Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Bila kuficha wala kuogopa, kwamba Rais Magufuli alifanya mambo ambayo ni kinyume kabisa na uongozi bora na alikuwa akitupeleka kwenye hali mbaya sana kama taifa la Tanzania. Alikuwa na kauli za kinafiki na hata kuamuru taasisi za serikali kubambikia watu kesi. Kuna mengi sana ambayo yote yakiwekwa wazi hakuna atakaetaka jina la Magufuli lionekane popote nchini, labda hayo mengine tuyaache kwa sasa.
Lakini sasa kazi kubwa anayofanya Rais Samia ni kuturudisha kwenye mstari sahihi wa uongozi kwa maslahi ya Watanzania wote. Rais Samia anastahili pongezi toka kwa kila Mtanzania mwenye akili timamu, sio lawama na shutuma. Wito wangu kwa Raisi Samia ni kuwaondoa au angalau kuwabadilisha kazi viongozi wa taasisi wote waliomtumikia Magufuli katika kutekeleza mambo maovu dhidi ya serikali na wananchi - iwe kwa kuwadhuru watu au kuhujumu mali na fedha za taifa. Nenda mbali zaidi ya Takukuru - angalia pia katika taasisi zote za serikali, za kijeshi na kiraia kutia ndani wakuu wa mikoa na wilaya. Watu hawa wamekosa imani toka kwa wananchi na hawafai tena katika nafasi zao, hawana legitimacy ya kuendelea kushika nafasi walizotumiwa vibaya. Wanaweza kuwa walitumika na si kosa lao la moja kwa moja, lakini kanuni za uongozi zinalazimu waondoke au waondolewe.
Ni vizuri watu wakaelewa haya ili kumwelewa Rais Samia. Haisaidii lolote kuficha ficha mambo. Tuko pamoja nawe Rais Samia, kwa maslahi ya Watanzania na Afrika kwa ujumla. Hongera sana mama, ziba masikio usisikie kelele za vyura wanaodhani watamzuia ng'ombe kunywa maji wakizidisha kelele.