Rais Kikwete nchi imemshinda mwanzo mwisho

Rais Kikwete nchi imemshinda mwanzo mwisho

Faiza Foxy lete utetezi wako hapa naona kwa style hii koo lako limekabwa hatakuongea itakuwa shida sasa na mikono yako imetiwa ganzi jibu la maana huna tena.

Ushabiki tu,
unachoshangaa nini?
Nchi kuwa na deni kuna Tatizo gani?
Nitafutie nchi yoyote duniani ambayo haidaiwi
Anzia Marekani! Ukiipata njoo na hoja yako hii hii
uliyoitoa Buguruni team!
 
#kwahii nchi ni baba yako??

Babu yako ni Mnyarwanda,Baba yako ni Mtusi,wewe ni Banyamlenge utakuwa na mzigo na Nchi yetu kweli?
Huna fungu wala sehemu TANZANIA rudi msituni ukapigane na kufia porini.

USITUPUMBAZE HII NCHI NI YETU SOTE KAMA WEWE HAIKUHUSU KAA KANDO.
 
fanya kazi acha kulalamika lalamika tunutu weweeee

KAZI NILIYONAYO MIMI NI YA UHAKIKA,itakugharimu ujaliwe na MOLA miaka mia tatu ya kuishi katika Sayari hii ndio huenda UKAFANIKIWA KUWA NA AJIRI KAMA YANGU.
Sio kila anayezungumzia mambo ya Taifa letu basi,ndio kakosa kazi ya kufanya.
PANUA WIGO WA KUFIKIRI,YAONE MAMBO KWA PICHA KUBWA.
 
Nimejaribu kufuatilia kwa makini na hatua kwa hatua tangu huyu mzee aingie madarakani ili nibaini ni kipi ametenda hata tumkumbuke baada ya kuondoka kwake madarakani Octoba 2015. Nimegundua kwa 97% mkuu wa kaya ameshindwa vibaya mno kuleta MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA aliyotuahidi.

Mh.MKAPA alimwambia nakuachia Nchi kama ni Ndege wakati huo ilikuwa iko kwenye RUNNING,Alichopaswa kufanya ni kuipaisha tu ili ikifika Octoba ili ndege hio itue ikiwa imesheheni unono na urojorojo, Uchumi ulioimara kwa kila MWANANCHI. BADALA YAKE NDEGE HIO JK ALIIZIMA,

Tumaini la Wananchi likapotea, kila kitu kikavurugika:-

-Mfumko wa bei kwa BIDHAA zote ukawa juu.

-Shillingi yetu ikaporomoka kwa KASI MPYA,NGUVU MPYA na ARI MPYA.

-Tatizo la umeme mpaka kesho ni kitendawili Nchini.

-Ujambazi umerudi kama ilivyokuwa zama za kale hadi Polisi wanauawa na silaha kuibiwa VITUONI.

-Ziara za nje ya Nchi za kutembeza BAKULI LA OMBA OMBA (BLO)Awamu ya nne inaongoza kwa safari zenye kulitia hasara Taifa letu.

-Waandishi wa Habari na Wanaharakati kuuawa na kuteswa.

-Umwagaji damu usio wa lazima kutokea kwenye maandamano.

-Ajali na ongezeko la vifo na vilema vimekithiri awamu ya nne.

-Mikataba mingi inayohusu RASILIMALI ZETU imesainiwa kwa SIRI na WACHINA bila Raia kujua kinachoendelea ndani yake.

-KATIBA PENDEKEZWA ni kiini macho uhalisia UMEENGULIWA na BATILI imewekwa mbele.

-DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA -Uandikishwaji wake unacheleweshwa kwa MAKUSUDI.

-Hata ndani ya CCM uchaguzi wa kumpata Mgombea Urais hali ni tete mpaka leo.

Kwa uchache tu haya ni baadhi ya mambo yanayoonesha kuwa NCHI IMEMSHINDA JK MWANZO MWISHO.

RAIS ajaye anatakiwa awe ngangari kweli kweli la sivyo JAHAZI LITAZAMA.
Nyota ya jk itawatesa sana mwaka huu hata mfanye ni mazuri ya jk hamuwezi kuyafunika jipangeni tena.

Uongozi wa jk umekuwa wa manufaa siku zote kwenye nyanja zote za maisha,

Wapo wehu wachache wanajaribu kumchafua jk lakini wameshindwa kamwe.
 
KAZI NILIYONAYO MIMI NI YA UHAKIKA,itakugharimu ujaliwe na MOLA miaka mia tatu ya kuishi katika Sayari hii ndio huenda UKAFANIKIWA KUWA NA AJIRI KAMA YANGU.
Sio kila anayezungumzia mambo ya Taifa letu basi,ndio kakosa kazi ya kufanya.
PANUA WIGO WA KUFIKIRI,YAONE MAMBO KWA PICHA KUBWA.

Acha mipasho na taarabu hapa
kazi ni ya kwako inatuhusu nini rudi kwenye mada
au unasema nini?Jk ni kamanda na hilo liko wazi!
 
iiiishiii huyu mgambo nae kawaje tena??
 
Yote kwa yote ila kuna mambo anastahili pongezi kwa upande wangu,kama miundombinu.
.....ingawa ukienda kwa kina, kubwa, kama tungeelewa ni 'katiba mpya', sababu tatizo letu kubwa ni mfumo unaotupa aina ya viongozi wengi wao wakiwa wababaishaji, wapigaji,wabinafsi, na wajanjawajanja ( waliojazana serikalini na ktk vyama vyote vya siasa)....ni kweli "kanali",kiuongozi dhaifu, ingawa ndio, ni mzalendo na mwenye uzoefu,suala lisilo na ushahidi kuhusu "upigaji" libaki majungu ya kisiasa mpaka likithibitishwa kisheria...!.....na pia ndio, na mengine mengi yamefanyika, lkn ni kwa wale wenye kuijua tanzania ilivyokuwa..na ilivyo..
 
Nyota ya jk itawatesa sana mwaka huu hata mfanye ni mazuri ya jk hamuwezi kuyafunika jipangeni tena.

Uongozi wa jk umekuwa wa manufaa siku zote kwenye nyanja zote za maisha,

Wapo wehu wachache wanajaribu kumchafua jk lakini wameshindwa kamwe.

Ni nyota ama Nyongo???

labda useme NYONGO YA JK INATUTESA SAANA HAPO NITAKUBALIANA NAYE 100%.
 
Acha mipasho na taarabu hapa
kazi ni ya kwako inatuhusu nini rudi kwenye mada
au unasema nini?Jk ni kamanda na hilo liko wazi!

mie nilimjibu IKISIMAMA PANDA,Wewe umekurupuka acha mihemko,uwe makini,Hata hivyo tangu lini JK ni kamanda?

Lini alivua gamba na kuvaa gwanda???
wee bado kinda kwenye siasa tulie ujifunze kwa wengine.
Madhaifu ya kikwete ni mengi kuliko maelezo.
 
KAZI NILIYONAYO MIMI NI YA UHAKIKA,itakugharimu ujaliwe na MOLA miaka mia tatu ya kuishi katika Sayari hii ndio huenda UKAFANIKIWA KUWA NA AJIRI KAMA YANGU.
Sio kila anayezungumzia mambo ya Taifa letu basi,ndio kakosa kazi ya kufanya.
PANUA WIGO WA KUFIKIRI,YAONE MAMBO KWA PICHA KUBWA.

sasa mbona unaonekana kama mlalamishi lalamishi sana?
 
mie nilimjibu IKISIMAMA PANDA,Wewe umekurupuka acha mihemko,uwe makini,Hata hivyo tangu lini JK ni kamanda?

Lini alivua gamba na kuvaa gwanda???
wee bado kinda kwenye siasa tulie ujifunze kwa wengine.
Madhaifu ya kikwete ni mengi kuliko maelezo.

sasa unatuambie sisi ili iweje kwani?,...uende ushitaki kwa babako....sie tuko busy tunatafuta hela.....
 
sasa unatuambie sisi ili iweje kwani?,...uende ushitaki kwa babako....sie tuko busy tunatafuta hela.....

Ulalamishi wangu u wapi?
Kusema RAIS KIKWETE NCHI IMEMSHINDA MWANZO MWISHO haya ndio yamegeuka kuwa malalamishi kwako???
Umevimbiwa na kutafuta fedha na kiburi kimejaa iko siku utajaujua ukweli wa mambo.
 
Nyota ya jk itawatesa sana mwaka huu hata mfanye ni mazuri ya jk hamuwezi kuyafunika jipangeni tena.

Uongozi wa jk umekuwa wa manufaa siku zote kwenye nyanja zote za maisha,

Wapo wehu wachache wanajaribu kumchafua jk lakini wameshindwa kamwe.

Sidanganyiki2015 liked this.......sisiemu bwana.....
 
Ni nyota ama Nyongo???

labda useme NYONGO YA JK INATUTESA SAANA HAPO NITAKUBALIANA NAYE 100%.

Kikwete huwezi mnanisha na yeyote wa kabla yake, mfupa uliowashinda wote wa kabla yake, Kikwete kauavuruga vuga kulaini kabisa.

Nyerere, life expectancy miaka 38, changanya na Mwinyi na Mkapa ikafika 48 kwa jumla ya miaka 44 ya utawala wao, Kikwete pekee katupaisha mpaka miaka 62 na hiyo ni hesabu ya mwaka 2012.

Inakueleza nini hiyo?
 
Ulalamishi wangu u wapi?
Kusema RAIS KIKWETE NCHI IMEMSHINDA MWANZO MWISHO haya ndio yamegeuka kuwa malalamishi kwako???
Umevimbiwa na kutafuta fedha na kiburi kimejaa iko siku utajaujua ukweli wa mambo.

Imemshinda kwa lipi? wakati huu wa Kikwete Tanzania imepaa katika nyannja zote kuliko wakati wowote wa kabla yake.

Tuanze moja moja hapa tuone ukweli ukoje. Tuanze na Rais yupi tumlinganishe nae? tuanze na wa awamu ya kwanza, Nyerere.

Tuanze na life expectancy ya Mtanzania kwa miaka 24 ya Nyerere alipopewa nchi ilikuwa ngapi na alipowachia madaraka kaiwacha ngapi? na Kikwete alipopewa nchi ilikuwa ngapi na mpaka sasa iko ngapi?

Wacha porojo.
 
Back
Top Bottom