Rais Kikwete nchi imemshinda mwanzo mwisho

Rais Kikwete nchi imemshinda mwanzo mwisho

Hakuna utawala ambao umasikini umeongezeka kwa kasi kubwa kwa wananchi kama huu utawala Jakaya Mrisho Kikwete
wewe faizFoxy kama unaishi maisha mazuri mshukuru Mungu huko vijijini watu wanateseka sana mtu anatumia 2000 kwa siku nzima kulisha familia ya watu 6 bado nyie mnakuja hapa JF kujigamba tumsifu raisi kwa lipi .

Emma kweli wewe ni mtumwa!hutakaa uone maendeleo
ya nchi yako labda utawaliwe na Malaika!
 
Miundombinu ni mzee nkapa. Yeye zaidi kazalisha madeni makubwa sekta ya miundombinu. Ni shidaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaamen.

Najua unakataa kwa njee lakini Moyo wako unakiri mafanikio yaliyofanywa na Jk
na hizi kelele zote ni ili muonewe huruma mnafikiri
Ikulu wanaingia wachovu kwi kwi kwi kwi!
 
Najua unakataa kwa njee lakini Moyo wako unakiri mafanikio yaliyofanywa na Jk
na hizi kelele zote ni ili muonewe huruma mnafikiri
Ikulu wanaingia wachovu kwi kwi kwi kwi!
pesa za Escrow hazikuwa za umma .JK
ndo mafanikio hayo hongera raisi wetu
 
Yaani hii mada inanipa machungu nikifikiri jinsi leo nilivyobadili safari huku nikiwa nimeaga nyumbani kuwa naenda Kampala kununua bidhaa lakini nilipokaribia Geita rafiki yangu akanipigia simu na kunieleza shilingi imeshuka vibaya sana na inaelekea kuwa sawa na shilingi ya Uganda. Nimegeuza Mwanza kula ugali.
 
Attachments

  • 1435172321799.jpg
    1435172321799.jpg
    49.7 KB · Views: 111
2005 Kilo ya sukari ilikuwa 800TSH leo 2000TSH cement imepanda zaidi, mabati karibu kila kitu kimedouble Shiling inaanguka kwa kasi ya kutisha nchi inawaza kukopa tu.madini yanatoroshwa et kenya ndo wanauza tanzanite zaidi kuliko tanzania bado ss tunaendelea kucheka tu Polen
 
Acha uongo wewe ndio hujui. Kwanza hujui hata aliyemwachia nchi, ni mkapa. Aliachiwa akiba ya miezi 8 yeye jk hataacha hata ya mwezi mmoja.

Kikwete anatuachia Gas cubic feet zaidi ya trillion 55 na bado utafiti unaendelea mpaka mwakani tutakuwa tunaongelea cubic feet zaidi trillion 100, hiyo ni bora kuliko akiba yoyote uijuayo kwa sasa.

Leta ushahidi wa hiyo akiba ya miezi minane aliyoacha Mkapa na ukshindwa ujuwe wewe ni muongo.
 
2005 Kilo ya sukari ilikuwa 800TSH leo 2000TSH cement imepanda zaidi, mabati karibu kila kitu kimedouble Shiling inaanguka kwa kasi ya kutisha nchi inawaza kukopa tu.madini yanatoroshwa et kenya ndo wanauza tanzanite zaidi kuliko tanzania bado ss tunaendelea kucheka tu Polen

Nenda tu hapo Karagwe uone wahaya wanavyotorosha Tin kwenda Rwanda, na utasikia Rwanda + Congo ndio nchi zinazochimba Tin kwa wingi, kumbe wala Rwanda haipo kwenye ramani...!!
 
umasikini wa leo umevunja rekodi za duniani umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana bora maraisi wote waliotangulia kuongoza

Huna haya wala haujuwi vibaya, hujawahi kukaa foleni ya chakula, nguo, nyama, sabuni, sukari Tanzania hii, ungewahi usingeyasema hayo. Basi hata hawajakuhadithia umasikini huo ulikuwa awamu ipi? Tuulize tulioishi kwenye umasikini huo, miaka michache tu iliyopita.
 
Hakuna utawala ambao umasikini umeongezeka kwa kasi kubwa kwa wananchi kama huu utawala Jakaya Mrisho Kikwete
wewe faizFoxy kama unaishi maisha mazuri mshukuru Mungu huko vijijini watu wanateseka sana mtu anatumia 2000 kwa siku nzima kulisha familia ya watu 6 bado nyie mnakuja hapa JF kujigamba tumsifu raisi kwa lipi .

Wewe mimi nnakaa kijijini utanieleza nini?

