Rais Magufuli, Kikwete na wafanyabiashara

Rais Magufuli, Kikwete na wafanyabiashara

Binafsi Magufuli nimemuona angalau kumbe ana busara kwa hili
huwezi anzisha vita na kila mtu kila upande
kuchagua nani wa kupigana nae na saa ngapi upigane nae ni busara

Wafanyabiashara wanakwepa kodi sababu kodi nayo ni kubwa saana

ipunguzwe ilipike kwa urahisi......hari unanunua Japan milioni moja tu
hadi ulitoe unalipa milioni saba...jumla milioni nane

busara zitumike kuondoa tatizo........
 
Wafanyabiashara hao wakubwa nchini walishusha pumzi na kushukuru kuepukwa na dhahama ya kisheria. Lakini, makontena husika yatajulikana yalikuwa na nini na hata kujua usahihi wa kodi ambayo wafanyabishara walikwepa?
Mkuu VUTA-NKUVUTE hoja yako ni nzito. Nilisoma gazeti moja juzi kuwa mmojawapo wa 'wapambe' kakimbilia Somaliland, sijui tunaweza kujiridhisha vipi juu ya mizigo iliyoingizwa. Siwezi kukubali kuwa siraha zote zinazosumbua DRC, Nigeria, Syria na kwingineko zilipitishwa na forodha za huko!
Wananchi wanazipenda nchi zao lakini walioaminiwa kuongoza ndio wanaleta matatizo yote haya.
 
Uchumi wa nchi yeyote inayoendelea unategemea sector binafsi kwa asilimia kubwa mno,
Alichokifanya Mh Rais ni kuweka mazingira rafiki na wafanyabiashara, kawaamuru wakalipe kodi walizokwepa, pia kawaomba wawekeze katika shughuri zote za kiuchumi ili kisudi Nchi iate mapato zaidi na Watanzania wapate Ajira,

Hawa wafanyabiashara usipoweka mazingira rafiki kwao kwa kweli nchi itayumba, kama walifanikiwa kukwepa kodi awamu iliyopita awamu hii watazilipa kwa wingi mno..

Rais Magufuli yupo sahihi
 
Mimi sioni tatizo. Wanalipa kodi waliyokwepa. Hajawasamehe. Ubaya uko wapi? Ukizingatia hii n serikali mpya lazima acompromise. Hajataka kuweka mpasuko na wafanyabiashara.

Kuwawajibisha watumishi na kuweka wapya n salam tosha kuwa hawatosaidia tena ukwepaji kodi. Tunaanza upya.



Hongera magufuli
Mkuu naunga mkono hoja. Katika conflict resolution kuna kitu inaitwa Amnesty..yaani unawapa waasi muda wa kukisalimisha ilinkujenga nchi na baada ya hapo atakayekaid ndo ametangaza vita rasmi.
Kwa maoni yangu njia hii ni muafaka kuliko kuendelea kutoa vitisho. Ila kinachotakiwa kufanyika ni kusimama kwenye kauli yake..baada ya siku saba na hakuna maelezo washughukikiwe.
Nna ili kutoa taswira nzuri..tuelezwe wafanyabiashara wangapi wali comply na kiasi gani kimekusanywa..isije ikawa ni kama yale ya EPA mpaka sasa haijulikani kilicholipwa.
 
Mzee Tupatupa,

Shida inaweza ikawa ni ileile ya Zaifu. Ni ukweli uliositirika kuwa fedha ya EPA ndiyo iliyotumika kumweka madarakani Zaifu. Hakuwa na ujasiri wa kuukata mkono uliomshikilia.

Halikadhalika kwa Mako-meo naye, si ajabu hizo kodi zilizoachiwa (hali tukijua serikali bado ni ya FISIEM) zilikuwa ndicho chanzo cha mapesa mengi yaliyotumika kwenye kampeni ya kumwingiza ikulu. Ingawa mwenyewe jana alidai kuwa hakuchukua mchango wowote kwa mfanyabiashara, lakini hiyo kauli inamhusu yeye kama Mako-meo. Kwa upande wa chama ambacho yeye alikuwa mgombea wake ni hadithi nyingine kabisa. Kwa mtaji huo jeuri ya kusimamia sheria ya kodi kwa wafanyabiashara ataipata wapi?

Sasa hivi amegusa upande mmoja tu wa shilingi. Waswahili wanasema "pesa matumizi". Kama ana uthubutu achungulie matumizi ya umma wakati wa kampeni. Akiwa mkweli, atapata kizunguzungu. Hiyo ndiyo fedha iliyompeleka ikulu. Iwe imetumika vizuri ama vinginevyo. Au alidhani kutamba kote kwa chama nchi nzima walikuwa wanatumia fedha kutoka wapi?

Ghafla atakuwa mpole!
 
Ni kweli kabisa kulipa kodi walizokwepa ni lazima, baada ya kulipa ilitakiwa wafunguliwe mashtakamashtaka sio kusamehe
 

Ulipotokea wizi wa mabilioni ya shilingi za kitanzania, yaliyochotwa isivyo halali BOT, Rais Mstaafu Kikwete aliwaamuru wafanyabiashara waliohusika 'kurudisha' fedha hizo. Ni kama Rais mstaafu aliwaambia wezi warudishe pesa walizoiba. Wananchi wakasema na kuhema hadi wakalala. Mambo yakapita. Hadi sasa, haijulikani kama zilirudishwa au la na kwa kiwango gani. Maisha yanasonga.

Jana, Rais Magufuli amewapa siku saba wafanyabiashara, waliohusika na kupitisha makontena yao Bandarini bila kulipa kodi, walipe kodi waliyokwepa. Wengi wetu tunajua kuwa kukwepa kodi ni kosa la jinai.

Wafanyabiashara hao wakubwa nchini walishusha pumzi na kushukuru kuepukwa na dhahama ya kisheria. Lakini, makontena husika yatajulikana yalikuwa na nini na hata kujua usahihi wa kodi ambayo wafanyabishara walikwepa?

Hakika, katika hili la wafanyabishara watenda jinai, Rais Magufuli amefanana na Rais Mstaafu Kikwete!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

CC Mzee Mwanakijiji.
Mdogo mdogo tutafika.Kuondoa mfumo uliooza ni kazi kweli kweli.Kama ulivyo sema Mzee Tupatupa kweli kuna la kujiuliza hiyo Kodi wanayotakiwa kulipa ni ipi?
Si tuliambiwa makontena zaidi ya 300 hayaonekani ?
Au yamepatikana na kama yamepatikana ndani yake kulikuwa na nini?
Je ni akina nani wenye hayo Makontena?

Bila mlolongo wa taarifa sahihi kama hivi;
Makontena mfano.200 ya Mr.X yaliyokuwa na ..... kodi dhamani.........
Mpaka tuone idadi kamili imetimia na hatua za kisheria imechukuliwa hata kama ni kwa kukubaliana nje ya mahakama sijui kama sheria zetu za Kodi inatoa mwanya huo au raisi kutumia mamlaka yake lakini kwa vyovyote Faini dhidi ya wahusika tena kubwa ni muhimu sana kinyume na hapo ni sanaa ile ile ya miaka nenda rudi.

MMM kwenye kijijarida hili usisahau kuliongeza.
 
Last edited by a moderator:
sisi tunataka kodi yetu tu na penalty zote watalipa ....

mzee tupatupa ngo`mbe wa lowassa wanaendelaje...?
 
Baba unavyo mdai MTU lazima utampa notice b4 akishindwa Na hapo ndo mengine hufata so Tusubiri n mapema sana kusema JPm ni km Mkwere

Hatujakopeshana,wametuibia!Mwizi adhabu yake ni kupewa muda arudishe?Hapa kafanana na mkwere,JPM umetuangusha katika hili
 
Kuongoza ni hekima, mbona Wafungwa wakisamehewa na Raisi hamshangai?

Sheria zipo, lakini kuongoza kunahitaji mambo yote yaani busara, hekima na sheria.

Wanaotaka Magufuli awashitaki watu hao ili " Waridhike", basi watu hao nao pia wawe tayari kuchunguzwa nyumba na mali zao wamezipataje, wachunguzwe kama wamezilipia kodi etc etc

Magufuli anaona mbali, unaweza fungua kesi ya madai ya bilioni moja kesi ikagalimu milioni 900 maana take umeokoa m1000 tu
 
Wale wafanyakazi wameajiliwa na wanalipwa na serikali na ndio maana wametolewa nduki,il wafanyabiashara huwezi kuwafunga,ila inabidi tu kulipa wanachodaiwa.harafu usimfananishe Mwizi mkwepa kodi

Kwa China huyu mkwepa kodi anaitwa "muhujumu uchumi"!Huyu anahali ngumu kuliko kibaka!
Suala hapa ni kuwa watu wataendelea kujaribu kukwepa kodi coz wakikamatwa wanapewa muda wa siku 7 warudishe!
 
