Rais Magufuli, Kikwete na wafanyabiashara

Rais Magufuli, Kikwete na wafanyabiashara

Lazima uangalie nyakati, sikumbuki kwa JK ni muda gani alitoa agizo baada ya kuingia madarakani, JPM ndo kwanza ana mwezi, wafanyabiashara wakubwa ni watu wa muhimu sana, karata yake ya kwanza lazima aicheze vizuri na hawa watu. Kawapa grace period, na tuwe fair, JPM anachosema anamaanisha! Tusubiri hizo siku sita zilizobaki!

Tunaangalia umri wa serikali au tunaangalia sheria inasemaje?
 
Wewe mwenye akili huoni hii double standard ya wafanyakazi na wafanyabiashara?

Mzee Tupatupa

Baba unavyo mdai MTU lazima utampa notice b4 akishindwa Na hapo ndo mengine hufata so Tusubiri n mapema sana kusema JPm ni km Mkwere
 
Kuongoza ni hekima, mbona Wafungwa wakisamehewa na Raisi hamshangai?

Sheria zipo, lakini kuongoza kunahitaji mambo yote yaani busara, hekima na sheria.

Wanaotaka Magufuli awashitaki watu hao ili " Waridhike", basi watu hao nao pia wawe tayari kuchunguzwa nyumba na mali zao wamezipataje, wachunguzwe kama wamezilipia kodi etc etc

na si wafungwa wote husamehewa mdai,ila alokwepa kodi amefanya makosa na anapaswa kushtakiwa,unamsamehe ili iweje?
 
Msije mkanilisha maneno baadaye. Nasema hapa hapa mwanzoni, si Rais Magufuli wala Kikwete ambaye anawaogopa au aliwaogopa wafanyabiashara. Wafanyabiashara ni watu muhimu kwa uchumi wa kitaifa. Lakini, natumai wote mnajua kama nijuavyo mimi, Rais Magufuli naye ameshajifananisha na Kikwete katika mambo yawahusuyo wafanyabishara.

Ulipotokea wizi wa mabilioni ya shilingi za kitanzania, yaliyochotwa isivyo halali BOT, Rais Mstaafu Kikwete aliwaamuru wafanyabiashara waliohusika 'kurudisha' fedha hizo. Ni kama Rais mstaafu aliwaambia wezi warudishe pesa walizoiba. Wananchi wakasema na kuhema hadi wakalala. Mambo yakapita. Hadi sasa, haijulikani kama zilirudishwa au la na kwa kiwango gani. Maisha yanasonga.

Jana, Rais Magufuli amewapa siku saba wafanyabiashara, waliohusika na kupitisha makontena yao Bandarini bila kulipa kodi, walipe kodi waliyokwepa. Wengi wetu tunajua kuwa kukwepa kodi ni kosa la jinai.

Adhabu ya kukwepa kulipa kodi stahiki ni kubwa tu mhusika anapokutwa na hatia Mahakamani. Ni Rais Magufuli na Serikali yake ndiyo waliogundua ukwepaji kodi wa makontena pale Bandarini. Uchunguzi na kusimamishwa kazi watumishi ukafuata. Rais yuko serious juu ya kadhia hii.

Wakati watumishi wamepoteza na wengine kusimamishwa kazi, wafanyabiashara wahusika wametakiwa kulipa kodi walizokwepa ndani ya siku saba. Is it fair? Wafanyabiashara, jana, walimpigia makofi sana Rais Magufuli wakati akisema hivyo.

Wafanyabiashara hao wakubwa nchini walishusha pumzi na kushukuru kuepukwa na dhahama ya kisheria. Lakini, makontena husika yatajulikana yalikuwa na nini na hata kujua usahihi wa kodi ambayo wafanyabishara walikwepa?

Hakika, katika hili la wafanyabishara watenda jinai, Rais Magufuli amefanana na Rais Mstaafu Kikwete!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

nchi inayoongozwa kibepari wafanyabiashara na matajili ndio wanaoshika nchi, wakiungana matajiri 10 tu unaowafahamu ww, wahamishe au wafiche ndani hela zao nakuhakikishia nchi itayumba.nimesikia akisema anaetaka kuwekeza mahari fulani tutafanya haraka. hili pia linaweza kua tatizo wasipokua makini kwenye maeneo atakayotaka kuwekeza,maana ili mtu afungue kiwanda ni bora wachunguze kwanza mazingira,hasa kwenye maeneo ya karibu na makazi ya watu, tumeshudia kesi nyingi kwa jinsi wawekezaji walivyonyanyasa watu kwenye makzi yao. lakini yote kwa yote, hawa matajiri hasa wafanyabiashara wanatakiwa kuwa wazalendo na nchi yao.
 
Wale wafanyakazi wameajiliwa na wanalipwa na serikali na ndio maana wametolewa nduki,il wafanyabiashara huwezi kuwafunga,ila inabidi tu kulipa wanachodaiwa.harafu usimfananishe Mwizi mkwepa kodi

Mdau mkwepa kodi ni mwizi,yaani unaanzaje kuwatofautisha mwizi na mkwepa kodi?
 
Magufuli is a very smart guy!, ukiwa makini kumtafakari utagundua kuwa alikua ana peti peti wafanya biashara humo humo anawapiga madongo wajiongeze, kuna fursa nyingi za wao kuwekeza na wakiwa serious inchi hii itawanufaisha kwa kuwapatia faida halali, na wananchi kufaidi matunda ya nchi yao.

Hakusema amewasamehe walipa kodi, bali amewapa grace period ya siku saba ikiwa kuna mfanya biashara ambaye alikwepa kodi kwa namna yoyote ile akalipe. Hapa kwa uelewa wangu, kwenye kulipa kuna mengi, kuna ambao wataenda kulipa kiudanganyifu, na naamini tayari ana rekodi za kila mfanyabiashara namna alivyokwepa kodi. Its likely pia wapo ambao watapuuza agizo hilo, wapo ambao watakua ndio kama wamejipeleka wenyewe kwenye mikono ya sheria...

Ni mtego mkubwa sana amewawekea, ila mtu ukichukulia kwa haraka haraka huwezi kumuelewa lengo lake. JPM is very smart. Kawapiga madongo sana kwenye ule mkutano. Na ikumbukwe kasema kabisa wafanyabiashara ndio wamemuomba sana kukutana naye, hii inaonyesha wanajaribu kujiweka karibu naye, lakini magufuli anawajua vizuri sana.

Ngoja uone movie inayoufuata.
 
Inawezekana na yeye anaanza kurudi kwenye square one?
 
mfanyakazi ambae nimlipa kodi halali na mwaminifu kwa serikali ndio wakutishiwa kila siku..ntachelewa kusupport na kupongeza anachofanya Magufuli,naona majipu ya sasa yamegeuka manundu kwa mtumbuaji
 
Magufuli is a very smart guy!, ukiwa makini kumtafakari utagundua kuwa alikua ana peti peti wafanya biashara humo humo anawapiga madongo wajiongeze, kuna fursa nyingi za wao kuwekeza na wakiwa serious inchi hii itawanufaisha kwa kuwapatia faida halali, na wananchi kufaidi matunda ya nchi yao.

Hakusema amewasamehe walipa kodi, bali amewapa grace period ya siku saba ikiwa kuna mfanya biashara ambaye alikwepa kodi kwa namna yoyote ile akalipe. Hapa kwa uelewa wangu, kwenye kulipa kuna mengi, kuna ambao wataenda kulipa kiudanganyifu, na naamini tayari ana rekodi za kila mfanyabiashara namna alivyokwepa kodi. Its likely pia wapo ambao watapuuza agizo hilo, wapo ambao watakua ndio kama wamejipeleka wenyewe kwenye mikono ya sheria...

Ni mtego mkubwa sana amewawekea, ila mtu ukichukulia kwa haraka haraka huwezi kumuelewa lengo lake. JPM is very smart. Kawapiga madongo sana kwenye ule mkutano. Na ikumbukwe kasema kabisa wafanyabiashara ndio wamemuomba sana kukutana naye, hii inaonyesha wanajaribu kujiweka karibu naye, lakini magufuli anawajua vizuri sana.

Ngoja uone movie inayoufuata.

Mdau hata JK aliwaambia wale wa.EPA warudishe hela hakusema kama hatawashtak,na hatujui zilirud au lah
 
VUTA-NKUVUTE hata mimi jambo hili limenishangaza sana, tena nimesikitika sana, kwangu mimi naona JPM nae anawahadaa watanzania, anafanya sanaa. ..anendeleza yale yale ya mtani wangu JK. ..Najiuliza Kwani kukwepa kodi si kosa kisheria? Hao ni wezi wa fedha za umma. ..ndivyo ninavyo oona.

Najiuliza watakapokwenda kulipa kodi je kodi hiyo italipwa kwa ustahiki wake? Je itakuwa rahisi kujua ni bidhaa gani zilikuwemo kwenye makontena hayo? Na kwa kuwa walikwepa obviously kuna watu walichukua rushwa je hao watumishi nao watasamehewa?

Hapana hapa JPM umeniangusha. ...unapitia njia ile ile kwa hadaa kubwa. ..Hata hivyo sikuwa na imani sana kama kweli ungebadilika na kuibadili nchi hii. ...mikwala yako yote umenywea kwa wafanya biashara. ...basi bhana endelea na sanaa hii

Mimi kama mimi naunga hoja kitu alichokiamua Rais, wafanyabiashara walikwepa kodi kwa kusaidiana na Serikali iliyokuwa madarakani, tena wengine walitumia memo za Rais wa kipindi hicho.

Sasa kama Rais au memba wa familia yake alitumika kutoa ruhusa hizi, siyo rahisi rahisi tu kwenda kumkamata mtu huyo, maana yake hata Rais mstaafu inabidi akamatwe au mwana familia aliyehusika.

Kinachofanyika hapa kawapa nafasi ya kuepuka kuaibishana, na kama mtu hatakubaliana na hili, atamjua Magu ni nani na kutakuwa hakuna amani baina yao.

Nina imani na Rais.
 
Wale wafanyakazi wameajiliwa na wanalipwa na serikali na ndio maana wametolewa nduki,il wafanyabiashara huwezi kuwafunga,ila inabidi tu kulipa wanachodaiwa.harafu usimfananishe Mwizi mkwepa kodi

serikali ni nani sasa???
 
Kuna point hapa! Tusipinge tu kila kitu. Kwa nini aonee dagaa, na kuwaacha akina Sangara?;
 
Cost benefit analysis, mimi nadhani wamegundua huu ukwepaji kodi umefanywa na wafanyabiashara wengi sana kiasi kwamba ukiwafunga jela wote lazima uchumi uyumbe sana, kikubwa walipe ushuru na baada ya hizo siku saba iwekwe wazi ni kiasi gani kimelipwa na ni wafanyabiashara kiasi gani wameendelea kukiuka na watachukuliwa hatua gani. Mabadiriko lazima yawe na mahala pa kuanzia. From there on ward sheria iendelee kua msumeno
 
Hapo sasa ndio tusubirie, sio ku judge moja kwa moja, ndani hizi siku sita tutatjua tu kama similar to JK au lah!, nadhani tunahitaji kuwa na subira kabla hatujaanza kubeza.
 
Mimi kama mimi naunga hoja kitu alichokiamua Rais, wafanyabiashara walikwepa kodi kwa kusaidiana na Serikali iliyokuwa madarakani, tena wengine walitumia memo za Rais wa kipindi hicho.

Sasa kama Rais au memba wa familia yake alitumika kutoa ruhusa hizi, siyo rahisi rahisi tu kwenda kumkamata mtu huyo, maana yake hata Rais mstaafu inabidi akamatwe au mwana familia aliyehusika.

Kinachofanyika hapa kawapa nafasi ya kuepuka kuaibishana, na kama mtu hatakubaliana na hili, atamjua Magu ni nani na kutakuwa hakuna amani baina yao.

Nina imani na Rais.

kumbe wakina Bade ndio wanastahili kuaibishwa kwa kupewa vimemo lakini sio wale walio toa mamlaka!!!Jivike uhusika wa hao watendaji walio aibishwa na kufedheheshwa ,kwa maono na mawazo kama yakwenu we have long and wrong way to go...!!!tunapenda mabadiliko lakini hatuna utashi wakuyasimamia na kuyatekeleza hayo mabadiliko
 
Wanalipa kodi kuanzia mwaka gani? au trip ya mwisho tu!?
Kwa maana nyingine mfanyabiashara anathamani kuliko kamishna wa TRA.
 
Uamuzi huu ni muzuri kwa sababu huwezi jua ukwepaji kodi huu yawezekana ulifanyika kwa shinikizo flani
Hivyo ukiwaadhibu kwa kuwapeleka jela unaweza kuathiri uchumi.

Lakini tushukuru haya yanayofanywa na serikali ya jpm
Kwani ukawa walisema wao wakipewa nchi hawafukui makaburi na walisema.
Tena watunda tume ya muafaka wa kitaifa hii maana yake nini?

ANAYOYAFANYA LEO JPM NASEMA UKAWA WASINGEYAWEZA.
TUSIDAGANYANE.
 
tusubili siku 7 zipite afu tuje tuendelee na huu mjadala.
 
Back
Top Bottom