Huyo anaeishi hivyo amma ni mvivu wa kutupwa amma ni mgonjwa amma kipato cha mavuno anakimalizia kwenye pombe. Maana hawa watu wa vijijini siku zote wanakunywa pombe za kienyeji lakini wakishauza mavuno hujidai kufakamia ma beer. Tunayajuwa ya vijijini, leo hii utajiri 80% wa Tanzania upo vijijini kama haujuwi hayo.

Usiniletee story za vijijini, wakati huko mijini kuna watu hawataki kufanya kazi na kutwa kazi yao kupiga wenzao "mizinga" na au kuwa matapeli.

Tanzania hii leo mpaka Mchina anakuja anaiona fursa iliyopo kwenye kuuza karanga mitaani na mi Tanzania kibao inaomba-omba na hawaioni hiyo fursa, unataka kusema nini wewe? Labda ujidanganye na wajinga wenzio. Umasikini wa Tanzania upo kwenye vichwa vya Watanzania (superficial) siyo real.
 
Nimejaribu kufuatilia kwa makini na hatua kwa hatua tangu huyu mzee aingie madarakani ili nibaini ni kipi ametenda hata tumkumbuke baada ya kuondoka kwake madarakani Octoba 2015. Nimegundua kwa 97% mkuu wa kaya ameshindwa vibaya mno kuleta MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA aliyotuahidi.

Mh.MKAPA alimwambia nakuachia Nchi kama ni Ndege wakati huo ilikuwa iko kwenye RUNNING,Alichopaswa kufanya ni kuipaisha tu ili ikifika Octoba ili ndege hio itue ikiwa imesheheni unono na urojorojo, Uchumi ulioimara kwa kila MWANANCHI. BADALA YAKE NDEGE HIO JK ALIIZIMA,

Tumaini la Wananchi likapotea, kila kitu kikavurugika:-

-Mfumko wa bei kwa BIDHAA zote ukawa juu.

-Shillingi yetu ikaporomoka kwa KASI MPYA,NGUVU MPYA na ARI MPYA.

-Tatizo la umeme mpaka kesho ni kitendawili Nchini.

-Ujambazi umerudi kama ilivyokuwa zama za kale hadi Polisi wanauawa na silaha kuibiwa VITUONI.

-Ziara za nje ya Nchi za kutembeza BAKULI LA OMBA OMBA (BLO)Awamu ya nne inaongoza kwa safari zenye kulitia hasara Taifa letu.

-Waandishi wa Habari na Wanaharakati kuuawa na kuteswa.

-Umwagaji damu usio wa lazima kutokea kwenye maandamano.

-Ajali na ongezeko la vifo na vilema vimekithiri awamu ya nne.

-Mikataba mingi inayohusu RASILIMALI ZETU imesainiwa kwa SIRI na WACHINA bila Raia kujua kinachoendelea ndani yake.

-KATIBA PENDEKEZWA ni kiini macho uhalisia UMEENGULIWA na BATILI imewekwa mbele.

-DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA -Uandikishwaji wake unacheleweshwa kwa MAKUSUDI.

-Hata ndani ya CCM uchaguzi wa kumpata Mgombea Urais hali ni tete mpaka leo.

Kwa uchache tu haya ni baadhi ya mambo yanayoonesha kuwa NCHI IMEMSHINDA JK MWANZO MWISHO.

RAIS ajaye anatakiwa awe ngangari kweli kweli la sivyo JAHAZI LITAZAMA.

Kama hukunufaika ni wewe tu coz mie Liz moko na Dogo sila wa haji mbona tuko njema sana tu!
 
Huna haya wala haujuwi vibaya, hujawahi kukaa foleni ya chakula, nguo, nyama, sabuni, sukari Tanzania hii, ungewahi usingeyasema hayo. Basi hata hawajakuhadithia umasikini huo ulikuwa awamu ipi? Tuulize tulioishi kwenye umasikini huo, miaka michache tu iliyopita.

Aiseee mbona unareply kikoloni hivi?
 
Kikwete anatuachia Gas cubic feet zaidi ya trillion 55 na bado utafiti unaendelea mpaka mwakani tutakuwa tunaongelea cubic feet zaidi trillion 100, hiyo ni bora kuliko akiba yoyote uijuayo kwa sasa.

Leta ushahidi wa hiyo akiba ya miezi minane aliyoacha Mkapa na ukshindwa ujuwe wewe ni muongo.

Jaribu kuwa makini kidoooogo.
 
Tulibugi sana.
Natoa mwito kwa watanzania wenzangu tuwe makini kuchagua kiongoz anayetufaa.
 
Back
Top Bottom