Kauli tata za Emmanuel Nchimbi vs Samia na kauli tata za Jakaya Kikwete vs Magufuli wakimnukuu baba wa taifa

Kauli tata za Emmanuel Nchimbi vs Samia na kauli tata za Jakaya Kikwete vs Magufuli wakimnukuu baba wa taifa

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
12,351
Reaction score
39,195
Miaka kadhaa iliyopita Kikwete akiwa mstaafu aliwahi kualikwa kwenye kigoda cha Mwalimu na wakati huo Magufuli akiwa Rais. Kikwete aliongea mambo ya kujimwambafai na ubabe kauli ambazo zilionyesha moja kwa moja kumnanga aliyekuwa Rais Magufuli kutokana na ubabe aliokuwa nao. Kikwete kamwe hakuwahi kuongelea mambo ya ufisadi kwenye kigoda hicho.

Miaka kadhaa mbele Rais Samia yupo madarakani na ni kana Makamu wake hamkubali kutokana na mienendo ya matamko yake anayotoa hadharani.

Kuna wakati alitoa hotuba akikemea wachawi kuisogelea ikulu ya Tanzania mara tukamuona akiwa kwa Papa anaombewa.

Leo tena katoa hotuba tata akitumia jukwaa lile lile la shughuli za kumbukumbu kwa Mwalimu Nyerere akikemea mafisadi na wezi huku akimnukuu mwalimu Nyerere kuwa mtu akikemea rushwa kweli kweli hata uso wake unaonyesha kuwa hadanganyi.

Mara ghafla hotuba hiyo ikaondolewa kwenye mtandao wa gazeti la serikali. Sote tunaoa uelekeo wa huu utawala kuhusu ufisadi. Ufisadi umeshamiri kuliko kawaida huku kukiwa na utendaji mbovu uliokithiri serikalini. Sasa awamu hii husikii kabisa kauli za ubabe na umwambafai, unasikia kauli za ufisadi, uzembe na kutokujua majukumu kwa wengi wa watendaji serikalini.

Ni kwamba watu wanatetea maslahi yao? Ninachojua kwenye mnyukano wa aina hii lazima mmoja apoteze, je awamu hii ni nani atapoteza?
 
ukiondoa alioko juu, hao wengine wasionyeshe hisia zao za kujifanya wazalendo.kutokana na rekodi za waliopita ote.hakuna alioko chini akaonesha tamaa yake ya kuthubutu kupambana na aliejuuyake akamshinda. ujinga wa ainahiyo ingekua sudani au kongo ni sawa,ila sio Tanzania ninayoijua mimi.
yeyote mwenye madaraka ya juu akitamani waziwazi nafasi ya urais ajue kabisa amechagua kufeli siasa.
 
As long as hao wote ni CCM sinaga imani na kauli zao hao wanafiki na wazandiki
 
Back
Top Bottom