Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
2,639
2,000
20210130_120616.jpg
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”.

20210130_170545.jpg
20210130_170548.jpg
 

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
14,317
2,000
Rais lazima asaidiwe na wasaidizi wake kauli zake za siku hizi hata chekechea anashangaa. Kuwekeana masharti mtu anatafuta maisha yake ni ujinga, ajirini wengine wapo mtaani kibao tu. what if alijisomesha mwenyewe hakutumia huu mkopo ambao umeturudisha kwenye Ukoloni aliopambana nao Nyerere.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,377
2,000
Kule hawatibu watu?

Wanadaiwa? Wamelipa hawajalipa? kuliko kufungia hospital/ mtu anayetibu watu pia ni rahisi sana kwenye mkataba wa mkopo waseme kwa miaka kadhaa lazima ufanye kazi ya serikali sehemu yoyote utakayopelekwa (hapo mtu anakuwa anabanwa kwa mkataba) sio aina hii ya sheria / maamuzi kutoka kwenye kinywa cha mtu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom