Uchaguzi 2020 Rais Magufuli azungumzia wapinzani wanaohamia CCM na kupewa kipaumbele cha uongozi na kugombea

Kashasema atamkata mtia nia yeyote kwa kuangalia jinsi alivyoamka siku hiyo.

Yani si kuangalia katiba, si miongozo, si taratibu, si tamaduni, bali kuangalia anavyojisikia alivyoamka siku hiyo.
Tumerudi rasmi kwenye uongozi wa kichifu
 
Binafsi sioni kosa as far as na wao ni watanzania. Kuwepo vyama vya upinzani haukuwafanyi wao kutopewa kipaumbele pindi wanaporudi CCM.

Kama sio unatetea udhaifu wa Magufuli, basi hujui unachotetea. Huyo mwanaccm aliyekuwa anaalialia anasema mtu anatoka huko atokako, na kuachwa aliowakuta, kisha yeye anapewa nafasi na kupita bila kupingwa.
 
Wenyeji kwisha habari yao...
Wenyeji hawajaisha nao wahame wanang'ang'ania na kulilia liChama mfu kwa niñi? Wao pia Wana haki ya kuhama Chama kama wanaona kinapendelea wa kuja na kuwabagua lakini kama mnashindwa kushinda hukohuko basi hata mtakakohamia mtashindwa na kuanza kulalamà. Bahati mbaya sana wanachama wote wa CCM wanaona Chama hicho ndo Alpha na Omega katika maisha yao. Chama hicho kimepitwa na wakati hadi viongozi wake wanapita majalalani kuokoteza PhD waonekane wamesoma kumbe ni darasa la nne.
 
Binafsi sioni kosa as far as na wao ni watanzania. Kuwepo vyama vya upinzani haukuwafanyi wao kutopewa kipaumbele pindi wanaporudi CCM.
Kosa ni kwamba hakuna mfumo unaoeleweka.

Kwa mfano, hakuna muongozo kwamba teuzi fulani zinataka mtu awe mwanachama wa CCM kwa muda fulani. Au hazijali muda mradi mtu ni mwanachama wa CCM. Au hazijali hata kama mtu ni mwanachama wa CCM.

Katika mfumo kama huo, mteuzi ana uhuru wa kuteua na kutengua vyovyote, kwa jinsi anavyojisikia kaamka siku hiyo.

Na hawa wanachama wa CCM waache kulialia na kufikiri teuzi ni haki yao kwa sababu wao wamekuwa katika chama siku nyingi.

Kwa sababu, mtu anaweza kuwa katika chama siku nyingi, akawa hana sifa, halafu akaja mtu kaingia kwenye chama jana ana sifa zote, akapewa uteuzi.

Uteuzi si zawadi kwa mtu aliyedumu katika chama siku nyingi.

Unatakiwa kwenda kwa mtu mwenye sifa hata kama kaingia kwenye chama muda si mrefu.

Now, whether Magufuli is looking at merit more than seniority is debatable.
 
Sina njaa nimezaliwa ndani ya mfumo mpaka sasa napiga hela za ndani ya mfumo.na wazazi wangu wakistaafu wanalipwa hela za ndani tena mapema sana.
Kwa hiyo unashabikia CCM kwa sababu unapiga hela. Basi mtakuwa wengi wenye mtazamo huo.
 
Binafsi sioni kosa as far as na wao ni watanzania. Kuwepo vyama vya upinzani haukuwafanyi wao kutopewa kipaumbele pindi wanaporudi CCM.
Kwa hiyo waliopo chamani wazuiwe kugombea au kutia nia kwa sababu aliyekuwa mpinzani alikuwa anashikilia jimbo hilo.

Sio kwamba wanatakiwa waweke uwanja sawa.
 
Magufuli anavyofanya si sawa, Silinde hakuchaguliwa na wananchi kwa sababu anapendwa, bali alichaguliwa kwa sababu alikuwa CHADEMA. inatakiwa apambane kupata nafasi ya kugombea sio kupitishwa kihuni huni
 
Binafsi naona ujumbe huu wa CCM ni mzuri sana, kama mtu alikuwa mbunge wa upinzani, mkakubaliana ahame chama chao na kujiunga CCM, lile jimbo ni bora muache huyo huyo aliyehamia CCM agombee, sbb hilo jimbo halikuwa la CCM bali upinzani, huyo Mbunge apewe kipao mbele aendelee kugombea jimbo hilo hilo. CCM kama mlikuwepo miaka yote mlishindwaje hadi jimbo likaenda upinzani? Huyo mbunge wa upinzani akihamia CCM aendelee kugombea bila kupingwa.
 
Rais Magufuli akijibu swali la Sojo"

Kwani mwanamke au mme wako akikosea, siku nyingine akaja kukuomba msamaha kwani utakataa? Siyo ajabu akaja na mapenzi mazuri mazuri kuliko ya zamani amejifunza huko mbinu nyingi na mbadala, Sasa unakataa uhondo huo? Rais amemaliza kwa kusema CCM oyeee

Aisee....!!!
 
Back
Top Bottom