Rais Magufuli, Kikwete na wafanyabiashara

Rais Magufuli, Kikwete na wafanyabiashara

JPM yuko sahihi kabisa:
(1) Ukwepaji kodi bandarini ulikuwa widespread, na naamini majority yake unahusisha vimemo vya ikulu, na wakubwa wa serikali iliyopita. Sasa kwa kuwa ndio ameingia madarakani, si sawa kuanza tu unafungafunga wafanyabiashara wakubwa wengi hivyo, lazima uwape 'breathing space' ya wao kua-adjust katika mazingira mapya ya serikali mpya ambayo haina mchezo, ndio maana amewapa muda.
(2) JPM akianza kwa kufunga wafanyabiashara ovyo, ingeleta signa mbaya kwa hata wawekezaji wengine kitaifa na kimataifa kuwa serikali haina dialogue na wafanyabishara, kitu ambacho ni muhimu sana
(3) Kufunga au kufilisi biashara kubwakubwa e.g. Bakhresa kunaweza kuwa na athari mbaya sana kwa upande wa ajira na kodi nyingine. HIvyo inabidi uende nao taratibu huku ukiwafanya watambua kuwa mazingira na serikali vimebadirika
(4) kutoa siku saba sio kuvunja sheria, hata sisi kwenye vibiashara zetu, TRA inatupaga mda fulani kulipa kodi vinginevyo wanachua hatua kali, kwa hiyo ni sawa kabisa kwa kutoa 'grace period'
(5) Ni ujinga kusema kuwa kama wafanyabiashara wanasamehewa na wafanyakazi wa TRA na TPA nao wasamehewe: kumbuka kama wafanyakazi hao wa umma wangesimamia taratibu na maadili ya kazi zao hakuna mfanyabiashara angeweza kutorosha makontena hata angekuwa na fedha kiasi gani. Na bila shaka wafanyakazi ndio waliowa shawishi wafanyabiashara wakwepe kodi na hata kuwapa njia jinsi ya kufanya hivyo. Ni sawa na kumlaumu mgoni wakati mke kajitongozesha mwenyewe na kujipeleka gesti kwa hiari yake.

Mwisho: tumwache JPM afanye kazi, tumuamini, wakati mwingine sheria tu na maguvu ya serikali haviwezi kusaidia sana kama busara, maonyo na mazungumzo. Tumpime baada ya hizo siku 7 tuone anafanya nini kwa wale watakaokaidi.
 
Me,
Nilitaka kujua tuu Kwa wataalamu wa sheria na uchumi,

Hapa ni wakwepa KODI wanatakiwa kulipa hiyo Kodi, ambayo tuna jua hii wasinge lipa au wangeilipa pole pole? kwanini Nimeuliza hivyo nataka hili liwekwe bayana kisheria ya kodi

Naombeni majibu kwa swali hili chini hapa au ufafanuzi
( Umeshusha mzigo wako Bandarini or Umepita bandari ya Mombasa au umetua any International Airport within EAC Swali langu Je huo mzigo utapita hivi hivi au Unatakiwa lipwa Kodi inayotakiwa? Na kwa kawaida hizo sehemu zote tajwa lazima ukomboe mzigo wako kwa kulipa kodi na ndio utoke)

Kwa wafanyabiashara hawa waliokuta na rais ningelipenda kujua wao wana azingingira gani ya kulipa kodi pindi waingizapo mzigo ndani ya nchi hiii huwa wana kipindi cha ku clear mizigo yao au na waou hulipa direct mzigo ufikapo na mda anapotaka kuutoa lazima alipe ndio mzigo utoke?

My Take:
JPM anatupa shaka saaaana pindi anapo taka kutuambia kwamba anataka kufanya mfumo mzuri kuwa ufuatwe kwa kuwapa wafanyabiashara mda ili waweke record zao sawa ndani ya siku 7 then ndio mfumo ufuatwe siju hii itawezekana kweli?

Scandal ya EPA wakati wa JK hali ilikuwa kama hiii ya JPM sasa mrejesho wa EPA haukuwa wazi mpaka leo, Je na hili la wafanya biashara wakubwa itakuwaje?

Inanipa shaka saaana JPM kuamini kuwa ataweza kwendana na kasi yake yeye mwenyewe maana anaaanza kinzana na mwenendo wake. Au CCM ule mfumo wao ambao wapinzani walitaka utoke kumbe unarudi kwa kivingine kwa kuwa mbwa mkali lakini haliwezi kuuma wala kufukuza majizi na vibaka. mna kumbuka wimbo wa Joti Mbwa wenu ni mkali lakini hang'ati. Hii ndio Tafsili inayo kuja kwa wananchi sasa.

IKULU inapaswa kuwa na watu makini sana wa kumwongoza JPM na wenzake wasikurupuke lazima kuwe na wataalamu wa sheria, Uchumi na vinginevyo ili nchi isingie kwenye mkanganyiko na sintofahamu
 
kwahili suala la kuwapa muda wafanyabiashara waliokwepa kodi magufuri amechemka na ameonesha double standards kati ya wafanyakazi na wafanyabiashara, kukwepa kodi ni kosa la jinai sasa inakuwaje wapewe muda wa kulipa na wakati kuna wafanyakazi wanapelekwa mahakamani kwa issue hiyo hiyo?
hii inaonesha aina ya utawala tkao kuwa nao kwa miaka kadhaa ijayo, old wine in new bottle!
 
Kwa hali ya sasa ya ulimwengu, Wafanyabiashara ndiyo nguzo ya uchumi. Ukiwashughulikia vibaya basi uchumi utayumba..
Kwa wale wanaokumbuka vita ya Wahujumu Uchumi na Walanguzi miaka ya 1983-84.. Nchi iliyumba.. Uchumi ukayumba.. Ilibidi Rais Nyerere aingilie kati kupunguza kasi ya Marehemu Sokoine na kutoa agizo kuwa wenye 'mali za magendo wazisalimishe Polisi na Polisi waangalie mbali'..
Hivyo JPM hajakosea kufanya anayofanya, anakuwa mwerevu ('using carrot-and-stick'). Anajua huwezi kukusanya kodi yote iliyokwepwa sasa hivi kwa kutumia sheria pekee bila kuyumbisha uchumi. hata hivyo hajaanza vibaya kama ataendelea na kasi hiyo na kujenga Taasisi imara.
 
Me,
Nilitaka kujua tuu Kwa wataalamu wa sheria na uchumi,

Hapa ni wakwepa KODI wanatakiwa kulipa hiyo Kodi, ambayo tuna jua hii wasinge lipa au wangeilipa pole pole? kwanini Nimeuliza hivyo nataka hili liwekwe bayana kisheria ya kodi

Naombeni majibu kwa swali hili chini hapa au ufafanuzi
( Umeshusha mzigo wako Bandarini or Umepita bandari ya Mombasa au umetua any International Airport within EAC Swali langu Je huo mzigo utapita hivi hivi au Unatakiwa lipwa Kodi inayotakiwa? Na kwa kawaida hizo sehemu zote tajwa lazima ukomboe mzigo wako kwa kulipa kodi na ndio utoke)

Kwa wafanyabiashara hawa waliokuta na rais ningelipenda kujua wao wana azingingira gani ya kulipa kodi pindi waingizapo mzigo ndani ya nchi hiii huwa wana kipindi cha ku clear mizigo yao au na waou hulipa direct mzigo ufikapo na mda anapotaka kuutoa lazima alipe ndio mzigo utoke?

My Take:
JPM anatupa shaka saaaana pindi anapo taka kutuambia kwamba anataka kufanya mfumo mzuri kuwa ufuatwe kwa kuwapa wafanyabiashara mda ili waweke record zao sawa ndani ya siku 7 then ndio mfumo ufuatwe siju hii itawezekana kweli?

Scandal ya EPA wakati wa JK hali ilikuwa kama hiii ya JPM sasa mrejesho wa EPA haukuwa wazi mpaka leo, Je na hili la wafanya biashara wakubwa itakuwaje?

Inanipa shaka saaana JPM kuamini kuwa ataweza kwendana na kasi yake yeye mwenyewe maana anaaanza kinzana na mwenendo wake. Au CCM ule mfumo wao ambao wapinzani walitaka utoke kumbe unarudi kwa kivingine kwa kuwa mbwa mkali lakini haliwezi kuuma wala kufukuza majizi na vibaka. mna kumbuka wimbo wa Joti Mbwa wenu ni mkali lakini hang'ati. Hii ndio Tafsili inayo kuja kwa wananchi sasa.

IKULU inapaswa kuwa na watu makini sana wa kumwongoza JPM na wenzake wasikurupuke lazima kuwe na wataalamu wa sheria, Uchumi na vinginevyo ili nchi isingie kwenye mkanganyiko na sintofahamu

Rais anataka walipwe kwanza kodi zote na waendelee na biashara zao. Ila ni lazima walipwe penalty zote. Tunataka kodi na tutazipata wakiendelea kaagiza bidhaa. Alisema hili ni onyo la mwisho. Hao watumishi walioruhusu mizigo wafukuzwe kazi na kushitakiwa kama kuna ushahidi wa rushwa.
 
kumbe wakina Bade ndio wanastahili kuaibishwa kwa kupewa vimemo lakini sio wale walio toa mamlaka!!!Jivike uhusika wa hao watendaji walio aibishwa na kufedheheshwa ,kwa maono na mawazo kama yakwenu we have long and wrong way to go...!!!tunapenda mabadiliko lakini hatuna utashi wakuyasimamia na kuyatekeleza hayo mabadiliko

Binadamu hawana jema mkuu, kila unalolifanya kuna watakaoafiki na kuna watakao likataa, labda nikuulize, kama wewe ndo ungekuwa Rais ungelichulia hatua gani hili swala?

Maana tusiishie kulaumu peke yake, tuweke ni njia mbadala za kuchukua hapa.
 
Sheria ya kodi ni lazima ulipena faini. Kama akishindwa kulipa ndio atashitakiwa kwa kushindwa kulipa kodi. huweizi kusema eti wafungwe na wafilisiwe mali zao. Hizo zitakuwa chuki tu. halafu system ndio inaruhusu. Kodi ni nyingi na kubwa mno ndio maana wafanya biashara wanakwepa.

BTW. Psychologically, watu wengi wasiofanya biashara huwa wana chuki na wafanyabiashara ambayo wala huweizi kuelezea chanzo chake. The have not hate the haves. Na tanzania hii iko juu sana. Ukisoma huu uzi kwa makini wengi wanelekea huko huko.

Let us be more positive on solving problems.
 
Siamini kwamba uongozi ni kufuata sheria peke yake. iko wapi nafasi ya hekima na busara kwenye uongozi.

Rais akitumia sheria peke yake bila hekima na busara tutafika salama huko tuendako?
 
Lazima uangalie nyakati, sikumbuki kwa JK ni muda gani alitoa agizo baada ya kuingia madarakani, JPM ndo kwanza ana mwezi, wafanyabiashara wakubwa ni watu wa muhimu sana, karata yake ya kwanza lazima aicheze vizuri na hawa watu. Kawapa grace period, na tuwe fair, JPM anachosema anamaanisha! Tusubiri hizo siku sita zilizobaki!

barafuyamoto;
Mbona mnapenda kujitia wazimu ki hivi?? Nataka uelewe kwamba, hatuwakatai wafanya biashara, wala soko halitakiwi kuambiwa limejaa. Lakini, tunataka mfanya biashara anayekuja kufanya biashara yake ili alipe kodi. Tukipata kodi, tumepata maendeleo.
Anapotokea mfanyi biashara mwenye kuja na mbinu zake za kukwepa kodi lakini biashara yake iendelee huyo sio mfanyi biashara bali ni mwizi wa gizani. Hakuna mtu mbaya kama huyo. Hukumu yake ingefaa afilisiwe na hata kunyongwa hadharani ili wengine wakija waje kupitia njia nyeupe. Tanzania imesema ipo wazi na inakaribisha wawekezaji si majambazi makwepa kodi.
Huyu ni mwizi tena mhujumu uchumi. Sasa JPM anavyo waambia kiungwana ati jipelekeni wenyewe mkalipe hiyo kodi, jiulize yafuatayo:
Huyo mkwepa kodi, anaaminika vipi kuwa hiyo kodi anayolipa leo ndiyo ya kweli?? Tofautisha na mcheleweshaji kodi na mkwepa kodi. Mcheleweshaji kodi, hesabu yake ipo pale pale ila mkwepa kodi ni nani anajua kilicho kwepeshwa??
Jiulize, hao walioshiriki naye walipewa ngapi? Je, watazirudisha serekalini? Kwa sababu si zao za halal.
JPM, ameshaingizwa kwenye system ya ccm. CCM, tajiri hakosei kwani ndiye kampeleka Ikulu. Tulikuwa tunachanganywa ubongo tusahau Uchaguzi Zenj. Sasa, tutaanza kweli kuisoma ile namba
 
Au ndo mana tulisema wakati wa kampeni, Magufuli ni mzuri, tatizo ni mfumo, .
 
Jana alisema kuwa hakuchangiwa na mfanya biashara yeyote kwenye mbio zake za urais, je anamjua aliyefadhili mabango yake yote nchi nzima? Hapo hakwepi, ameshakwama.
 
Cost benefit analysis, mimi nadhani wamegundua huu ukwepaji kodi umefanywa na wafanyabiashara wengi sana kiasi kwamba ukiwafunga jela wote lazima uchumi uyumbe sana, kikubwa walipe ushuru na baada ya hizo siku saba iwekwe wazi ni kiasi gani kimelipwa na ni wafanyabiashara kiasi gani wameendelea kukiuka na watachukuliwa hatua gani. Mabadiriko lazima yawe na mahala pa kuanzia. From there on ward sheria iendelee kua msumeno

Dah, wote tungekuwa tunafikiri kama wewe, malalamiko yangepungua sana humu JF, numekuelewa sana
 
Binadamu hawana jema mkuu, kila unalolifanya kuna watakaoafiki na kuna watakao likataa, labda nikuulize, kama wewe ndo ungekuwa Rais ungelichulia hatua gani hili swala?

Maana tusiishie kulaumu peke yake, tuweke ni njia mbadala za kuchukua hapa.
Katika mazungumzo yangu na watu kadhaa niliwahi kusema kwa jinsi nchi ilipo fikia na kwa juhudi kubwa sana za Kikwete na familia yake kutuweka hapa tulipo kwanza kabisa ilitakiwa tutafute muafaka wahaya yote ,hakuna ambae alikuwa hajui bandarini na TRA kama kuna wizi kila mtu alikuwa anajua hilo lakini wengi wetu wenzangu na mimi hatukujua ni kwakiwango gani,watendaji wazembe ilikuwa ndio wimbo wakila siku ubadhirifu nakadhalika..!!! Je tulisha wahi kujiuliza tatizo ni nini kwanini wafanyabiashara hawalipi kodi,kwanini watendaji wa serikali wanakuwa wabadhirifu? kama tunania yadhati ya kupambana na haya lazima tufanye national reconciliation kwa kutambulisha upya katiba mpya itayoendana na wakati wasasa na kila mmoja alie kwenye ofisi ya umma au anae fikiria kuhudumia umma ajue analindwa na kusimamiwa na vifungu vya sheria...kuna kaulimoja Obama aliitoa anakwambia hata yeye kama raisi wamarekani anajua akikosea walinzi walionyuma yake wakati huohuo akatiwandani na kushitakiwa..!!Sheria lazima zifuatwe ndo lengo la msingi
 
Mkuu kwenye haya maelezo sijaona kama umejibu swali nililoliuliza, ungekuwa wewe ungefanyaje?

Au ni kwa jinsi gani unaona hili linaweza kufanyika?
 
Na tatzo kubwa la wafanyabiashara wa Tz hawa engage kwenye production wapo kama ma middlemen tu wanaishi kiujanja ujanja walipe kodi yetu na penalties zilipwe sababu kama watalipa kodi bila Penalties wats a point ya kuwaadabisha wale watumish wa umma ?
 
Msije mkanilisha maneno baadaye. Nasema hapa hapa mwanzoni, si Rais Magufuli wala Kikwete ambaye anawaogopa au aliwaogopa wafanyabiashara. Wafanyabiashara ni watu muhimu kwa uchumi wa kitaifa. Lakini, natumai wote mnajua kama nijuavyo mimi, Rais Magufuli naye ameshajifananisha na Kikwete katika mambo yawahusuyo wafanyabishara.

Ulipotokea wizi wa mabilioni ya shilingi za kitanzania, yaliyochotwa isivyo halali BOT, Rais Mstaafu Kikwete aliwaamuru wafanyabiashara waliohusika 'kurudisha' fedha hizo. Ni kama Rais mstaafu aliwaambia wezi warudishe pesa walizoiba. Wananchi wakasema na kuhema hadi wakalala. Mambo yakapita. Hadi sasa, haijulikani kama zilirudishwa au la na kwa kiwango gani. Maisha yanasonga.

Jana, Rais Magufuli amewapa siku saba wafanyabiashara, waliohusika na kupitisha makontena yao Bandarini bila kulipa kodi, walipe kodi waliyokwepa. Wengi wetu tunajua kuwa kukwepa kodi ni kosa la jinai.

Adhabu ya kukwepa kulipa kodi stahiki ni kubwa tu mhusika anapokutwa na hatia Mahakamani. Ni Rais Magufuli na Serikali yake ndiyo waliogundua ukwepaji kodi wa makontena pale Bandarini. Uchunguzi na kusimamishwa kazi watumishi ukafuata. Rais yuko serious juu ya kadhia hii.

Wakati watumishi wamepoteza na wengine kusimamishwa kazi, wafanyabiashara wahusika wametakiwa kulipa kodi walizokwepa ndani ya siku saba. Is it fair? Wafanyabiashara, jana, walimpigia makofi sana Rais Magufuli wakati akisema hivyo.

Wafanyabiashara hao wakubwa nchini walishusha pumzi na kushukuru kuepukwa na dhahama ya kisheria. Lakini, makontena husika yatajulikana yalikuwa na nini na hata kujua usahihi wa kodi ambayo wafanyabishara walikwepa?

Hakika, katika hili la wafanyabishara watenda jinai, Rais Magufuli amefanana na Rais Mstaafu Kikwete!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Wewe mnafiki unacho takiwa kujua hamaanishi kuwa watasamehewa bali hiyo ni njia ya kuwakamata kwa kujipeleka wenyewe!
 
Wewe mnafiki unacho takiwa kujua hamaanishi kuwa watasamehewa bali hiyo ni njia ya kuwakamata kwa kujipeleka wenyewe!

Sawa wewe usiye mnafiki. Tutaona kama watakamatwa wakienda kulipa. Kijana una mihemko kuliko hoja. Kama huelewi hoja si uulize?

Mzee Tupatupa
 
Nimemsikiliza sana mh. Rais akiongea, hakika amenipa
matumaini makubwa.
 
Back
Top Bottom