Rais Magufuli, Kikwete na wafanyabiashara

Rais Magufuli, Kikwete na wafanyabiashara

Hatua ya Raisi kusema wakalipe Kodi bila kwanza makontena kupatikana na kujulikana kulikuwa na nini ndani yake-ni kumweka Raisi kwenye mitego mibovu kuliko kitu kingine-maana kesho waweza shangaa mmoja ya makontena yanayodaiwa kupotea kukakuta picha na video limepostiwa humu JF ndani yake likiwa na Sembe-mie nawaza tu!

mrema enzizake alishawahi kukamata kontena la sembe, wakati kesi iko mahakamani wenzake wamepakua mzigo wakaweka. mabox tupu, siku anaihakikishia mahakama
kua anauhakika ndani kuna sembe mahaka kama kawaida ya kuheshim ushahidi ,wakalifungua na wakakuta mabox tupu.mrema hajaamini kilichotokea.yaan hawa matajiri na wafanyabiashara wa tz ukiwchekea, watekulusha kichurachura.
 
Ningependa nami nitoe maono yangu juu ya hili,kwanza lazima tukubali kwa kitendo cha rais Magufuli kuwaita wafanya biashara na kuongea nao ni busara tosha kwani alikuwa na uwezo akatuma wakamatwe wale wote waliokwepa kulipa kodi ya serikali na wakashughulikiwa mara moja,aliona kwanza awajue physically na pia awasikie maoni yao huku utaratibu wake bado anao mwenyewe,pia hawa wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi tuseme haki, ni kutokana na utaratibu waliowekewa before,sasa,nini kinachofanyika ni kuwaweka karibu na serikali yenye taratibu za ulipaji kodi kisheria na wala si suala la kuwa na vita na wafanyabiashara.Matumaini yetu ni kwamba wafanyabiashara washatambua kuwa kulipa kodi sasa ni wajibu sio kuifanya nchi kama wa waavyoweza
napia serikali bado inawajali sana na tena wanayo nafasi kubwa tu kuleta tija nyingi ktk maendeleo ya nchi yetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,
MUNGU IBARIKI AFRIKA

MAGUFULI TUPO PAMOJA NA WEWE
 
Msije mkanilisha maneno baadaye. Nasema hapa hapa mwanzoni, si Rais Magufuli wala Kikwete ambaye anawaogopa au aliwaogopa wafanyabiashara. Wafanyabiashara ni watu muhimu kwa uchumi wa kitaifa. Lakini, natumai wote mnajua kama nijuavyo mimi, Rais Magufuli naye ameshajifananisha na Kikwete katika mambo yawahusuyo wafanyabishara.

Ulipotokea wizi wa mabilioni ya shilingi za kitanzania, yaliyochotwa isivyo halali BOT, Rais Mstaafu Kikwete aliwaamuru wafanyabiashara waliohusika 'kurudisha' fedha hizo. Ni kama Rais mstaafu aliwaambia wezi warudishe pesa walizoiba. Wananchi wakasema na kuhema hadi wakalala. Mambo yakapita. Hadi sasa, haijulikani kama zilirudishwa au la na kwa kiwango gani. Maisha yanasonga.

Jana, Rais Magufuli amewapa siku saba wafanyabiashara, waliohusika na kupitisha makontena yao Bandarini bila kulipa kodi, walipe kodi waliyokwepa. Wengi wetu tunajua kuwa kukwepa kodi ni kosa la jinai.

Adhabu ya kukwepa kulipa kodi stahiki ni kubwa tu mhusika anapokutwa na hatia Mahakamani. Ni Rais Magufuli na Serikali yake ndiyo waliogundua ukwepaji kodi wa makontena pale Bandarini. Uchunguzi na kusimamishwa kazi watumishi ukafuata. Rais yuko serious juu ya kadhia hii.

Wakati watumishi wamepoteza na wengine kusimamishwa kazi, wafanyabiashara wahusika wametakiwa kulipa kodi walizokwepa ndani ya siku saba. Is it fair? Wafanyabiashara, jana, walimpigia makofi sana Rais Magufuli wakati akisema hivyo.

Wafanyabiashara hao wakubwa nchini walishusha pumzi na kushukuru kuepukwa na dhahama ya kisheria. Lakini, makontena husika yatajulikana yalikuwa na nini na hata kujua usahihi wa kodi ambayo wafanyabishara walikwepa?

Hakika, katika hili la wafanyabishara watenda jinai, Rais Magufuli amefanana na Rais Mstaafu Kikwete!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
CCM ni ile ile,watu ni wale wale,mfumo ule ule,sera zile zile na ahadi zile zile, tofauti yao tu ni majina,kabila,dini na mikoa wanayotoka then wadanganyika wanasubilia kitu tofauti
 
Mimi sioni tatizo. Wanalipa kodi waliyokwepa. Hajawasamehe. Ubaya uko wapi? Ukizingatia hii n serikali mpya lazima acompromise. Hajataka kuweka mpasuko na wafanyabiashara.

Kuwawajibisha watumishi na kuweka wapya n salam tosha kuwa hawatosaidia tena ukwepaji kodi. Tunaanza upya.

Hongera magufuli
mkuu alivyoambiwa aache ubabe wa bomoa bomoa aliwaambia wabunge wabadirishe sheria ili upana wa barabara uwe mita mbili yeye atatekeleza tu.sasa hata hili la ukwepaji kodi kama hataki kuleta mpasuko na wafanyabiashara alitakiwa akabadilishe sheria kwanza au kuifuta kabisa ndo atoke hadharani,otherwise atekeleze sheria kama alivyoapa kuzilinda pale uwanja wa uhuru tarehe 5.11.2015
 
Naona UKIWA,wanatafuta Matumaini Kwa Kuangalia Makosa Pasipo Kujua Undani Wa Mambo Yenyewe Mmeshaanza Nyie!
 
Mimi sioni tatizo. Wanalipa kodi waliyokwepa. Hajawasamehe. Ubaya uko wapi? Ukizingatia hii n serikali mpya lazima acompromise. Hajataka kuweka mpasuko na wafanyabiashara.

Kuwawajibisha watumishi na kuweka wapya n salam tosha kuwa hawatosaidia tena ukwepaji kodi. Tunaanza upya.

Hongera magufuli
Kabisa kabisaWasotakia mema nchi hii wataanza kuyumbisha watu. Ni strategy nzuri hebu nipe ata za walorudisha hizo pesa awamu ilopita!!!
 
Wakuu habari za muda.

Leo nikiwa hoteli moja maarufu hapa mjini (jina nalihifadhi) kupata chakula cha mchana, nimekuta watu watano ambao walikuwa na maongezi makubwa kidogo.

Watu hawa ambao kwa muonekano ni kama maofisa wa idara ya serikali ambao inaonekana wanafanya katika wazara tofauti nao wakipata chakula cha mchana.

Hoja ambayo ilikuwa mezani ni nani ambaye anaweza kumdhibiti mwezake kati ya Rais Dr Magufuli au Mwenyekiti wa chama Dr Kikwete.

Katika maongezi yao wawili walikuwa wanamuunga mkono kikwete na watatu wanamuunga mkono Magufuli.

Wanaomuunga kikwete walisema, Kikwete ndiye mwenye chama, anaisimamia serikali yake ambayo ni mtoto kwenye chama, hivyo kama mwenyekiti lazima ahakikishe aliyepewa dhamana ya chama kuongoza serikali anafuata ilani na taratibu za chama.
Wakadai kuwa Mwenyekiti ananguvu ya ushawishi ndani ya chama na kama rais atakwenda kinyume na chama kinavyotaka, mwenyekiti anaweza pitisha azimio la kumwondolea uanachama rais na hivyo kuvuliwa urais, hii ni kutokana na katiba ya chama.

Kwa upande wa waliokuwa wanamtetea rais nao walijuwa na hoja zao nzito.

Walidai kuwa Rais ni mkubwa zaidi ya mwenyekiti wa chama, kwani yeye anaongoza hata wasiokuwa wanachama.

Kulingana na katiba ya nchi rais anaweza hata kumweka kizuizini mtu yeyota hata mwenyekiti wake.
Hivyo Mwenyekiti wa chama hafui dafu kwa Rais.

Kutokana na mjadala ulivyokuwa mkali imebidi niulete humu tuone hoja zikipanguliwa.
 
Mambo ya FB ndani ya JF. Hiyo nani zaidi yako mpelekee Abubakar Sadik pale Radio One, apambanishe Jumapili hii.
 
Mambo ya FB ndani ya JF. Hiyo nani zaidi yako mpelekee Abubakar Sadik pale Radio One, apambanishe Jumapili hii.

mkuu hapa pia ni shule, ndio maana ya jukwaa la siasa, hivyo kama huna cha kuchangiaa kaa kimyaa
 
Mh. Magufuli kwa maili millioni mia nane na zaidi

Hakuna ubishi hapo.

Na bado jipu lako limetumbuliwa unahaha tuuu na bado ibilisi
 
Acha kulimnganisha Mh Dr Magufuli na vitu vya kijinga wewe.

Move yoyote ya kujaribu kumvua Rais uanachama ili asiwe na sifa ya kuwa Rais ni UHAINI

Mh. Magufuli kwa maili millioni mia nane na zaidi

Hakuna ubishi hapo.

Na bado jipu lako limetumbuliwa unahaha tuuu na bado ibilisi

Naomba kujua kiwango cha elimu ya mtoa mada
 
Acha kulimnganisha Mh Dr Magufuli na vitu vya kijinga wewe.

Huyu mleta mada mie ninapata wasi wasi na utimamu
wa akili yake, sijui labda ana dege dege kichwa...
Hivi kama kusoma hujui basi hata kuangalia tu umeshindwa...?
 
Inakuaje mtu au kikundi chawatu wachache wanaamua kumfananisha mh magufuli na vitu vingine vya ajabu...huu nao ni uhaini
 
Back
Top Bottom