Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Wafanye kama Cuba wanaingia nao mkataba mapema ni waajiriwa wa serikali wanapopokea mkopo wa masomo tu.

Ukienda kufanya kazi private hiyo hospitali inabidi iingie mkataba na serikali yao na kuwalipa asilimia kadhaa ya mshahara wako kila mwaka. Brazil na Venezuela wanaotegemea madaktari wa Cuba ndio wanavyofanyiwa.

Ikitokea daktari bingwa ndio kabisa yaani wakusomeshe, wakupe na experience mpaka uitwe bingwa mtu anaemtaka lazima alipe dau kubwa zaidi; that’s how Cuba manages to keep their highly skilled Drs wanaopokea mishahara midogo compared to the world.
 
Hapa Rais wangu unakosea, tuweke sawa sentensi tunakopeshwa hizo fedha hatupewi bure kwa hiyo tunajisomesha kikubwa mkopo unarejeshwa?

habari ya mimi nafanya kazi wapi haikuhusu, hata wewe uliacha ualimu ukaenda bungeni ulifuata maslahi unalalama uraisi ni kazi ngumu lakini huachi kisa maslahi.

huu mwaka wa ngapi huongezi mshahara tunafanyaje?
 
Unasema vipi daktari pesa kala wakati ni mkopo ulimpa? halafu hiyo mikopo haiwezi kuwazuia watu kutafuta maslahi mazuri zaidi, kwanza mikopo yenyewe mmeweka riba ili kuzidi kuwakamua, wacha wakimbie.
Ukiwauliza ajira wanasema hamsomi ili muajiriwe na serikali pekee jiajirini au mtafute ajira kwingine. Mkijitafutia ajira mnaambiwa serikali iliwasomesha. Basi serikali iajiri wasomi wote wenye mikopo!!
 
Mengine watu washaongea uwezi kwenda kufungua hospitali kubwa kila sehemu, kuna maeneo hayana motisha kwa wafanyakazi kuishi hasa medical consultants.

Binafsi nimetabiri hospitali inayojengwa Chato itashushwa hadhi soon as Magufuli leaves office, kwa sababu Chato sio sehemu ya kuweka consultants.

Ni bora waiongeze ukubwa hospitali ya Geita mjini ije kuwa ya kanda the area as the right population density na ni mji mkubwa. Lakini Chato bora wajikite na hospitali ya wilaya I do not see senior consultants wenye demand kubwa ulimwenguni kuishi Chato.
 
Huu ni upumbavu, Rais lazima asaidiwe na wasaidizi wake.....kauli zake za siku hizi hata chekechea anashangaa. Kuwekeana masharti mtu anatafuta maisha yake ni ujinga, ajirini wengine wapo mtaani kibao tu...........what if alijisomesha mwenyewe hakutumia huu mksector nopo ambao umeturudisha kwenye Ukoloni aliopambana nao Nyerere.
Mkuu hata kama angekuwa amesomeshwa kwa mkopo,hata huko private bado anahudumia walipa kodi wa nchi hii
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom