Rais Magufuli afuta shamrashamra za Muungano 2016, fedha zikajenge barabara Mwanza

ii ndio aina ya hoja za kuunga mkono uamuzi huo .....
watu wengi wanaojuwa mambo ya nchi na misingi yake aidha wameshikwa na bumbuwazi au wanatazama tu .....wale ambao siku zote mambo ya uzalendo kwao hayana maana ndio wamekuwa wakishangilia ....aina ya watu ambao hata ikitokea vita hawawezi kuipigania nchi yao kama hata misingi yake hawaiheshimu...
wanangojea kushangilia Mwenge kufutwa ...na pengine hata mashujaa tuache kuwakumbuka...ni gharama sana ....tutakuwa tunafanya tukipata pesa .....
wakati nchi ikiwa kati kati ya vita kali ya iddi amin ....maisha yakiwa magumu ..watu wamefunga mkanda haikuweza kuingia akilini kuacha au kuahirisha chochote cha kitaifa

Ndugu philemon habari yako!
Kwanza nianze kwa kukuambia nimekuelewa mno hoja yako, umeiweka clear na kila kitu ni selfexplanatory, ila kuna msingi wa mie binafsi kuzipinga baadhi ya sherehe zinazoendeshwa na serikali hapa nchini kwetu, sherehe hizi nyingi ziligeuzwa miradi ya makada wa chama kile, tende za kugawa skafu, vipeperushi na tenda nyingi zinazihusiana na mambo hayo MAKUBWA KITAIFA zilibakwa na makada wakubwa wa chama kile, haya ni mambo yaliyo wazi na yanajulikana!!

Honestly kwangu mimi kama i have two option between betraying my country or a stranger i have just meet i will have the guts to betray my country, such a choice may be a scandal katika modern society hii ila ndio ukweli. I will tell you why.

Tuianzie hii sikukuu ya mashujaa, hivi kweli sisi tunawaenzi hao mashujaa wetu au tunaigiza tu?! Ni watoto wangapi wanawajua mashujaa wa nchi yao?! Wangapi wanawajua wakina Songera Mbano, Mkwawa, Bibi Titi na wengine kiundani kabisa?! Niambie ni ipi bora kati ya kuchapisha kitabu kimoja chenye mkusanyiko wa mashujaa wetu wote na kuvigawa shule za msingi ili kuwajengea watoto mapenzi na nchi yao na kuwajua mashujaa wao au kufanya sherehe za anasa kila mwaka huku mashujaa hao hawathaminiwi?!
Ndugu ulishawai kutembelea sight zozote za mashujaa wetu?! Mie nimetembelea baadhi, ya Songea (mashujaa wa vita ya majimaji), ya Tabora na ya hapa Dar, mkuu makumbusho zote hizi ni aibu, hamna utunzaji mzuri wa kumbukumbu, zina vumbi, majani yameota hovyo, yani ni uhuni tu, ila eti huwa tuna siku ya kutumia mabilioni ya pesa kwaajiri ya siku hizi. This is insane.

Unazungumzia mashujaa wa vita ya Kagera, ila je una habari kuwa wako wazee maveterani wanaidai serikali pesa (tena ni pesa kidogo kabisa) kwaajiri ya kushiriki vita hivyo?! Kuna umuhimu gani wa kuandaa sherehe kwa mabilioni ya pesa huku tukiwazunguka baadhi ya hao mashujaa ambao bado wako hai kwa kuwapiga chenga ya mwili?!

Tuna mashujaa ambao hatuwathamini na hatuwajali, hii ni fact!!

Nisiandike sana nikakuchosha, ila twende mdomdo i hope and i pray tutafikia sehemu moja ambayo tutastand katika common platform.
 
Tangu tupate uhuru tumeshawahi kubadili namna ya kukumbuka uhuru wetu?? wewe hilo gwaride unaona ni kitu kidogo sana eeh!...kwani wale wananchi wanaokusanyika makao makuu ya wilaya,mikoa,au taifa pale wanafuata chakula eeh...,Tusichukulie mambo kirahisi namna hiyo ..au watu kama nyie ambao wanamshauri bosi kile anachotaka kusikia ....mshauri mzuri lazima atofautiane na wewe ..ukiona una mshauri ambaye kila unachosema ..anaunga mkono ...ujuwe ni tatizo ...ni lazima mara nyingine awe na mawazo tofauti na yako na ayatete mradi awe genuine.....most ya ushauri ninaouona kwenye thread hii uko so genuine ...wala sio ligi.