Kwanini watu wanakwepa kodi? Kwanini kodi isababishe wafanyakazi wa TRA wajione miungu watu..na kujenga mazingiza ya rushwa? Uwazi katika kodi na kodi zinazolipika bila kinyongo ndio msingi wa kuondoa changamoto ya ukwepaji kodi.
 
Magufuli will never win the battle he has started to fight within his corruptive party unless and until he desert that syndicate.

Kama kweli ana nia thabiti ya kuokoa taifa hili linalodidimia kiuchumi na kimaadili ahimize bunge la katiba lipitishe katiba mpya kama ilivyopendekezwa na kamati ya Warioba; na kutoka hapo akishindwa itabidi 'atoroke aje' ili tupige tena kura. Atapata kura nyingi tu kupitia Ukawa.

 
Hatua ya Raisi kusema wakalipe Kodi bila kwanza makontena kupatikana na kujulikana kulikuwa na nini ndani yake-ni kumweka Raisi kwenye mitego mibovu kuliko kitu kingine-maana kesho waweza shangaa mmoja ya makontena yanayodaiwa kupotea kukakuta picha na video limepostiwa humu JF ndani yake likiwa na Sembe-mie nawaza tu!


[h=3]Ripoti UN: Tanzania kinara dawa za kulevya - Jamii Forums[/h]www.jamiiforums.com ? ... ? Jukwaa la Siasa


Translate this page
Sep 10, 2013 - 20 posts - ‎15 authors
 
Wasikuzoea. Wataingia mpaka jikoni. Kumbuka walivyomfanyA Mzee Mkapa
 
I mean it needs action, but also constrained by many other factors and sometimes they can't avoid discussing win-win scenarios. That's why at times we said mwenye bunduki illegal apeleke police mwenyewe in a certain grace period na hatutakuuluza. Beyond grace period ukikutwa nayo you are in trouble. Those are unavoidable, diplomatic leadership scenarios that sometimes can be best options.
 
Mimi sioni tatizo. Wanalipa kodi waliyokwepa. Hajawasamehe. Ubaya uko wapi? Ukizingatia hii n serikali mpya lazima acompromise. Hajataka kuweka mpasuko na wafanyabiashara.

Kuwawajibisha watumishi na kuweka wapya n salam tosha kuwa hawatosaidia tena ukwepaji kodi. Tunaanza upya.



Hongera magufuli

Hapana ndugu. Kosa likifanyika ni lazima mkosaji awajibike. Kwa hiyo wakwepa kodi ilifaa wapate penalties kwa kukaa na pesa za serikali. This is not serious. Tutaendelea kuwafuga hawa wezi mbaka lini???
 
"Mzee tupatupa" kama unavojiita, wakati mwingine huna fikra barabara! Hivi unawezaje kumlinganisha magufuli na kikwete wakati kwanza anachokifanya ni kuonesha uozo wa iliyokua serikali ya kikwete? Magufuli amekua mzalendo kwanza kwa kuibua uozo huo na pili kuomba walipe kodi walizokwepa huoni kama huyu mtu muungwana? Unamfananishaje na Kikwete aliesababisha upotevu mkubwa wa pesa za serikali na mtu ambaye ndo kwanza kaaanza kazi na inaonesha yuko serious na maendeleo ya watanzania?
Kama unavojiita "mzee wa lumumba" nadhani wewe ni kati ya wale CCM wanafiki ambao magufuli kaahidi kuwashughulikia ndani ya chama.
 
Mtamwelewa tu.....
Yupo sahihi na kama hamjui watu wamewekewa mitego kitakachofuata mtarudi hapa kuniambia

Wanaoshutumu naamini ni UKAWA tu, hawaji na mapendekezo. Wataisoma namba kama baadhi ya hao ni wafanya biashara. Kwa mfanya biashara aliyesikiliza hotuba yake kwa makini akalipe ushuru unaostahili mara moja.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Back
Top Bottom