Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Kwani waajiriwa private sector hawarejeshi mikopo waliyopewa? Huko private hospital anawatibu warundi au watanzania? Kwani private hospital wanapata madaktari toka nje ya nchi au hao hao waliopewa mikopo na serikali?
 
Heeeeeee bhanya bhabya ketaaaaaa🤪🤪🤪🤪🤪, ujinga na upuuzi mtupu. Kumpa mkopo ndo tiketi ya kumtesa na malipo madg ya mshaharaa?

Lisu alisema "TUNA RAISI WA AJABU, NARUDIA TENA, TUNA RAISI WA AJABU SIJAWAHI KUONA"

leo nimekubali, kweli TUNA RAISI WA AJABU SANAAAAAAAAAAAAA. full stop.
Umeshawahi kusikia kitu kinaitwa ‘restrictive covenant’ kwenye mkataba wa ajira?

Sijui kama madokta Tanzania wana hiyo clause kwenye mkataba wao wa ajira but that is normal practice kwenye taasisi nyingi duniani hata huko ulaya depending umeajiriwa katika nafasi gani.

Kuna sehemu ukitaka kuacha kazi inabidi uwalipe fidia kubwa au mkataba uliokuwa nao una kuzuia kufanya kazi kwenye hiyo field bila ya ridhaa ya mwajiri.

Hakuna cha ajabu alichoongea Magufuli, that is normal.
 
Mkuu kasahau kua yeye alikimbia ualim akaingia kwenye siasa , daaah kwel Hii Nchi inazidi kua ngumu
 
Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri wa Afya Dkt Dorothy Gwajima, kuhakikisha anawafuatilia madaktari walioacha kazi katika hospitali ya rufaa mkoa wa Tabora kwa sababu ya maslahi na kuhamia hospitali binafsi na ikiwezekana afungiwe yeye pamoja hospitali aliyoikimbilia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 30, 2021, wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika hospitali hiyo na kwamba haiwezekani serikali ipoteze pesa kwa ajili ya kusomesha madakatari na wao badala ya kuwatumikia wananchi wanaanza kuwa wabinafsi kwa kutaka maslahi makubwa.

"Mfuatilie huyo daktari aliyekimbia hapa, uifuatilie na hiyo hospitali ikiwezekana tunamfungia huyo daktari na tunaifungia na hiyo hospitali aliyoenda kutibia ili watu waanze kujifunza kwamba wizara ya afya siyo ya kuchezea tu, unamsomesha mtu kwa fedha za watanzania halafu anasema maslahi madogo", amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Dkt. Magufuli, "Madaktari wote wanapata mkopo kwa asilimia 100, unasoma pale kwa miaka mitano ukishatoka pale unasema maslahi madogo, si ungekimbia wakati unasoma hela yetu umekula halafu unasema maslahi madogo, nia ya serikali ni kuboresha maslahi lakini unaanza na kimoja, unaboresha maslahi wakati huna majengo wala vifaa vya kutosha".
 
Umeshawahi kusikia kitu kinaitwa ‘restrictive covenant’ kwenye mkataba wa ajira?

Sijui kama madokta Tanzania wana hiyo clause kwenye mkataba wao wa ajira but that is normal practice kwenye taasisi nyingi duniani hata huko ulaya depending umeajiriwa katika nafasi gani.

Kuna sehemu ukitaka kuacha kazi inabidi uwalipe fidia kubwa au mkataba uliokuwa nao una kuzuia kufanya kazi kwenye hiyo field bila ya ridhaa ya mwajiri.

Hakuna cha ajabu alichoongea Magufuli, that is normal.
Hiyo hufanyika kwenye seriously private institutions, but kwenye ile form ya mkopo haina vipengele hivyo mkuu! Na hiyo serikal yetu hakuna vipengele kama hivyo. Mbona walimu weng sana wanahamia huku private schools na hakuna wa kulalamika🤫💥
 
Hili waimba mapambio watakutoa macho.
Ukweli ni mchungu kumeza. Daktari bingwa sio mtu mdogo halafu umpeleke kijijini you are not serious.

Huko UK kwenyewe south-east nzima yenye miji kama kumi mikubwa hospitali ya kanda moja tu University Hospital London.

Sio rahisi kusambaza madaktari bingwa kama Magufuli anavyoongea yeye akifika sehemu pandisha hadhi hii iwe hospitali ya hadhi fulani, unao hao wataalamu wa kusambaza kama unavyopondisha hadhi kirahisi rahisi.
 
Tunakoelekea mikopo itawekwa masharti ya "lazima kufanya kazi serikali"
Mbona kila Leo vijana wanaaswa kujiajiri?!
Hapa ni wito wa Waziri mkuu:
 
Hela za Buree hizii zinaanza kuleta maafa...!! Enzi hizo Madr walikuwa wanapewa Grant au msaada kwa jina lingine na masharti yake lazima ufanye kazi serikalini kwa muda flani kurudisha fadhila.. sasa huyu Dr vimeumanaa..
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
Sasa mkuu hospitali aliyoenda mnaifungia kwa lipi ? kwa roho zako mbaya kama hizi ndio maana watu wengi hawaamini kama wewe ni mtanzania .

Madaktari chungu mzima hawana kazi si wapeni hiyo nafasi muachane na huyo aliyehama , mbona ni rahisi tu !
 
Back
Top Bottom