sizzya007
JF-Expert Member
- Mar 15, 2016
- 771
- 2,416
ii ndio aina ya hoja za kuunga mkono uamuzi huo .....
watu wengi wanaojuwa mambo ya nchi na misingi yake aidha wameshikwa na bumbuwazi au wanatazama tu .....wale ambao siku zote mambo ya uzalendo kwao hayana maana ndio wamekuwa wakishangilia ....aina ya watu ambao hata ikitokea vita hawawezi kuipigania nchi yao kama hata misingi yake hawaiheshimu...
wanangojea kushangilia Mwenge kufutwa ...na pengine hata mashujaa tuache kuwakumbuka...ni gharama sana ....tutakuwa tunafanya tukipata pesa .....
wakati nchi ikiwa kati kati ya vita kali ya iddi amin ....maisha yakiwa magumu ..watu wamefunga mkanda haikuweza kuingia akilini kuacha au kuahirisha chochote cha kitaifa
Ndugu philemon habari yako!
Kwanza nianze kwa kukuambia nimekuelewa mno hoja yako, umeiweka clear na kila kitu ni selfexplanatory, ila kuna msingi wa mie binafsi kuzipinga baadhi ya sherehe zinazoendeshwa na serikali hapa nchini kwetu, sherehe hizi nyingi ziligeuzwa miradi ya makada wa chama kile, tende za kugawa skafu, vipeperushi na tenda nyingi zinazihusiana na mambo hayo MAKUBWA KITAIFA zilibakwa na makada wakubwa wa chama kile, haya ni mambo yaliyo wazi na yanajulikana!!
Honestly kwangu mimi kama i have two option between betraying my country or a stranger i have just meet i will have the guts to betray my country, such a choice may be a scandal katika modern society hii ila ndio ukweli. I will tell you why.
Tuianzie hii sikukuu ya mashujaa, hivi kweli sisi tunawaenzi hao mashujaa wetu au tunaigiza tu?! Ni watoto wangapi wanawajua mashujaa wa nchi yao?! Wangapi wanawajua wakina Songera Mbano, Mkwawa, Bibi Titi na wengine kiundani kabisa?! Niambie ni ipi bora kati ya kuchapisha kitabu kimoja chenye mkusanyiko wa mashujaa wetu wote na kuvigawa shule za msingi ili kuwajengea watoto mapenzi na nchi yao na kuwajua mashujaa wao au kufanya sherehe za anasa kila mwaka huku mashujaa hao hawathaminiwi?!
Ndugu ulishawai kutembelea sight zozote za mashujaa wetu?! Mie nimetembelea baadhi, ya Songea (mashujaa wa vita ya majimaji), ya Tabora na ya hapa Dar, mkuu makumbusho zote hizi ni aibu, hamna utunzaji mzuri wa kumbukumbu, zina vumbi, majani yameota hovyo, yani ni uhuni tu, ila eti huwa tuna siku ya kutumia mabilioni ya pesa kwaajiri ya siku hizi. This is insane.
Unazungumzia mashujaa wa vita ya Kagera, ila je una habari kuwa wako wazee maveterani wanaidai serikali pesa (tena ni pesa kidogo kabisa) kwaajiri ya kushiriki vita hivyo?! Kuna umuhimu gani wa kuandaa sherehe kwa mabilioni ya pesa huku tukiwazunguka baadhi ya hao mashujaa ambao bado wako hai kwa kuwapiga chenga ya mwili?!
Tuna mashujaa ambao hatuwathamini na hatuwajali, hii ni fact!!
Nisiandike sana nikakuchosha, ila twende mdomdo i hope and i pray tutafikia sehemu moja ambayo tutastand katika common platform.