafiri gari likakwama kwenye mchanga au tope watu hulazimika kushuka ili kulisukuma, hawawezi kulisukuma wakiwa ndani. Hii ina maana kuwa Tanzania ni gari lililozama kwenye tope la ufisadi, madawa ya kulevya, mikataba mibovu, mfumo mbovu wa elimu, rushwa, ujambazi, ujangili, vurugu za vyama vya siasa na mangineyo. Tanzania haiwezi kutoka humo mpaka Watanzania wote waamue kuacha na kuchukia uchafu huo na kulisukuma gari ili liendelee mbele na safari. Tayari Magufuli ameshuka analisukuma gari, kinachotakiwa ni wasafiri wote tuungane naye ili kwa umoja wetu gari letu – Tanzania litoke humo lilimozama.

Pia tuelewe kuwa kulingana na kanuni hii ya kwanza ya Newton gari linapokuwa limesimama, dereva akaliondoa ghafla wasafiri waliomo ndani husituka na kuangukia nyuma. Kama lilikuwa kwenye mwendo likasimama ghafla watu waliomo huangukia mbele na kama ni kwenye kona wasafiri hulalia upande mmoja. Wasafiri baadaye humzoea dereva wao na mshituko hupungua kwa sababu huiandaa miili yao kila wanapotaka kuondoka au wanapotaka kusimama au kupita kwenye kona.Lakini watu wengine wanaoangalia huwa hawaoni athari zozote.

Komredi Magufuli ni dereva mwenye spidi kubwa. Hivyo anapokuta gari limesimama huliondoa ghafla (mfano: ujenzi wa makao makuu) na anapolikuta linaendelea vibaya hulisimamisha ghafla(mf. Madini) waliomo katika gari hilo ndio wanaoshituka ama kuangukia nyuma au mbele. Malalamiko yanayosikika yanatokana na wale waliomo ndani ya gari hilo. Watu wengine wasiokuwemo hawaoni lolote la kulalamikia kwa sababu hawamo ndani ya gari hilo la ufisadi. Wote wanaomlalamikia Komredi Magufuli bila kujali kama wako serikalini, mitaani, makanisani, Misikitini kwenye CCM au vyama vya upinzani wamo humo kwenye gari la ufisadi na kama si moja kwa moja watakuwa ni wanufaika wa mfumo ambao Magufuli anajaribu kuubomoa.Nitalizungumzia hili katika makala nyingine nitakapotoa makala juu ya “Magufuli na siasa za Tanzania”. Itoshe kusema kwamba kanuni hii imemthibtisha Magufuli kisayansi.

2.Kanuni ya pili ya Newton inadai kwamba kasi ya mabadiliko ya mwendo wa kitu chochote hutegemea nguvu iliyotumika na huelekea mahali nguvu hiyo inaelekea kwa kuvuta au kusukuma (The rate of change of momentum is directly proportional to the force applied and it takes place in the direction of the force). Kwa kanuni hii tunaweza kusema kwamba mwendo- kasi wa ufisadi uliokithiri katika nchi hii ulikuwa umewavuta Watanzania wengi kuelekea upande wake. Kuna Mafisadi ambao ni dhahiri na kuna mafisadi ambao si dhahiri ambao wanatamani kuwa mafisadi na wengine ambao wanaupenda ufisadi kwa sababu walikuwa wananufaika. Nguvu hiyo ya ufisadi ilikuwa imewasukumia wengine mbali, ikawatupa katika lindi la umasikini na bahari ya Sahau. Hawa ndio wale kwa maneno ya Frantz Fanon kama tulivyosema angewaita “viumbe wa ulimwengu waliolaaniwa (The wretched of the Earth). Komredi Magufuli anapoingia madarakani anaingia kupitia mlango huu wa walalahoi na kuungana nao kubadilisha mwelekeo wa lile kundi la mafisadi na kwa nguvu za pamoja za Watanzania wote wanyonge wabadilishe mwendo – kasi wa nchi kuelekea kwenye maendeleo ya wote. Lakini kwa sababu kundi hili ni la muda mrefu, limejiimarisha na lina mtandao mkubwa ili komredi Magufuli apate nguvu zaidi za kulishinda kwa haraka ninamshauri afanye yafuatayo:-

· Uchunguzi wa KINA ufanywe wa kuwatambua mafisadi na waovu wote bila kumwonea mtu pamoja na mitandao yao na kuiweka wazi kwa Watanzania wote wanapodhihirika. Kwani mwovu ukimtambua nguvu zake huwa zimekwisha.

· Mafisadi watakaothibitishwa washughulikiwe na kupewa adhabu kali kwa kutumia mkondo wa sheria. Tunaamini mahakama ya mafisadi haitafanya mchezo katika jambo hili.Tunawaomba waweke uzalendo wa Tanzania mbele.

· Itabidi komredi Magufuli aandae mpango- mkakati wa elimu kwa jamii ili Watanzania wengi tusiojua ufisadi ni nini tuelewe maana ya ufisadi, mbinu zinazotumika, athari zake na namna ya kupiga vita ufisadi. Yaani kuwe na kampeni nchi nzima dhidi ya ufisadi. Ufisadi uonekane kama ni adui aliyetuingilia na anayeweza kumjeruhi yeyote asiyepambana naye. Hii itafanya watu wasishiriki katika mkondo wa ufisadi na wauchukie ufisadi.

· Komredi Magufuli aandae sera ambayo itamnyima fursa mtu yeyote kuwa fisadi au kula rushwa au hata kutamani kushiriki katika ufisadi.

· Kuweka mazingira ya amani ili watu washiriki katika kujenga uchumi wao kwa kudhibiti kwa nguvu zote kila aina ya kikwazo kinachojitokeza.

· Kuwapa semina- elekezi wateule wake wote na wafanyakazi wa ngazi za juu serikalini waelewe ni nini Tanzania inataka ifanyiwe na watumishi hao wa umma. Badala ya kuvizia Rais akitumbua jipu na wao wanavizia waliochini yao wanatumbua. Kila msaidizi wake awe mbunifu mahali pake pa kazi.

· Watanzania wote kwa pamoja tuamue kwamba yeyote, bila kujali yuko chama au taasisi ipi, atakayekuwa kinyume na vita dhidi ya ufisadi ahesabike kuwa ni adui wa jamii nzima ashughulikiwe bila huruma.

· Komredi Magufuli aandae mazingira ambayo yatawafanya wanyonge ambao ndio wanamuunga mkono mitaani waanze kuona unafuu katika maisha yao binafisi ya kila siku kwani upotoshwaji mkubwa wa vita hii hufanyika kupitia shida walizo nazo walalahoi.

Ninaamini kwamba komredi Magufuli akizingatia ushauri huu utamwongezea nguvu za kuvuta ule upande mwingine kuelekea upande ambao Watanzania tunataka kwa ajili ya maendeleo yetu.Hii ni kwa sababu atakuwa na jeshi kubwa la watu waelewa wanaomuunga mkono katika vita hii na yeye atatumia nguvu kidogo kuliko ilivyo sasa. Kanuni hii itathibitishwa pale tu nguvu zitaongezeka kwa upande wa komredi Magufuli.

3.Kanuni ya tatu ya Newton inadai kwamba kwa kila kitendo kuna nguvu- kinzani ambayo ni sawa na kitendo kinachofanyika. (To every action there is an equal but opposite reaction).

Kanuni hii hutufundisha kwamba viumbe vyote kwa asili yake, akiwemo binadamu, hutaka kubaki katika hali hiyo vilivyomo na hutoa nguvu za ukinzani mkubwa yanapojitokeza mabadiliko yoyote. Binadamu,kwa asili yake, hapendi mabadiliko (man is conservative) na hasa yale yanayokuja ghafla. Hii ina maana kwamba kama ulikuwa umezoea mtindo wa ufisadi na rushwa huwezi ukakubali kutoka humo na utatoa nguvu kinzani (reaction) dhidi ya mabadiliko hayo. Kanuni hii inatuonesha kuwa upinzani ambao komredi Magufuli anakabiliana nao unatokana na watu kutotaka kugeuka kutoka ufisadi na kuingia kwenye maendeleo ya wote. Jambo moja ninaloliona hapa ni kwamba kitendo cha komredi Magufuli kushughulikia ufisadi na rushwa kimedhihirisha mambo kadhaa.

· Kwamba ufisadi ulikuwa umejikita sana nchini kiasi kwamba hakuna mtu ambaye angezaliwa na mfumo wa ufisadi halafu ukaushambulia kama anavyofanya komredi Magufuli. Yaani hakuna ambaye angemkumbuka mnyonge!

· Watanzania walio wengi walikuwa hawajui kiwango cha ufisadi kilichokuwa kimefikiwa, mianya yake na athari zilizokuwa zimesababishwa na ufisadi.

· Kwamba vita dhidi ya ufisadi inayoendeshwa na komredi Magufuli imebainisha wazi ni nani aliyekuwa hapendi ufisadi na rushwa kwa dhati na nani ambaye alikuwa anazungumzia ufisadi kwa unafiki. Watu wote waliokuwa wamechoshwa na ufisadi wameungana na Magufuli kupambana na ufisadi.Mfano vyama vyote vya siasa vya upinzani ambao wanaunga mkono juhudi za komredi Magufuli katika vita hii. Hii ndiyo inayowadhirishia Watanzania kwamba kumbe walipokuwa wanapiga kelele kuhusu ufisadi walikuwa wanamaanisha kwa dhati ya mioyo yao yote kwamba walikuwa na ajenda.

· Kwamba ufisadi na rushwa ndivyo vilikuwa ajenda ya kitaifa na ili uendelee kubaki katika ulingo wa siasa ni lazima uunge mkono kupiga vita ufisadi au ukae kimya vinginevyo ni kujiabisha mbele ya watanzania wote. Hatutegemei mtanzania mwenye akili timamu na mwenye mapenzi na nchi hii kwamba anaweza kuthubutu kupingana na juhudi zinazofanywa na komredi magufuli.

Mimi si mnafiki, ukiacha Nyerere ambaye alikuwa ni mpendwa na rafiki ya kila Mtanzania, mimi mpaka sasa tangu nimezaliwa nimekuwa rafiki wa watu wanne tu ambao wamewahi kuwa wanasiasa katika nchi hii. Hao marafiki zangu hawakuwahi kujua kwamba mimi ni rafiki yao ila mimi ninajua kwamba ni rafiki zangu.Hii ni kwa sababu urafiki wangu hautokani na maslahi yoyote bali msimamo na imani yangu ya kuchukia uovu sehemu zote nilizosoma na nilizoishi. Nilikuwa rafiki mkubwa wa Edward Moringe Sokoine na nilishangilia sana wakati wa kukamatwa wahujumu uchumi. Nikamuunga mkono kwa kufichua ufisadi shuleni Sengerema kwa mgomo mkubwa sana(1982) na chuo cha ualimu Korogwe(1986) na mabadiliko makubwa yakafanyika ya uongozi. Mungu akamtwaa akaniacha yatima! Nikaanza urafiki na Mrema akiwa serikalini kwa mpango wake wa siku saba kuondoa uzembe kazini na ufisadi uliokuwa unajitokeza wakati huo akiwa waziri wa mambo ya ndani.Tunakumbuka kashifa ya dhahabu uwanja wa ndege wa Dar es salaam.Nikamuunga mkono kwa kuibua ufisadi UDSM nikiwa rais wa kwanza wa DARUSO(1989-1990). Matokeo yake, yalikuwa kuwajibishwa kwa uongozi wa juu wote wa chuo (1990) Yaliyomkuta ninampa pole lakini nimpongeze kwa kukumbukwa na komredi mwenzetu. Dr.Magufuli naomba uitumie hazina hiyo ya Mrema ambayo ilikuwa ipotee kwa kusahauliwa na mfumo wa kifisadi na wewe Mrema mwachie komredi Magufuli mawazo na uzoefu wako afanyie kazi utakuwa umetimiza mapenzi yako kwa taifa lako ukiwa na haraka kwa Dr. Magufuli mtagongana muda si mrefu. Nimekuwa rafiki wa Dr. Slaa kwa uzalendo wake wa kuibua kashifa kubwa za ufisadi katika nchi hii zilizosababisha wananchi kujua kinachoendelea katika nchi. Ninampenda sana msomi Yule kwa sababu hana unafiki ndio maana kukosekana kwake kwenye upinzani na ajenda ya kuwambia wanancha imekosekana kwenye upinzani. Ninasema bila unafiki wowote na bila kuogopa, kwamba Dr. Slaa kama angepata fursa kwenye serikali ya Magufuli angekuwa ni jembe la kutifua vumbi maana ni mtu anayefanya kazi kwa utafiti na vielelezo kama Dr. Magufuli mwenyewe.Kwa kuwa alishasema ana imani na Dr. Magufuli ataufungua moyo wake kutimiza kile alichokusudia katika maisha yake yote ya mapambano. Nina hakika Magufuli hawezi kujuta hata siku moja kwa ushauri huu. Halafu rafiki yangu mwingine wa sasa ni komredi Magufuli.Sijapata rafiki mwingine. Urafiki wangu hutanguliwa na mtu kuchukia uovu kwa dhati kama mimi, si lazima tuonane uso kwa uso lakini matendo mema ya mtu hutangulia sura yake kutengeneza njia kwangu. Nimalize kwa kuwaomba watanzania wenye nia na nchi yetu tuwe na mjadala wa kitaifa wa namna tutakavyoijenga Tanzania mpya badala ya kulaumu tu.

JOSEPH MATIKO MATARE

SLP 1284

SONGEA

jmmatare@yahoo.com

0757282151
 
Ndugu yangu Matiko Matare
Nimekusoma. Nakuombea Mungu/Allah akujalie uvumilivu utakapolazimika kujutia maneno haya uliyoyaandika. Huo mchanyato wa Sokoine/Mrema/ Slaa/ Magufuli/Matare ni wa kusadikika.
Nakushukuru kwa kumuondoa JKN katika mchanyato huo.
 
Asante sana Yosefu kwa makala yako fupi, imemfikia na zamu yako kukumbukwa, imekaribia, na kushauri jiunge na chama ndipo uwe na uwezekano wa kusaidiwa.
Pasco
 
Jamani jamani , nikiri sijaisoma yote nimeiprint na nitakwenda somea nyumbani! Kitu tu kimoja niseme. Wote uliowataja marafiki zako nami ni marafiki zangu. Si kwa kufaidika bali kwa faida ya watanzania wote. Labda mmoja tu hukumtaja nae nadhani kosa moja tu basi limefunika uzuri wake woote. Aliinua heshima ya Serekali. Bdio aliyethubutu kuhakikisha miundo mbinu inajengwa nchi nzima. Ofisi za serekali ziliboreshwa. Learning environment ya wanafunzi iliboreshwa kwa kiasi chake. Mengi baada ya kusoma uloandika!
Ndio maana Ml. Nyerere alisema watu wenye uzalendo bado wapo. Naam bado wapo!
 
Tuwekee na hiyo clip Mkuu! Sio kwa ajili ya kihakikisha bali kufurahia tu. Na amini nakuambia kuna waliomtaka jpm LAKINI WALIKATISHWA TAMAA NA MCHAKATO WA KUMTATA RAIS. lakini Mungu akafanikisha kwa hali ilivyokuwa!
 
Ndio maana si rahisi kwa JF kupata misukosuko kwasababu watu wa mh.huitumia pia kupost habari za mfalme.
 
UMELANIWA UNATAFUTA UDC AU HAKUTEUWI SAHAU
 
mkuu Pasco sikutarajia ungechangia hivi...wakipinga mnawaita wapinga maendeleo wakisifu mnawaita wanataka cheo..
 
Ndio maana si rahisi kwa JF kupata misukosuko kwasababu watu wa mh.huitumia pia kupost habari za mfalme.
Kwa hiyo ulitaka JF iwe mali ya CHADEMA pekee? Mkiweza hivyo kabla ya 2010. Baada ya hapo wazee wa kazi tumeingia na sasa mwendo mdundo
 
mkuu Pasco sikutarajia ungechangia hivi...wakipinga mnawaita wapinga maendeleo wakisifu mnawaita wanataka cheo..
Mkuu Ikoa, tufike mahali wote humu tuwe na uwezo wa kuchambua threads za kusifu au kumpongeza Magufuli kwa kazi nzuri anayolifanyia taifa letu ambazo ni bonafide genuine za kupongeza tuu kwa maana ya kupongeza na zile za kupongeza ili kujikombakomba mtu ujitambulishe upo na umepongeza ili ukumbukwe.

Kwenye maandishi kuna kitu kinaitwa "graphology", ukijaaliwa kuisoma hiyo graphology na kuielewa, ukisoma tuu bandiko, unabaini the motive behind! .

Mfano mabandiko yangu ya kumsifu Magufuli, yoyote atakayedhania nasifu kutafuta UDC au u DED huyo ni kichaa!.
Pasco
 
MATIKO HUJAMBO NADHANI HUMJUI VIZURI HUYO UNAYE MSIFIA PIA HAO WENGINE MARAFIKI ZAKO BADO WANA MAPUNGUFU MAKUBWA SANA YA KIUONGOZI, NA KAMA UNAPENDA WATU WA AINA HIYO UJUE WANAWEZA WAKAIHARIBU SANA NCHI,

HEBU FIKIRIA LEO VYUO VIKUU WAMEZUIWA KUFANYA MIDAHALO NA MAKONGAMANO MPAKA KIBALI CHA POLISI?
KUMBUKA ULIVYOKUA NA UHURU PALE DARUSO JINSI MLIVYOKUA HURU KUJADILI MPAKA MKAFUKUZWA LAKINI SASA HAKUNA.

WEWE ULISEMA NI MLOKOLE HEBU OMBA MUNGU AKUFUNULIE AKUONYESHE

GAMBA
 
Asante sana Yosefu kwa makala yako fupi, imemfikia na zamu yako kukumbukwa, imekaribia, na kushauri jiunge na chama ndipo uwe na uwezekano wa kusaidiwa.
Pasco
Kwani wewe Pasco unapoandika hapa makala za kumsifu Rais Magufuli huwa unafanya hivyo ili Rais Magufuli akukumbuke? Sikufahamu kama huwa unafanya hivyo ili ukumbukwe!

Kwa nini wengine wakiandika mnadhani wanatafuta kukumbukwa lakini ninyi mkiandika mnadhani tofauti?

Kama katika mada zako huwa hutafuti kukumbukwa, kwa nini unadhani huyu mwandishi anatafuta kukumbukwa? Ninafahamu utanioambia nisome kati ya mistari lakini huo ni mtazamo tu ambao utaendelea kuwa hauna ukweli mpaka mwandishi aseme anatafutwa kukumbukwa.

Tuepuke kutoa hukumu kwa masuala ambayo hatuna ushahidi halisi.
 
Back
Top Bottom