Huhitaji hata dictionery hata kumjuwa DC aliyeandaliwa kwa ngazi yake kuwa kiongozi .....kama alivyowahi kusema Mwalimu.....rais akitaka anaweza kujeuka kuwa "Mungu" , anapokea mambo mengi mazito ambayo katika ubinadamu wa kawaida unaweza hata kupiga mtu ......lakini lazima awe na shock absorber ...watu wanaomzunguka ambao wanayachuja yale anayofikishiwa naye akiyapata anayachuja kwa utulivu
Sisi tulitaka mabadiliko kuelekea kwenye Tanzania ya kipato cha kati wewe bado unatueletea hadithi ya uhuru.

Tanzania kwa sasa tuko kwenye vita vya kiuchumi wewe bado unatuletea hadithi za vita vya kisiasa.

Tanzania ya sasa na ijayo inafanya maamuzi ya kitaifa kwa kutumia mzani wa kiuchumi na siyo kisiasa.

Kuna faida gani ya kufanya gwaride la kisiasa na kutumia mabilioni ya pesa za watanzania wote wakati watoto wetu hawana hata madarasa, madawati, vitabu na chaki.

Kuna faida gani ya kufanya sherehe kwa gwaride la kisiasa na kuteketeza mabilioni wakati hakuna hata vitanda na madawa kwenye hospitali.

Kuna faida gani ya kufanya sherehe kwa gwaride la kisiasa wakati wananchi vijijini wanatembea makumi kama siyo mamia ya kilometre kwenda kwenye kituo cha afya au zahanati.

Kuna faida gani ya kufanya sherehe kwa gwaride na kutumia mabilioni ya pesa wakati wananchi hawana hata barabara zinazowarahisishia mawasiliano kiuchumi ili kuuza au kununua mazao na vifaa vingine vya kusaidia kukua kwa uchumi kwa haraka.

Hivi unadhani Rais Magufuli hafahamu umuhimu wa Muungano?

Wewe endelea kuishi jana na hadithi za uhuru!

Unashangaza kweli!
 
Sisi tulitaka mabadiliko kuelekea kwenye Tanzania ya kipato cha kati wewe bado unatueletea hadithi ya uhuru.

Tanzania kwa sasa tuko kwenye vita vya kiuchumi wewe bado unatuletea hadithi za vita vya kisiasa.

Tanzania ya sasa na ijayo inafanya maamuzi ya kitaifa kwa kutumia mzani wa kiuchumi na siyo kisiasa.

Kuna faida gani ya kufanya gwaride la kisiasa na kutumia mabilioni ya pesa za watanzania wote wakati watoto wetu hawana hata madarasa, madawati, vitabu na chaki.

Kuna faida gani ya kufanya sherehe kwa gwaride la kisiasa na kuteketeza mabilioni wakati hakuna hata vitanda na madawa kwenye hospitali.

Kuna faida gani ya kufanya sherehe kwa gwaride la kisiasa wakati wananchi vijijini wanatembelea makumi kama siyo mamia ya kilometre kwenda kwenye kituo cha afya au zahanati.

Kuna faida gani ya kufanya sherehe kwa gwaride na kutumia mabilioni ya pesa wakati wananchi hawana hata barabara zinazowarahisishia mawasiliano kiuchumi.

Hivi unadhani Rais Magufuli hafahamu umuhimu wa Muungano?

Wewe endelea kuishi jana na hadithi za uhuru!

Unashangaza kweli

Binafsi hii ndo vita yangu na hizi mambo za mapokeo!! Lazima tujue vipaumbele vyetu kama nchi ni nini, na tuchague kipi tufanye kipi tuache, development expenditure na recurrent expenditure?! Tujenge barabara au zahanati au tutumie tu kwa matumizi ambayo hayatokuja kutulipa in any way whasoever!!

