Rassa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2013
- 332
- 295
Mzee Tupatupa,
Shida inaweza ikawa ni ileile ya Zaifu. Ni ukweli uliositirika kuwa fedha ya EPA ndiyo iliyotumika kumweka madarakani Zaifu. Hakuwa na ujasiri wa kuukata mkono uliomshikilia.
Halikadhalika kwa Mako-meo naye, si ajabu hizo kodi zilizoachiwa (hali tukijua serikali bado ni ya FISIEM) zilikuwa ndicho chanzo cha mapesa mengi yaliyotumika kwenye kampeni ya kumwingiza ikulu. Ingawa mwenyewe jana alidai kuwa hakuchukua mchango wowote kwa mfanyabiashara, lakini hiyo kauli inamhusu yeye kama Mako-meo. Kwa upande wa chama ambacho yeye alikuwa mgombea wake ni hadithi nyingine kabisa. Kwa mtaji huo jeuri ya kusimamia sheria ya kodi kwa wafanyabiashara ataipata wapi?
Sasa hivi amegusa upande mmoja tu wa shilingi. Waswahili wanasema "pesa matumizi". Kama ana uthubutu achungulie matumizi ya umma wakati wa kampeni. Akiwa mkweli, atapata kizunguzungu. Hiyo ndiyo fedha iliyompeleka ikulu. Iwe imetumika vizuri ama vinginevyo. Au alidhani kutamba kote kwa chama nchi nzima walikuwa wanatumia fedha kutoka wapi?
Ghafla atakuwa mpole!
Chagadema hawanaga jema,wenyewe kila jambo hulalama na mtabakia upinzani mpaka kiama cha chama chenu. Wananchi wameshtuka wanataka siasa za hoja/masuala na sio siasa za matukio na kupinga kila kitu.