Rais Magufuli afuta shamrashamra za Muungano 2016, fedha zikajenge barabara Mwanza

Rais Magufuli hana sura ya muungano kabisaa.Alighairisga semina elekezi kwa bunge .Hela zote zikamalizikia muhimbili utadhan zanzibar sisi tuna hospitali ya mtakatifu Thomas.Ameghairisha sherehe za muungano na kuelekeza fedha hizo zitumike kwa kutengeneza bara bara za Tanganyika .Jiandae kupata upinzani mkubwa usio utarajia huko mbeleni
 
Soma yanayojiri nchi zilizoendelea, punguza kukariri. Patriotism haiji kwa kukusanyika national stadium, kupiga gwaride na kunywa soda;

Celebrate Independence Day in the US.

Independence Day is a day of family celebrations with picnics and barbecues, showing a great deal of emphasis on the American tradition of political freedom. Activities associated with the day include watermelon or hotdog eating competitions and sporting events, such as baseball games, three-legged races, swimming activities and tug-of-war games.

Many people display the American flag outside their homes or buildings. Many communities arrange fireworks that are often accompanied by patriotic music. The most impressive fireworks are shown on television. Some employees use one or more of their vacation days to create a long weekend so that they can escape the heat at their favorite beach or vacation spot.

Independence Day is a patriotic holiday for celebrating the positive aspects of the United States. Many politicians appear at public events to show their support for the history, heritage and people of their country. Above all, people in the United States express and give thanks for the freedom and liberties fought by the first generation of many of today's Americans. The Statue of Liberty is a national monument that is associated with Independence Day.


umeona hapo wamesema as per american tradition ...si wamekubaliana ....,mimi sina tatizo na uamuzi wowote wa magufuli ambao unagusa wananchi kupitia katiba au sheria zilizotungwa na wananchi wao...ili mradi tu awashirikishe .....hakuna tatizo....
Hata hii ambayo imekuwa kawaida ya kuhamisha matumizi bila kushirikisha wawakilishi wao ...ni bora tu tuamue ku suspend bunge kwa miaka hii mitano tutaokoa pesa nyingi ...zaidi kama kazi zao zinafanywa na executive basi wao wanaenda dodoma kufanya picnic.......ukizingatia kuwa hata watakachosema ..hakifiki kwa watu
Kuanzia bunge hili ...watarekodi wenyewe na wao ndio watagawa clips kwa media ......kama uamuzi wa Nape aliosema juzi utatekelezwa .....wanasema tbc inatumia bilioni 4.2 kuonyesha bunge live peke yake ...wakati ambapo TV kama ITV na star hazifikishi kutumia kwa pamoja hata milioni 500 kurusha bunge live kwa mwaka ......this is stalinist !!! work up !
 
Rais Magufuli hana sura ya muungano kabisaa.Alighairisga semina elekezi kwa bunge .Hela zote zikamalizikia muhimbili utadhan zanzibar sisi tuna hospitali ya mtakatifu Thomas.Ameghairisha sherehe za muungano na kuelekeza fedha hizo zitumike kwa kutengeneza bara bara za Tanganyika .Jiandae kupata upinzani mkubwa usio utarajia huko mbeleni

Mimi nafikiri zanzibar wasimame kusema kama kwenye hiyo 2 billion wao walikuwa wameweka ngapi ?? sherehe za kumwapisha shein ziligharamiwa na nani..?uchaguzi wa marudio aligharamia nani??mishahara toka mwaka jana na kuendelea atagharamia nani??
with all odds naona kudeka kwa Zanzibar kutafika mwisho ...kwa huyu Mzinza wa Geita .
 
Hatuna bunge, tuna wachumia tumbo tu. Rais na mawaziri wake watengeneze bajeti na kuitekeleza. Tumewakubali. Bunge livunjwe tu kwa kuwa haliaminiki tena. Spika Ndugai anawezaje kuwaweka wabunge wenye vituo vya mafuta kwenye kamati ya nishati na madini? Conflict of interest aliikanyigiaje chini?Hao watakuwa wamemhonga ili kulinda maslahi yao.! And they have the temerity to request that EWURA be disbanded just because they were fined for adulterating fuel and selling export fuel within the country! Rais kamata spika na hiyo kamati yote.
Bunge linatia kinyaa mfano mwenyekiti wa kamati anakua na elimu ya darasa la saba, unategemea nini apo? Jamaa amewaweka washkaji zake kwenye kamati na siasa kibao kaingiza.
 
Mimi nafikiri zanzibar wasimame kusema kama kwenye hiyo 2 billion wao walikuwa wameweka ngapi ?? sherehe za kumwapisha shein ziligharamiwa na nani..?uchaguzi wa marudio aligharamia nani??mishahara toka mwaka jana na kuendelea atagharamia nani??
with all odds naona kudeka kwa Zanzibar kutafika mwisho ...kwa huyu Mzinza wa Geita .
Iliochangia ni serikali ya muungano .KAma kuna serikali nyengine isiokua ya muungano basi ijitokeze "Tanganyika "Wazi wazi isijifiche.Hata hivyo hapa umeweka wazi kua munatutawala???kama si nyinyi Jecha asingeweza kurudia uchaguzi au sio??? Sasa
Weka sababu kwanini mututAwale wakati hatuchangii zaidi ya hasara??
 
Hajawahi kufuta Tukio
Lolote la kitaifa na Hana Ubavu huo!

ungesema ukweli ameahirisha kama ilivyotangazwa !

Pesa yenyewe hakuna ! Kuficha aibu ya zanzbaris
 
Huu sasa ugomvi pesa ya sherehe ya muungano inaenda kunufaisha upande mmoja tu ?vipi huku mchambawima?Ami Magu usifanze hivyo yakhe Shein ni nduguyo hivyo hebu mpe pande nae a mdorishe Seif!
 
Unajuaje kuna hela ilitoka Zanzibar katika bilioni 2 zilizotengwa awali kwa maandalizi?

Nyerere alisema kuna siku Tanganyika mtapata Yeltsin wenu atadai Tanganyika, ndio Magufuli amewasili.

Kama ambavyo Magufuli akiwa waziri kuna mambo alikuwa akiyaangalia hana jinsi lakini yanamkera, lingine ndio kama huu Muungano, kama una uchungu wa dhati na nchi hii lazima Zanzibar ikuume, kwamba wanatunyonya sana lakini there is no one doing anything about it. Magufuli ndani ya moyo wake anajua vyema kwamba Zanzibar is a colossal waste of time and resources.

Magufuli please futa Muungano wa kijinga huu!

Napingana na hapo kwa kutaka muungano ufutwe, binafsi kw upeo wangu bado sijaiona sababu ya kuufuta muungano!!

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar si wa kwanza duniani!! Muungano huu ndio historia harisi ya hii tunayoiita Tanzania, sehemu kubwa ya historia ya nchi hii, shida ambazo ziko ndani ya muungano wetu huu ni shida za kawaida na zinatatulika, inahitaji serikali serious kidogo kuzitatua zile kero za muungano, na hatujawai kuwa na serikali serious toka mwaka 1984. Muungano inabidi umpate mtu kivuruga kidogo, and i think Magu is, mie antiCCM ila huyu Magu ni aina ya kiongozi tulihitaji kwa kipindi kirefu.
 
Iliochangia ni serikali ya muungano .KAma kuna serikali nyengine isiokua ya muungano basi ijitokeze "Tanganyika "Wazi wazi isijifiche.Hata hivyo hapa umeweka wazi kua munatutawala???kama si nyinyi Jecha asingeweza kurudia uchaguzi au sio??? Sasa
Weka sababu kwanini mututAwale wakati hatuchangii zaidi ya hasara??

Kaka sisi wenyewe matatizo yetu yanamtosha magufuli ..nina mashaka kama atakuwa na muda wa kubishana ..ukizingatia yule hata hicho kiswahili cha kubishana hakijui ....you better come into your sense atawatosa ...read the signs on the walls .....kikwete mumempeleka peleka sana ....
Hamjasikia kawaambia muende mahakamani .........
Tangu ateuliwe anakuja amekuja zanzibar mara mbili tu tena kisela ....na shughuli ikiisha huyoo airport ....yuko busy ...hana muda wa kubakia overnight kuangalia chokocho ...na taarab asilia
 
Sisemi anapendelea kwao, lakini hizo pesa angezielekeza kwenye barabara ya matope inayotoka Nangurukuru hadi Liwale ambako tumeoneshwa kwenye tv watu wakiteseka kutokana na ubovu wa barabara. Au kutoka Nyakanazi hadi Kasulu basi!
Magufuli hatokei Mwanza.. Anatokea Mkoa wa Geita, wilaya ya chato.. So anapendelea nini hapo? Plus Kama ungekuwa umefika Mwanza ungeelewa kero ya hiyo barabara asubuh na jioni. Nani huko Nyakanazi ndio wapi vile?
 
Kwanini iende Zenj wakati gharama hizo zinatoka hazina Dar?

Sherehe zingekuwepo Zanzibar wasingehusika na gharama! iweje zikifutwa wahusishwe na mgao?
Kama zanzibar hatuchangii kitu zaidi ya hasara kwanini munain'gan'gania ni ajabu kweli kweli
 
Huu muungano si wa nchi mbili? Hao upande wa zanzibar nao wamenufaika vipi kwa kuhairishwa hizo sherehe?

Muungano huu ulikofikia JPM asingeweza kutengeneza hotuba, ikaeleweka,.. Utaeleza nini kwenye jukwaa kama Wazanzibar hawawezi kufanya uchaguzi ukaheshimika.
 
Misingi ya nchi huwa kwenye katiba ...bila hivyo hukika siku vikaja vizazi vikaanza kuona baadhi ya mambo ni ya kipuuzi kadiri ya umri wao....Misingi ya nchi haina mbadala ...na haiwezi tu kufutwa kwa sababu za kishabiki...tuacheni mihemko ..tunakoenda siko...lazima watu waende kwa sheria ..mila na taratibu ..huwezi tu kuamka na kusema ondoa hili ..peleka kule ../leo limekuwa zuri kesho limekuwa baya ...tunatabirika ?

kuna ambao bado wanaongelea juu ya kujitegeemea ...kila mtu anapenda tujitegemea ...tunamuunga mkono kiongozi wetu ..lakini ni wazi na dhahiri kuwa nchi ambayo inategemea wafadhili kwa asiloimia zaidi ya 40% haiamki tu asubuhi na kujitegemea ....tuambiane ukweli kuwa hatuwezi tu kukurupuka kujitegemea .....na kuanza kupayuka ...nendeni tunajitegemea tunajitegemea !!! bado tunahitaji wabia wa maendeleo kwa miaka kadhaa ijayo kabla ya kusimama wenyewe ..
hata kijaana huwa na hamu ya kujitegemea anapokuwa ...ila huwa hatua ..kuazia kujinunulia jozi yake ya viatu ...kumudu seehemu kubwa ya mahitaji..kuhama nyumbani na baadaye kumudu kuwa na familia na mwisho hadi kuweza kusaidia ndugu au wazazi au wahitaji baada ya kupata ziada ....wapo ambao huzeeka bila kufikia ndoto ya kujitegemea..

Hapo kwenye red hapo, je si katiba hiyo hiyo unayoizungumzia ambaye inampa raisi nguvu ya kutengua siku na kuteua sikukuu za umma?!

Siku ya muungano HAIJAFUTWA, ila kilichofanyika ni kuiadhimisha kwa namna tofauti tu.
 
Hapana sijasema 'hasara' Nimesema ZNZ huwa haichangii na huo ni ukweli.

Ili pesa iwe ya Muungano sio lazima Zanzibar ichangie.

Hapo ndipo makosa yanapoanza.
Vipo vyanzo vingi vya mapato ambavyo ni vya muungano.

Chukua mfano mikopo au misaada toka nchi za nje. Deni la taifa ni la Tanzania (muungano).

Ushuru wa forodha ni muungano matter. So pesa zinazotokana hapo ni za wate.

Tume ya pamoja ya fedha ilianzishwa ili kuweka sawa mambo haya, ingawa bado haijafanya kazi yake kwa ukamilifu.
 
Hizi ni Sherehe za kuadhimisha siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mbona mgao umejikita upande mmoja tu wa Muungano? Kwa mkwamo wa kisiasa tulio nao sasa hapa Zanzibar, ingependeza serikali ikazingatia namna ya kuridhisha na wananchi wa upande wa pili. Pamoja na hayo nayapongeza hayo maamuzi.
 
Back
Top Bottom