Jamani, tukiambiwa kuthink out of the box ndio huku, ebu tuwe na guts za kujaribu mambo, ebu tuskip hizo sherehe za muungano for one year tu afu tuone pesa za pale tunaweza kuzidirect wapi kwingine, na tuone je ina tija au lah?! Kama itakuwa na tija, wale waliofaidika basi sikukuu ya muungano kwao itakuwa na maana tofauti kwao na wataanza kuienzi vizuri zaidi. TUBADIRIKE JAMANI:mad::mad::mad:
 
Swali zuri sana ulilouliza.

Nami niongezee hivi, huyo Magufuli siyo alitwambia kuwa masuala ya Zanzibar hawezi kuyaingilia kwa kuwa Zenji ni nchi kamili yenye mamlaka yake.

Sasa swali liko hivi, kama Muungano ni wa nchi 2 za Tanganyika na Zanzibar, sasa swala la kuamua kutumia pesa ya Muungano kwa matumizi ya Tanganyika peke yake, je hiyo siyo ubabe na kuingilia mambo ya Zanzibar?
Hoja yako ni ipi hasa. Rais wa Muungano ni nani? Na pesa ya Muungano unayo isema wewe ulitaka ikatupwe katikati ya Bahari ya Hindi? Hivi hujui hata Mwanza ni Jamhuri ya Muungano ? Mi huwa naona kuna watu hamuna haja ya kuchangia ila mnapoteza mda labda kwa vile Mb zina-expire.
 
Kwa vile Tanzania haitasherehekea Uhuru na Muungano basi hakutakuwa na haja ya kusherehekea siku yeyote mwaka huu!!
 
Mi juu ya hili sina jibu ila watu kwenye shere kama hizi walikuwa wanatoka na nyumba na ada za watoto wao. Kubatilishwa sioni kama ni tatizo,tatizo ni kwamba waliozoea kupiga vya juu ambao miongoni mwetu ni wa wale tuliotegemea ukanjanja heshima bado itakuwepi? Tambo zetu kwamba wenzetu wajinga zitakuwepo? Ama ndo hivyo maomboleza
 
Me naona hii inafuta historia za nchi .... Iv ina maana nchi zote zilizoendelea sherehe za kihistoria kama hizi wamezifuta pia?? Then muungano ni wa nchi mbili vipi iweje hiyo hela itumike bara tu visiwani isitumike tuseme ndio hamna matatizo mengi sana,,,,, ni bora iyo bil 1 itumike tanzania bara na nyingine visiwani
 
Binafsi hii ndo vita yangu na hizi mambo za mapokeo!! Lazima tujue vipaumbele vyetu kama nchi ni nini, na tuchague kipi tufanye kipi tuache, development expenditure na recurrent expenditure?! Tujenge barabara au zahanati au tutumie tu kwa matumizi ambayo hayatokuja kutulipa in any way whasoever!!

Jamani, tukiambiwa kuthink out of the box ndio huku, ebu tuwe na guts za kujaribu mambo, ebu tuskip hizo sherehe za muungano for one year tu afu tuone pesa za pale tunaweza kuzidirect wapi kwingine, na tuone je ina tija au lah?! Kama itakuwa na tija, wale waliofaidika basi sikukuu ya muungano kwao itakuwa na maana tofauti kwao na wataanza kuienzi vizuri zaidi. TUBADIRIKE JAMANI:mad::mad::mad:
Kuna baadhi ya watu ambao wao kazi yao ni kupinga kila kitu. Kuna wengine ambao hawajui wanachokipinga na kundi la mwisho ni wanafiki.

Hili kundi la wanafiki ndilo la hatari kwa sababu linachokisema siyo kile linachokifahamu na kukiamini.

Hili kundi la wanafiki ndilo lilikuwa mstari wa mbele likipiga kelele kuhusu reckless and westeful government spending hasa kwenye sherehe za kitaifa. Leo serikali imeamua kukata gharama za sherehe na pesa zake kuzielekeza kwenye matumizi muhimu kulingana na uwezo wa taifa, kwa sasa wanaanza kuja na historia za umuhimu wa sherehe za Muungano kama justification ya hoja zao.

Hawa jamaa wanataka tuendelee kuwa business as usual ndani ya tope!
 
Misingi ya nchi huwa kwenye katiba ...bila hivyo hukika siku vikaja vizazi vikaanza kuona baadhi ya mambo ni ya kipuuzi kadiri ya umri wao....Misingi ya nchi haina mbadala ...na haiwezi tu kufutwa kwa sababu za kishabiki...tuacheni mihemko ..tunakoenda siko...lazima watu waende kwa sheria ..mila na taratibu ..huwezi tu kuamka na kusema ondoa hili ..peleka kule ../leo limekuwa zuri kesho limekuwa baya ...tunatabirika ?

kuna ambao bado wanaongelea juu ya kujitegeemea ...kila mtu anapenda tujitegemea ...tunamuunga mkono kiongozi wetu ..lakini ni wazi na dhahiri kuwa nchi ambayo inategemea wafadhili kwa asiloimia zaidi ya 40% haiamki tu asubuhi na kujitegemea ....tuambiane ukweli kuwa hatuwezi tu kukurupuka kujitegemea .....na kuanza kupayuka ...nendeni tunajitegemea tunajitegemea !!! bado tunahitaji wabia wa maendeleo kwa miaka kadhaa ijayo kabla ya kusimama wenyewe ..
hata kijaana huwa na hamu ya kujitegemea anapokuwa ...ila huwa hatua ..kuazia kujinunulia jozi yake ya viatu ...kumudu seehemu kubwa ya mahitaji..kuhama nyumbani na baadaye kumudu kuwa na familia na mwisho hadi kuweza kusaidia ndugu au wazazi au wahitaji baada ya kupata ziada ....wapo ambao huzeeka bila kufikia ndoto ya kujitegemea..
 
Me naona hii inafuta historia za nchi .... Iv ina maana nchi zote zilizoendelea sherehe za kihistoria kama hizi wamezifuta pia?? Then muungano ni wa nchi mbili vipi iweje hiyo hela itumike bara tu visiwani isitumike tuseme ndio hamna matatizo mengi sana,,,,, ni bora iyo bil 1 itumike tanzania bara na nyingine visiwani
Yaani gwaride, vyakula na vinywaji ndio havifuti historia ya nchi? Ninatumaini unatania!

Kwa hiyo kwa sababu nchi zilizoendelea hazijafuta sherehe kama hizi basi na sisi tufanye kama wao? Kwani hufahamu maana ya nchi zilizoendelea? Au unadhani nchi zilizoendelea ni sawa na Tanzania ambayo watoto wa shule wanalazimika kusomea chini ya miti huku wakiwa wamekaa chini bila madawati.

Kwa kukusaidia iliyofuta/inayofuta historia ya nchi ni ukosefu wa vitabu vya historia, walimu bora na vifaa vingine kwenye mashule ambayo ni sehemu ya kujikumbusha na kujifunza historia ya nchi.

Lastly, sherehe ya Muungano haijafutwa bali imebadilishwa namna ambayo tulizoea kusherekea. Kwa sasa badala ya gwaride, vinywaji na vyakula kwa gharama ya serikali, unaweza kufanya gwaride, ukapika chakula na kununua vinywaji kwa gharama yako.
 
Misingi ya nchi huwa kwenye katiba ...bila hivyo hukika siku vikaja vizazi vikaanza kuona baadhi ya mambo ni ya kipuuzi kadiri ya umri wao....Misingi ya nchi haina mbadala ...na haiwezi tu kufutwa kwa sababu za kishabiki...tuacheni mihemko ..tunakoenda siko...lazima watu waende kwa sheria ..mila na taratibu ..huwezi tu kuamka na kusema ondoa hili ..peleka kule ../leo limekuwa zuri kesho limekuwa baya ...tunatabirika ?

kuna ambao bado wanaongelea juu ya kujitegeemea ...kila mtu anapenda tujitegemea ...tunamuunga mkono kiongozi wetu ..lakini ni wazi na dhahiri kuwa nchi ambayo inategemea wafadhili kwa asiloimia zaidi ya 40% haiamki tu asubuhi na kujitegemea ....tuambiane ukweli kuwa hatuwezi tu kukurupuka kujitegemea .....na kuanza kupayuka ...nendeni tunajitegemea tunajitegemea !!! bado tunahitaji wabia wa maendeleo kwa miaka kadhaa ijayo kabla ya kusimama wenyewe ..
hata kijaana huwa na hamu ya kujitegemea anapokuwa ...ila huwa hatua ..kuazia kujinunulia jozi yake ya viatu ...kumudu seehemu kubwa ya mahitaji..kuhama nyumbani na baadaye kumudu kuwa na familia na mwisho hadi kuweza kusaidia ndugu au wazazi au wahitaji baada ya kupata ziada ....wapo ambao huzeeka bila kufikia ndoto ya kujitegemea..
Soma yanayojiri nchi zilizoendelea, punguza kukariri. Patriotism haiji kwa kukusanyika national stadium, kupiga gwaride na kunywa soda;

Celebrate Independence Day in the US.

Independence Day is a day of family celebrations with picnics and barbecues, showing a great deal of emphasis on the American tradition of political freedom. Activities associated with the day include watermelon or hotdog eating competitions and sporting events, such as baseball games, three-legged races, swimming activities and tug-of-war games.

Many people display the American flag outside their homes or buildings. Many communities arrange fireworks that are often accompanied by patriotic music. The most impressive fireworks are shown on television. Some employees use one or more of their vacation days to create a long weekend so that they can escape the heat at their favorite beach or vacation spot.

Independence Day is a patriotic holiday for celebrating the positive aspects of the United States. Many politicians appear at public events to show their support for the history, heritage and people of their country. Above all, people in the United States express and give thanks for the freedom and liberties fought by the first generation of many of today's Americans. The Statue of Liberty is a national monument that is associated with Independence Day.
 
Mkuu respect Mimi ningemshauri magu hiyo bil 2 moja ingekwenda zenji na iliyobaki ndio ingekwenda mwanza. Huu ni muungano sio 9 Dec.
Unajuaje kuna hela ilitoka Zanzibar katika bilioni 2 zilizotengwa awali kwa maandalizi?

Nyerere alisema kuna siku Tanganyika mtapata Yeltsin wenu atadai Tanganyika, ndio Magufuli amewasili.

Kama ambavyo Magufuli akiwa waziri kuna mambo alikuwa akiyaangalia hana jinsi lakini yanamkera, lingine ndio kama huu Muungano, kama una uchungu wa dhati na nchi hii lazima Zanzibar ikuume, kwamba wanatunyonya sana lakini there is no one doing anything about it. Magufuli ndani ya moyo wake anajua vyema kwamba Zanzibar is a colossal waste of time and resources.

Magufuli please futa Muungano wa kijinga huu!
 
Hili ni jambo jema na zuri sana.

Sioni kabisa tatizo lililopo hapo na kama ingekuwa mimi ningechukua uamuzi huo huo kama wa Magufuli.
Km ingekuwa wewe?
Teh teh teh.
We mjakazi wa mtu una uamuzi utakaotoa ktk maisha yako?

We utatumikishwa na hao wazungu mpk siku wanakuzika na huo ujauzito wako.
Magufuli anaua nchi we unampigia Vigelegele?

Nyie kina mama wazee mna shida sana kwa kweli.
Duh
 
Napenda matokeo ya uamuzi huu, lakini nadhani jamaa hakushauriwa vizuri katika jamii tete kama ya hii ya Tanganyika+Zanzibar. Ingekuwa vizuri kama sehemu ya fedha hizo zingejenga barabaraba Mwanza na sehemu nyingine ikajenga barabara Zanzibar kwenye ule mtaaa lilipo ghorofa la fatuma karume. Sijajua yule dada fatuma aliyekuwa anapiga mawakili mahakamani wakati baba yake akiwa madarakani atasemaje kuhusu hili, kwani bado anatamani baba yake awe madarakani kusudi awe ananyang'anya viwanja vya makanaisa bila karaha.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom