Dkt. Mwigulu ataka barabara za uhakika kijijini

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568

Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amesema umefika wakati wa kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuangalia namna ya kutengeneza barabara za zitakazodumu muda mrefu maeneo ya vijijini.

Mwigulu amesema hayo alipojibu hoja ya dharura ya mbunge wa Rorya, Jafar Chege aliyeomba mwongozo wa Spika Tulia Ackson leo Alhamisi Februari 15, 2024 baada ya kipindi cha kuwatambulisha wageni kumalizika bungeni.

Akiomba mwongozo huo, Chege amesema mawasiliano ya barabara katika maeneo mengi nchini yamekatika kutokana mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Amesema Januari 31, 2024, Dk Mwigulu alitoa ahadi kuwa Sh131 bilioni za dharura zitakuwa zimeenda kabla yakumalizika Bunge lakini hadi leo fedha hizo hazijaenda.

Mbali na Chege, wabunge mbalimbali walichangia kuhusu ubovu wa barabara hizo akiwamo wa Mvumi (CCM), Livingstone Lusinde.
 
Back
Top Bottom