Rais Magufuli, Kikwete na wafanyabiashara

Rais Magufuli, Kikwete na wafanyabiashara

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,006
Msije mkanilisha maneno baadaye. Nasema hapa hapa mwanzoni, si Rais Magufuli wala Kikwete ambaye anawaogopa au aliwaogopa wafanyabiashara. Wafanyabiashara ni watu muhimu kwa uchumi wa kitaifa. Lakini, natumai wote mnajua kama nijuavyo mimi, Rais Magufuli naye ameshajifananisha na Kikwete katika mambo yawahusuyo wafanyabishara.

Ulipotokea wizi wa mabilioni ya shilingi za kitanzania, yaliyochotwa isivyo halali BOT, Rais Mstaafu Kikwete aliwaamuru wafanyabiashara waliohusika 'kurudisha' fedha hizo. Ni kama Rais mstaafu aliwaambia wezi warudishe pesa walizoiba. Wananchi wakasema na kuhema hadi wakalala. Mambo yakapita. Hadi sasa, haijulikani kama zilirudishwa au la na kwa kiwango gani. Maisha yanasonga.

Jana, Rais Magufuli amewapa siku saba wafanyabiashara, waliohusika na kupitisha makontena yao Bandarini bila kulipa kodi, walipe kodi waliyokwepa. Wengi wetu tunajua kuwa kukwepa kodi ni kosa la jinai.

Adhabu ya kukwepa kulipa kodi stahiki ni kubwa tu mhusika anapokutwa na hatia Mahakamani. Ni Rais Magufuli na Serikali yake ndiyo waliogundua ukwepaji kodi wa makontena pale Bandarini. Uchunguzi na kusimamishwa kazi watumishi ukafuata. Rais yuko serious juu ya kadhia hii.

Wakati watumishi wamepoteza na wengine kusimamishwa kazi, wafanyabiashara wahusika wametakiwa kulipa kodi walizokwepa ndani ya siku saba. Is it fair? Wafanyabiashara, jana, walimpigia makofi sana Rais Magufuli wakati akisema hivyo.

Wafanyabiashara hao wakubwa nchini walishusha pumzi na kushukuru kuepukwa na dhahama ya kisheria. Lakini, makontena husika yatajulikana yalikuwa na nini na hata kujua usahihi wa kodi ambayo wafanyabishara walikwepa?

Hakika, katika hili la wafanyabishara watenda jinai, Rais Magufuli amefanana na Rais Mstaafu Kikwete!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
VUTA-NKUVUTE hata mimi jambo hili limenishangaza sana, tena nimesikitika sana, kwangu mimi naona JPM nae anawahadaa watanzania, anafanya sanaa. ..anendeleza yale yale ya mtani wangu JK. ..Najiuliza Kwani kukwepa kodi si kosa kisheria? Hao ni wezi wa fedha za umma. ..ndivyo ninavyo oona.

Najiuliza watakapokwenda kulipa kodi je kodi hiyo italipwa kwa ustahiki wake? Je itakuwa rahisi kujua ni bidhaa gani zilikuwemo kwenye makontena hayo? Na kwa kuwa walikwepa obviously kuna watu walichukua rushwa je hao watumishi nao watasamehewa?

Hapana hapa JPM umeniangusha. ...unapitia njia ile ile kwa hadaa kubwa. ..Hata hivyo sikuwa na imani sana kama kweli ungebadilika na kuibadili nchi hii. ...mikwala yako yote umenywea kwa wafanya biashara. ...basi bhana endelea na sanaa hii
 
Hapa napita tu ila hata mm nimekwazika, naona kama ameamua kuwabeba watu Fulani then wakipe kodi mambo yao yasiharibike, watakuja kukamatwa vijitu vidooogo tu,

Basi kama kaamua hivyo Na wale wafanyakazi warejeshwe makazini baada ya hawa jamaa kulipa kodi maana sheria n msumeno
 
Kwa kweli JPM hapa ametuangusha. Wakileta wenyewe maana yake hakuna penalties. Ni hasara kwa Taifa.
 
Mimi sioni tatizo. Wanalipa kodi waliyokwepa. Hajawasamehe. Ubaya uko wapi? Ukizingatia hii n serikali mpya lazima acompromise. Hajataka kuweka mpasuko na wafanyabiashara.

Kuwawajibisha watumishi na kuweka wapya n salam tosha kuwa hawatosaidia tena ukwepaji kodi. Tunaanza upya.



Hongera magufuli
 
Kusema kweli hadi simwelewi tena huyu makufuli. kama ni TRENI basi imeshaanza kupoteza uelekeo mapema asubuhiiiiiii!
 
Lazima uangalie nyakati, sikumbuki kwa JK ni muda gani alitoa agizo baada ya kuingia madarakani, JPM ndo kwanza ana mwezi, wafanyabiashara wakubwa ni watu wa muhimu sana, karata yake ya kwanza lazima aicheze vizuri na hawa watu. Kawapa grace period, na tuwe fair, JPM anachosema anamaanisha! Tusubiri hizo siku sita zilizobaki!
 
How absurd! Hao wafabyabiashara wangekuwa wamefanya kosa la kuua, rais angewaambia warudishe nini baada ya siku 7?
 
Mtamwelewa tu.....
Yupo sahihi na kama hamjui watu wamewekewa mitego kitakachofuata mtarudi hapa kuniambia
 
timu ya taifa ni ileile? wachezaji walewale? ari ileile? ushindi upo?
 
Kwa kweli JPM hapa ametuangusha. Wakileta wenyewe maana yake hakuna penalties. Ni hasara kwa Taifa.

Huenda amepigiwa magoti asiwaaibishe watoto wa wakubwa akaona huruma.Ila watumishi watakuwa makini zaidi sasa.
 
Kuongoza ni hekima, mbona Wafungwa wakisamehewa na Raisi hamshangai?

Sheria zipo, lakini kuongoza kunahitaji mambo yote yaani busara, hekima na sheria.

Wanaotaka Magufuli awashitaki watu hao ili " Waridhike", basi watu hao nao pia wawe tayari kuchunguzwa nyumba na mali zao wamezipataje, wachunguzwe kama wamezilipia kodi etc etc
 
Lazima uangalie nyakati, sikumbuki kwa JK ni muda gani alitoa agizo baada ya kuingia madarakani, JPM ndo kwanza ana mwezi, wafanyabiashara wakubwa ni watu wa muhimu sana, karata yake ya kwanza lazima aicheze vizuri na hawa watu. Kawapa grace period, na tuwe fair, JPM anachosema anamaanisha! Tusubiri hizo siku sita zilizobaki!

Ni kichekesho. Hizo kodi walizokwepa Magufuli anajua zilikuwa mali gani? Atajuaje kodi iliyokwepwa ni kiasi gani wakati hujui bidhaa iliyokwepwa ni nini na kiasi gani?

Sanaa siasani....
 
Pamoja na kuwa nilimwelewa kuwa uchumi unaweza shuka kama wafanya biashara watakuwa frustrated kwa tifua tifua hii, lakini wafanyabiashara ni wajanja sana; wamemwalika Rais mapema mapema ili kujisogeza karibu naye. Ninamwomba Mh. Rais awe makini sana na hao watu maana hata kama ni muhimu lakini umuhimu wao hauzidi wakulima na wafanyakazi wa Tanzania ambao ndiyo wakiishikilia uchumi wa nchi hii kama Rais alivyofafanua jana.

Hao wafanyabiashara wengi wao siyo wazalishaji ni wachuuzi tu kwahiyo mara nyingi sera zao na kutokana na nafasi ealiyojiwekea wamekuwa wakiyumbisha sana mwelekeo wa serikali katika kutengeneza uchumi imara na thabiti. Rais mwenyewe ameeleza jana kuwa biashara yote inafanywa na serikali kupitia mashirika ya umma na wazalishaji pamoja na walipa kodi wakuu ni wakulima na wafanyakazi. Sasa hiyo hofu ya kwamba eti wakiwa frustrated uchumi utayumba inatoka wapi? Hao ni midle man tu na practice zao ina fananafanana na hiyo kashfa ya London na mabenki, yaani wanaogeza % zisizo lazima katika value chain.

Rais wangu nakuomba sana usijeingia katika mtego wa hao watu. Kama walitenda kosa la jinai wawajibike kama ambavyo wafanyakazi wa serikali wamewajibika.

Mheshimiwa Rais wafanyakazi wapo kwenye mgomo usio rasmi kwa muda mrefu kutokana na haohao watu kuwabebesha mzigo mzito wa kulipa kodi huku wao wakiwekeza kwakutumia mitaji iliyotokana na hao hao walipa kodi (michango yao kwenye sekta ya umma kama pension) na wao kujipa nafasi ya kwanza katika biashara na serikali kupitia uchochoro wa tenda huku ukirahisishwa na sheria ya manunuzi. Ni vyema ukafahamu hilo, nakuwa hakuna uzalishaji wowote wanaoufanya zaidi ya kuwa middle men na kuweka riba kubwa hapo katikati huku wazalishaji ambao ndiyo wenye kushikilia uchumi wakiambulia hasara katika uzalishaji wao; hiyo ndiyo sababu uchumi wa taifa net value yake au marginal return ni negative (deni kubwa la taifa).

Kwahiyo mheshimiwa Rais ninakuomba sana kwakua umetamka msamaha tafuta informal ways la ku rejebisha hilo hata kama huta futa kauli yako maana ukifuta kwa sasa utotoa taswira huna msimamo. Baada ya hapo Mh. Rais nakuomba sana kaa mbali na hao wajanja mimi naamini kabisa ndiyo walioifikisha hii nchi hapo ilipo. Kama ulivyowaambia wawekeze wazalishe na waliope kodi basi hayo mengine yanayohusu sera raia wote wapewe nafasi sawa na kila mtu apewe haki yake stahiki. Ninasema hivyo kwakuwa hao hao ndiyo waliotuletea mambo kama BRN, kilimo kwanza etc ambazo ni paralell institutions zilizo weaken institutions zingine zinazo zalisha huku ndani ya hizo program zikiwepo mambo ya ujanjaujanja na udalali mwingi uliosababisha hata uzalishaji kutokuwa sustainable huku hao hao wakijipa mikopo na fursa nakusahau kuwa huko grasroot ndipo kwenye wazalishaji hasa ambao wanachangia pato kubwa la taifa katika ummoja wao. Hao hawaonrkani kwani wakiwekea mmojammoja utadhani nguvu yao ni ndogo lakini integration ya changuzo lao katika taifa hao bussiness community kwa ujumla wao hawafikii hata robo. Tofauti yao ni kuwa hao wanaoitwa matajiri mmojammoja ukilinganisha mapato yao na hao wengi wakiwekea mmojammoja hao wenye pato kubwa wanaonekana in absolute term ni wakubwa; lakini tukija kwenye marginal values hao mchango wao ni mdogo ukilinganisha na kundi la wafanyakazi na wakulima wadogowadogo.
 
Kuongoza ni hekima, mbona Wafungwa wakisamehewa na Raisi hamshangai?

Sheria zipo, lakini kuongoza kunahitaji mambo yote yaani busara, hekima na sheria.

Wanaotaka Magufuli awashitaki watu hao ili " Waridhike", basi watu hao nao pia wawe tayari kuchunguzwa nyumba zao wamezipataje, wachunguzwe kama wamezilipia kodi etc etc

Swala sio kuwashtaki... swala ni kuwatoza faini. Kama wafanyakazi unawaadhibu kwa kuwafukuza kazi kwanini wafanyabishara wasiadhibiwe kwa kuwatoza faini??
 
Mambo yameshaanza kuharibika,kweli nimeamini dogo jembe ni noma kapiga mkwala wa vikatuni tu mzee wa chato chaliiii
 
Wale wafanyakazi wameajiliwa na wanalipwa na serikali na ndio maana wametolewa nduki,il wafanyabiashara huwezi kuwafunga,ila inabidi tu kulipa wanachodaiwa.harafu usimfananishe Mwizi mkwepa kodi
 
Back
Top Bottom