Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Heeeeeee bhanya bhabya ketaaaaaa🤪🤪🤪🤪🤪, ujinga na upuuzi mtupu. Kumpa mkopo ndo tiketi ya kumtesa na malipo madg ya mshaharaa?

Lisu alisema "TUNA RAISI WA AJABU, NARUDIA TENA, TUNA RAISI WA AJABU SIJAWAHI KUONA"

leo nimekubali, kweli TUNA RAISI WA AJABU SANAAAAAAAAAAAAA. full stop.
 
Sasa wangekuwa wanalipwa wangekimbia?
Inawezekana wanalipwa vizuri lakini mazingira yote ya kazi hayafai, ukitembelewa na DC , Waziri, Katibu mwenezi unaanza kuulizwa maswali kama mtoto na ukimkera kwa majibu hata kama upo sawa unawekwa ndani saa 48. Kuna watu walikuwa wanaondoka private sector na kwenda serikalini sio tu kwa kufuata malipo mazuri lakini kwa sababu mbali mbali kama :

1. Frusa za kujiendeleza kimasomo.
2. Usalama wa kazi (Job Security) na kuheshimiwa.
3. Manufaa kama bima ya afya, nyumba ya kuishi etc.
4. Muda rafiki wa kufanya kazi.

Je hivyo vitu navyo vimeboreshwa au ni mwendo wa bakora tu.
 
Huu ni upumbavu, Rais lazima asaidiwe na wasaidizi wake.....kauli zake za siku hizi hata chekechea anashangaa. Kuwekeana masharti mtu anatafuta maisha yake ni ujinga, ajirini wengine wapo mtaani kibao tu...........what if alijisomesha mwenyewe hakutumia huu mkopo ambao umeturudisha kwenye Ukoloni aliopambana nao Nyerere.
Hata kama alisomeshwa na serikali, bado ana uhuru wa kuchagua. By the way, huko private bado ana tibu Watanzania hao hao. Na analipa mkopo wake hakupewa bure.
Huyu baba sasa atafutiwe jina..
 
Kule hawatibu watu ?

Wanadaiwa ?, Wamelipa hawajalipa ?, kuliko kufungia hospital / mtu anayetibu watu pia ni rahisi sana kwenye mkataba wa mkopo waseme kwa miaka kadhaa lazima ufanye kazi ya serikali sehemu yoyote utakayopelekwa (hapo mtu anakuwa anabanwa kwa mkataba) sio aina hii ya sheria / maamuzi kutoka kwenye kinywa cha mtu
Lbd anatibu kuku, alafu et hana uzalendo. Hiv huyu mzee anaujua uzalendo kweli?? Kwani huyo daktari amekimbilia malawi kuwatibu wamalawi au ? Raisi mjinga kweli huyu. Anazeeka vibaya kweli. Nahis bora m7 anajua kuchanganua mambo💥
 
Hapo weka kama 40% makato maana yake take home ni almost laki saba.

Kodi ya nyumba, umeme, maji, fuel (kama ana gari), ada ya watoto, chakula cha familia, kufanya maendeleo etc.

Lazima mtu upagawe.
20210130_125001.jpg
 
Rais Magufuli leo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma?, hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”-JPM

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”-JPM

My take:
Kuna maslahi madogo hasa ya kimshahara katika utumishi wa serikalini, naomba serikali iongeze mishahara kwa watumishi ili kuepukana na changamoto hii. La sivyo serikali itaendelea kupoteza mapato kwa watu kukimbia utumishi wa umma serikalini.
 
Kuna watu/ wafanyakazi wakienda masomoni, wanawekeana bond na mwajiri/ serikali tena kwa viapo mbele ya shahidi mwana sheria kuwa akimaliza masomo lazima arudi hapa kwenye kituo cha kazi afanye kazi miaka mitano ndipo ahame kutafuta marisho ya kijani ama aendelee pale. Na wanafanya hivi kwa sababu mfanyakazi wao huyo anakuwa analipwa mshahara akiwa kwenye likizo ya masomo. Sasa akimaliza masomo na akasema anatafuta marisho ya kijani mbuga nyingine, bond inamlazimisha kulipa gharama/ stahiki zote alizolipwa akiwa masomoni.

Tukirudi kwa ndugu yetu daktari. Je. Alikuwa na bond na serikali !?
Daktari aliyeajiriwa mwaka Jana kwa ajira za kutafutia kura kabond lini na serikali?
 
Mengine watu washaongea uwezi kwenda kufungua hospitali kubwa kila sehemu, kuna maeneo hayana motisha kwa wafanyakazi kuishi hasa medical consultants.

Binafsi nimetabiri hospitali inayojengwa Chato itashushwa hadhi soon as Magufuli leaves office, kwa sababu Chato sio sehemu ya kuweka consultants.

Ni bora waiongeze ukubwa hospitali ya Geita mjini ije kuwa ya kanda the area as the right population density na ni mji mkubwa. Lakini Chato bora wajikite na hospitali ya wilaya I do not see senior consultants wenye demand kubwa ulimwenguni kuishi Chato.
Hili waimba mapambio watakutoa macho.
 
Back
Top Bottom