Rais Magufuli: Majizi yamehamia CHADEMA

Rais Magufuli: Majizi yamehamia CHADEMA

Na wauaji wametokea chato (so long anao ushahidi kuwa ni majizi kwa nini asiyahukumu?
 
Chadema ni kichaka kipya cha mafisadi; Siasa za nchii ni za aina yake; Iba; Kimbilia Chadema watakuficha ipasavyo, kwa jasho na damu.
Japokua mahakama, polisi, na mamlaka wanazo CCM
 
Hivi Magufuli anapowataja majizi, yeye anajiweka upande gani? Kweli nyani haoni kundule...yaani mtu aliyekuwa bega kwa bega na majizi kwa miaka zaidi ya ishirini akiishi nao nyumba moja, kulala, kujifunika blanketi moja, kuamka nao, kukaa nao, kujadili, kutoa maamuzi na kuyatekeleza kwa pamoja kwa miaka yote hiyo, anapata wapi ujeuri wa kujitenga nao hivi sasa wakati nyumba bado ni ile ile, kitanda kile kile, ukumbi ule ule...! Halafu wajinga wapo wanaomwamini na kumpigia vigelegele!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.

“Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele” alisisitiza Rais Magufuli

======

My Take:ama wanaiba,wanaachwa ndani ya chama wanabembelezwa na unyweshwa uji wa ulez ama kina tibaijuka,kin angereja
Eti sasa anasema majizi yame hamia CHADEMA!!!!! Aibu kubwa hii....

Hivi Magufuli anatuchukuliaje Watanzania?

Yaani mko na mafisadi na bado mkasema mahakama ya mafisadi imekosa kesi? Aibu kubwa hii.

Nyie endelezi kasi ya chuki na dhuluma by the time mnaamka usingizini mmebak wawili.

Mwanacha ccm anaachwa aibe,anabembelezwa ,anafichwa ndani ya begi ili wengine wasijue.Siku anaamua kutoa kichwa mwenye begi anasema kwanza kakimbia na nyama mara hili mara lile.Kinachonishangaza na ambacho wanajf tujadiliane kwa nini ccm haiwafukuzi inaowaita mafisadi?,inasubiri wakitangaza kukiacha chama ndipo midomo iliyojaa ghiriba inaanza kusema?

chama kina dola kina kila aina ya msaada kuwabaini na kuwashughulika wezi kwa nn kinasubiri watoke ndipo kiseme?,je,ninani aliwahi kufikishwa mahakamani tangu wataje kuwa waliohama nimafisadi?,Yupo Lowassa hadi leo hana kesi ya kujibu,lakini tuliambiwa fisadi,Nikionacho wanajf,ccm inamsakama Nyarandu maana nijembe tegemewa ndani ya ccm,nikijana ana future kubewa,singida anapendwa na hofu yao ninyarandu kwenda kusaidia kulirudisha jimbo la singida ndani ya chadema na hivyo kuendelea kuibomoa ccm taratibu lakini kwa uhakika
 
Raisi wangu, wape chadema uhuru wa kukwea majukwaani waongee kama ccm inavyoongea ili tupime ukweli wa majizi yako ccm au chadema.
[emoji38] [emoji38] comment na username yako vimenifanya nicheke sana
 
MKapa,,Kikwete senior & jnr,Chenge,Tibajuka,Bashite aka Makonda,Kitwanga & Ligumi Co,Mwakyembe,Kinana n.k wahamie fasta Chadema chama cha mafisadi Papa wakaunge na fisada Lowassa sisi huku CCM raisi wangu Magufuli tumewachoka safisha usisubili wang'oke wenyewe.
 
pombe ametuita ..
*vilaza
*wapumbavu
*majizi
*wapiga dili
*mashetani
*mafisadi
Ivi pombe umsafi kiasi gani ?
*mtakatifu angeanza kurudisha amani kwenye familia yake na amuombe radhi mama yake
*mtakatifu arudishe nyumba walizouziana kishkaji bwerere hadi mpwa akapewa, bila kufata taratibu za mauzo
*mtakatifu arudishe zile bilioni 6.8 alizonunulia kivuko kibovu cha mwaka 1978
*mbona bashite katajirika ghafla ?
*mtakatifu mbona hukaguliwi ?
INTERAHAMWE WALIOKOSA RADHI ZA WAZAZI..
ushindi wenyewe ni asante mkapa na asante lubuva.
ukichaa ukipanda nyumba zinadondoshwa watu wanalala juu ya matofali.
Mwanangu uneandika vema sana
 
Nahisi sasa majizi yameisha ndani ya ccm yote yapo chadema?.. duuh lugha zingine yapaswa kufikiri na kuwa na hekima sana Ee mungu utunusuru
 
Mbona wanaotoka chadema kuingia ccm siyo wezi? Kwa hiyo ni chama gani chenye wezi wote Tanzania kama wote wanaotoka ccm ni wezi na wanaotoka chadema siyo wezi?
Akili ya mtu changanya na yako upate upate jibu.
 
Kwa hiyo ccm ni factory ya majizi kama hakuna hata moja atokaye chadema ni mwizi. Hongera sana chadema kwa huo unadhifu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.

“Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele” alisisitiza Rais Magufuli

======

My Take:
Eti sasa anasema majizi yame hamia CHADEMA!!!!! Aibu kubwa hii....

Hivi Magufuli anatuchukuliaje Watanzania?

Yaani mko na mafisadi na bado mkasema mahakama ya mafisadi imekosa kesi? Aibu kubwa hii.

Nyie endelezi kasi ya chuki na dhuluma by the time mnaamka usingizini mmebak wawili.

Hayo Majizi yanatokea wapi basi???
 
Kuna mwalimu wangu mmoja aliwahi kujinasibu mbele za watu kuwa yeye ni mtu safi sana hana mawaa wala dhambi. Lkn watu wengi ktk jamii yake qalikuwa wakushangazwa sana na yeye kuwa marafiki zake wengi wakikuwa ni waalifu, wezi, majambazi, walarushwa na riba pamoja na wazinifu. Sikumoja jamii yake ile ilimuuliza mbona wewe unajinasibu ni mtu safi lkn rafiki zako wengi ni waalifu? Yeye alijibu kwa upole : Mwenye afya haitaji tabibu bali walio wagonjwa hivyo yeye hasumbuki sana na watu wema bali waovu ili awarudishe ktk mstari na njia iliyosawa. Mwenye akili pevu ataelewa nini maana ya haya maneno, mwovu akijitambua makosa yake siku ukimkuta yuko msikitini au kanisani msimdhihaki bali apokelewe na kupewa support alikuwa amepotea sasa amerudi nyumbani na kutubu makosa yake. Inawezekana Nyalandu ni mwana mpotevu.....
 
Back
Top Bottom